Thursday, February 10, 2022

Tanzia - Dr. MweleNtuli Malecela

 



Dr.  Mwele Ntuli Malecela  1963-2022

Nimepokea kwa huzuni na masikitiko habari ya kifo cha dada yangu wa Ubatizo Dr. Mwele Ntuli Malecela.  Amefariki Geneva, Switzerland jana.  Alikuwa na sumbuliwa na ugonjwa wa Kansa tangu mwaka 2019.   Kwa maneno yake mwenyewe..kansa iligundulika ikiwa tayari imekwisha sambaa mwilini.

Wakati wa kifo chake, Dr. Malecela, alikuwa anafanya kazi World Health Organization, kama Mkurugenzi wa Udhibiti wa  Magonjwa ya Yasiopewa Kipaumbele.  Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti za Kiafya Tanzania (NIMRI). 

Tanzania na Africa kwa ujumla imepata hasara. Tumempoteza mtaalamu aliyeboboea katika fani yake.

Poleni sana familia ya Malecela.  Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.


Kwa  habari zaidi BOFYA HAPA

No comments: