Mwanahistoria na Mtembeza Watalii maarufu, "Professor" Samahani Kejeri, amefariki dunia, leo Februari 13, 2022, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu ya kansa.
Binti yake, Furaha Kejeri amethibitisha habari hiyo, Mazishi yatafanyika kesho, Jumatatu, Februari 14, 2022 nyumbani kwa marehemu, Magomeni, Bagamoyo. (Siyo Magomeni ya Dar es Salaam)
Prof. Kejeri alipewa jina la "Professor" kutokana na ufahamu wake wa Historia ya Bagamoyo. Alikuwa anatunza vitabu, "friend books" ambazo zimesainiwa na watu ambao aliwatembeza Bagamoyo. Mimi mwenyewe nilikutana naye mara la kwanza mwaka 1988, nikiwa mwanafunzi wa Tanzani School of Journalism. Tulienda Bagamoyo kwenye Field Trip na alitutembeza na kutoonyesha sehemu muhimu za kihistoria ya Bagamoyo ikiwemo "hanging tree" ambako wajerumani walikuwa wananyonga weusi.
Prof. Kejeri pia aliigiza katika sinema Maangamizi the Ancient One kama Mganga Simba Mbili. Sinema hiyo ilikuwa ya kwanza kutoka Tanzania kuwa katika mashindano ya Academy Awards (Oscars) Hollywood.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin
No comments:
Post a Comment