Showing posts with label Kibodya. Show all posts
Showing posts with label Kibodya. Show all posts

Monday, April 14, 2008

Msiba - Mzee Kibodya


Tunawaarifu msiba mzito uliotokea Dodoma, Tanzania, kwa kufiwa na baba yetu mzazi Alhaj mzee Abdallah Mkambavange Kibodya (pichani) aliyefariki dunia leo Jumapili tarehe 13 April 2008.

Mazishi yatafanyika huko Dodoma, Tanzania Jumatatu tarehe 14 April,2008 baada ya salat Asr.
Kwa hapa Marekani kilio kiko nyumbani kwa bwana Isaac Kibodya:
7 Upper Church Street,
Apt # 213
West Springfield,
Mass 01089

Kwa kutoa mkono wa pole tafadhali wasiliana na wafiwa:

Isaac Kibodya 413.209.8666 (nyumbani) 413.219.1153 (simu ya mkono)
Ahmad Mkambavange Kibodya 413.221.2935 (simu ya mkono)
Mohamed Kibodya 413.273.4591 (simu ya mkono)
Omar Kibodya 413.330.2007 (simu ya mkono)
Khalfan Kibodya 44.780.961.7416 (simu ya mkono)
Msemwa Kibodya 214.916.0879 (simu ya mkono)
Zainab Kibodya 832.208.0316 (simu ya mkono)
Albert Kiputa 413.208.0033 (simu ya mkono)
Severine Kiputa 413.306.2109 (simu ya mkono)

Saturday, September 08, 2007

Hafla ya Kumpongeza Dada Asha Rose Migiro New York






(All Photos courtesy of Issac Kibodya)
Kumbukumbu ya hafla ya Dr. Asha Rose Mtengeti Migiro ilofanyika Pelham, New York kumkaribisha Marekani na kupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa tarehe 25 Agosti 2007.

Monday, June 18, 2007

Lady Diana Kibodya Asherekea 50th Birthday!

Lady Diana witnessed the murder of Hector Pieterson by racist police.
Lady Diana Kibodya receives well wishes from a guest. A South African Guest leads a South African Dance


Lady Diana joins in a South African Song

Springfield Tanzanian Dance Group


Lady Diana Kibodya, alisherekea miaka 50 toka azaliwe katika Party kabambe iliyofanyika Springfield, Massachusetts siku ya jumamosi, juni 16. Ndugu na marafiki walitoka sehemu mbalimbali kusherekea naye.

Party ilifunguliwa kwa wageni kuimba wimbo wa taifa wa Afrika Kusini, (nkosi sikelel iAfrika) na wimbo wa taifa wa Tanzania. Asili yake Lady Diana ni Afrika Kusini. Pia walitoa shukrani kwa nchi ya Tanzania kusaidia sana katika ukombozi wa Afrika Kusini na hasa kutoa hifadhi kwa wakimbizi. (Mnakumbuka makambi ya Dakawa na Mazimbu?) Kwa kifupi wanafunzi waliandamana kupinga kufndishwa kwa lugha ya makaburu ya Afrikaans. Waliandamana kwa amani lakini polisi mbaguzi alianza kufyatua risasi ndipo vijana 20 walipoteza maisha yao.

Lakini watu wengi hasa vijana waliohudhuria sherehe hiyo walipatwa na butwa kusikia habari zake. Karibu kila mtu alijua kuwa asili yake ni Afrika Kusini. Lakini hawakujua kuwa alishuhudia kijana, Hector Pieterson mwenye miaka 12, alivyopigwa risasi na askari wa kibaguzi wa Afrika Kusini. Picha ya tukio hiyo ilisambazwa kwa wageni (picha ya kwanza kabisa).
Mume wake, Lady Diana, Bwana Isaac Kibodya, alisoma risala ambayo ilisimulia historia ya mke wake, na watu wengi walishikwa na machozi. Baada ya Hector kuuwawa, askari wa BOSS (polisi wa kikatili) walianza kusaka wanafunzi hao. Ilibidi wakimbie nchi yao kwa kutembea hadi Swaziland kwa mguu. Alisema kuwa wanafunzi wengine hawakufanikiwa kutoroka, lakini yeye alifanikiwa kufika Swaziland, halafu alipelekwa Uganda, na hatimaye Tanzania.

Tanzania alisoma Chuo cha Waandishi wa Habari, na Chuo cha Ustawi wa Jamii. Alikutana na mume wake, Isaac Kibodya, mwaka 79. Bwana Kibodya alifurahisha watu alivyosema, " Diana alikuja kwenye birthday party yangu ya kusherekea miaka 23, toka skiu hiyo alikuwa wangu!"

Lady Diane alikuja Marekani kusoma mwaka 1985, New Hampshire. Hivi sasa anakaa Springfield, Massachusetts na familia yake. Lady Diana na mume wake wana watoto wanne na mjukuu moja wa kiume.

Mungu ambariki Lady Diana na aweze kusherekee 'birthdays' nyingi zaidi.

Kwa habari zaidi ya SOWETO UPRISING someni: