![]() |
| Inabidi Ukalie |
![]() | |||||||||||
| Ukismama juu ya Choo Kinavunjuka |
Blogs in Kiswahili, the main African language of EAST AFRICA.





Wadau, hapa Marekani watu hawawezi kuishi bila toilet paper. Na nasema hivyo kwa sababu mwaka 1999, watu walienda dukani na kuzoa toilet paper zote kwa sababu kulikuwa na uzushi kuwa mwaka 2000 toilet paper itakuwa adimu. Haikutokea.



Kama mnavyofahamu kununua gauni ya arusi ni ghali. Kumbe si lazima ununue gauni kwa bei ya juu wakati unaweza kutengeneza na kitu ambacho bei ni rahisi kidogo tena ukitumia coupon ni bei rahisi zaidi.
Hapa Marekani ukienda dukani kununua toilet paper kuna kila aina. Kuna Charmin, kuna double ply, kuna quilted, zenye michoro na ngumu na laini. Mwaka jana kulikuwa na mashindano ya kutengeneza gauni ya arusi na Toilet paper baadala ya kitambaa. Ila nauliza hivi, ukitoka majasho hiyo gauni haitayeyeyuka huko umeivaa. Maana Toilet paper inaanza kuharibika (disintergrate) mara mkitia maji!
Hizi ni baadhi ya picha zilizoshinda. Kuona design zingine bofya hapa: