Showing posts with label Toilet. Show all posts
Showing posts with label Toilet. Show all posts

Saturday, February 20, 2021

Mwanamke Ang'atwa Takoni na Bear Akijisaidia Chooni Alaska


Huko Alaska, Mwanamke ameng'atwa na mnyama aina ya Bear, akiwa anajisaidia kwenye choo cha shimo iliyokuwa nje ya nyumba alifikia. 

Bi Shannon Stevens anasema alienda kujisaidia chooni kwenye giza.  Alipokaa kwenye choo akasikia maumivu makali baada ya kung'atwa matakoni!  Alipiga kelele kuomba msaada.  Ndugu yake alirudi na tochi na kukuta bear yuko ndani ya shimo ya choo!  

Waliaamua kukimbilia mjini. Waliporudi asubuhi walikuta bear huyo kaondoka.  Bi Shannon hakuumia sana na madakatri wanasema atakuwa mzima,.

*************************


 ANCHORAGE, Alaska (AP) — An Alaska woman had the scare of a lifetime when using an outhouse in the backcountry and she was attacked by a bear, from below.

“I got out there and sat down on the toilet and immediately something bit my butt right as I sat down,” Shannon Stevens told The Associated Press on Thursday. “I jumped up and I screamed when it happened.”

Stevens, her brother Erik and his girlfriend had taken snowmobiles into the wilderness Feb. 13 to stay at his yurt, located about 20 miles northwest of Haines, in southeast Alaska.

Her brother heard the screaming and went out to the outhouse, about 150 feet (45.72 meters) away from the yurt. There, he found Shannon tending to her wound. They at first thought she had been bitten by a squirrel or a mink, or something small.

Erik brought his headlamp with him to see what it was.

“I opened the toilet seat and there’s just a bear face just right there at the level of the toilet seat, just looking right back up through the hole, right at me,” he said.

“I just shut the lid as fast as I could. I said, ‘There’s a bear down there, we got to get out of here now,’” he said. “And we ran back to the yurt as fast as we could.”

Once safely back inside, they treated Shannon with a first aid kit. They determined it wasn’t that serious, but they would head to Haines if it worsened.

“It was bleeding, but it wasn’t super bad,” Shannon said.

The next morning, they found bear tracks all over the property, but the bear had left the area. “You could see them across the snow, coming up to the side of the outhouse,” she said.

They figure the bear got inside the outhouse through an opening at the bottom of the back door.

“I expect it’s probably not that bad of a little den in the winter,” Shannon said.

Alaska Department of Fish and Game Wildlife Management Biologist Carl Koch suspects it was a black bear based upon photos of the tracks he saw and the fact that a neighbor living about a half mile away sent him a photo of a black bear on her property two days later.

That homeowner yelled at the bear but it didn’t react. It also didn’t approach her but lumbered about its business, like it was in a walking hibernation mode.

Even though it’s winter, Koch said they get calls all year round about bears being out.

And 2020 was a record year for general bear problems in the Haines area. Reasons for that, he said, could include the fact it was a poor salmon run year combined with a mediocre berry crop. “It is also possible a bear couldn’t put on enough fat when they go in the den, that they might be out and about more often or earlier,” he said.

Koch suspects Shannon’s wound was caused by the bear swatting at her with a paw rather than being bitten. Either way, the location might be a first.

“As far as getting swatted on the butt when you’re sitting down in winter, she could be the only person on Earth that this has ever happened to, for all I know,” Koch said.

No matter the season, Erik says he’ll carry bear spray with him all the time when going into the backcountry, and Shannon plans to change one behavior as well.

“I’m just going to be better about looking inside the toilet before sitting down, for sure,” she 

Monday, August 01, 2016

Maandalizi ya Chakula Kutoka Mazingara Machafu!

Mnaopenda Kula restaurants, na chakula cha caterers..
halahala! Hizo kuku ziliingia kwenye michuzi, supu, roast, nk.  Halafu unashangaa Kwa nini tumbo inauma na unaharisha kesho yake.

Saturday, July 11, 2015

Jinis ya Kutumia Choo cha Kizungu


Inabidi Ukalie

Ukismama juu ya Choo Kinavunjuka       



Wednesday, April 07, 2010

Kutozwa Mapesa Kwenye Ndege Inazidi... Sasa Hata Kutumia Choo!

Haya, leo tumesikia kuwa tutatozwa hela kwa ajili ya 'carry on' bag kwenye Spirit Airlines. Mjue na airlines zingine zitaiga! Haya sasa Ryan Air wanasema utatozwa hela kutumia choo kwenye ndege! Jamani, sasa kama mtu kambanwa, ndo akae nayo mpaka ndege itue! Hii sasa ni uchu wa pesa!

Kaa habari zaidi:

http://www.cnn.com/2010/TRAVEL/04/07/ryanair.lavatory.fee/index.html?hpt=T2

http://www.latimes.com/business/la-fi-spirit7-2010apr07,0,5945292.story?track=rss

Thursday, January 14, 2010

Kula Chakula kutoka Kwenye Choo!

Hizi picha ni kutoka Modern Toilet Restaurant huko Taipei, Taiwan. Viti vya kukalia ni vyoo vya kizungu. Napkins ni toilet paper, meza ni bathtubs. Hebu mtazame hizi picha. Mimi mwenyewe natamani kutapika nikiwaza kula kula chakula hapo. Wateja 100 wanaweza kuingia kwa mpigo.









Wednesday, January 06, 2010

Wimbo wa Chooni



Huyo Dada ana hits zaidi ya milioni tatu huko YOU TUBE! Watu hapa wanasema sasa kila wakienda chooni wataimba wimbo huo. OFFICIAL TOILET SONG!

Saturday, November 21, 2009

Siku ya Choo Duniani - World Toilet Day





Siku ya Alhamisi ilikuwa siku ya choo duniani. Ilikuwa siku ya kutambua umuhimu wa kutumia choo, kuwa na choo kisafi, na hata kuwa na choo. Nchi zingine watu hawana choo wanajisaidia wanapojiweza. Ni kero, hasa sehemu zingine Africa na hata Bongo unatembea njiani na kukutana na kinyesi cha binadamu, au unakuta sehemu inanuka mikojo, kumbe ndo 'unofficial' choo cha wanaume! Wanaume wanajisaidia haja ndogo popote bila aibu.
Kwa habari zaidi tembelea: http://www.worldtoiletday.com/

Friday, November 13, 2009

Kuchimba Dawa Safarini Mkoani

Siku hizi Tanzania kuna tangazo kwenye TV la TIGO. Jamaa yuko kwenye basi ya mkoani kwenda songea. Wanasimama kuchimba dawa na yeye anaachwa. Anamtumia jamaa text message kwenye basi na wanamrudia.

Kwenye basi la kwenda Kyela, tulisamama mara kadhaa ili watu waweze kuchimba dawa. Tulisamama Kitonga Mountain Resort, kwenye kituo cha mafuta na kuna vituo vya kuchimba dawa porini. Chini ni picha ya kituo fulani huko Iringa. Mnashuka mnaingia bush. Hebu ona toilet paper zilivyozagaa.





Monday, September 08, 2008

Choo cha Kizungu



Wadau, watu wengi wa third world (dunia ya tatu) wamezoea vyoo vile vya kiasia na vya shimo, au kuchimba dawa porini. Sasa wakikutana na hivi vyoo vya kizungu badala ya kuikalia wanaipanda halafu ndo wanachuchumaa. Matokeo yake ni kuwa lundo unaishia kwenye choo, kwenye miguu au kwenye sakafu. Kwa kweli ni balancing act ya hali ya juu kusimama kwenye choo cha kizungu halafu kulenga!

Sehemu nyingi hapa Marekani zenye watu kutoka nchi za Third World siku hizi wanajaribu kuwaelimisha hao wageni wa hvyo vyoo hata kabla ya kuondoka nchini mwao. Hata kwenye ndege za kimataifa siku hizi kuna kideo cha kuwaelimisha.

Saturday, May 10, 2008

Ukiweka Maiti Kwenye Choo Atafufuka!


Hii sasa ni vituko vya vituko! Huko Wisconsin polisi wamekuta maiti ya Bi kizee mwenye miaka 90 ikiozea kwenye choo ndani ya nyumba.
Huyo bibi alikuwa anakaa na mama moja, Tammy Lewis (pichani) na wanae wawili. Yule bibi alifariki ndani ya nyumba yao. Alivyofariki badala ya kuita polisi yule mama mwenye nyumba alipiga simu kwa askofu wake. Askofu kamwambia aweke maiti ya huyo Bi kizee kwenye choo na atafufuka.

Miezi miwili ilipita na maiti ilianza kuoza kwenye hicho choo. Jana, polisi walienda kwenye hiyo nyumba kumtafuta yule bibi kizee maana alikuwa hajaonekana muda mrefu. Kufika walisikia harufu mbaya. Ndo walikuta maiti ya huyo bibi.

Sasa hiyo nyumba ina choo kimoja. Hao walikuwa wanajisaidia wapi? Na walikuwa wanaoga wapi? Na

Samahani lakini kuna kitu gani kwenye maji huko! Kule si ndipo yule Peter Kupaza alipomwua ndugu yake baada ya kumtia mimba!


**************************************

Necedah, Wisconsin - Two children and their mother are said to have lived for about two months with the decaying body of a 90-year-old woman on the toilet of their home's only bathroom.

Wisconsin authorities say a religious "superior" had claimed the corpse would come back to life.
The children, ages 15 and 12, cried hysterically after a deputy who came to the home looking for the woman ordered them out because of the stench from the body.

The children are in foster care. Their mother and a self-described "bishop" remain in custody on felony counts of being a party to causing mental harm to a child.

Kusoma habari kwa kirefu Bofya hapa:

Tuesday, April 15, 2008

Acheni Tabia Mbovu - Part 2


Bado nakemea vikali hiyo tabia mbaya ya wanaume kujisaidia hapa na pale bila hata kujali nani anapita au watoto watacheza hapo!
Picha kwa hisani ya Mzee wa Sumo

Choo Chako


CHOO CHAKO NI KIPIMO HALISI CHA AFYA YAKO


Kabla hujapatwa na matatizo makubwa ya kiafya, kuna dalili ambazo hujionesha wakati unapokwenda kujisaidia haja kubwa ama ndogo, dalili ambazo mara nyingi huzijui kuwa ni kiashiria kwamba una tatizo la kiafya.


Katika makala ya leo, tutaangalia aina kadhaa za choo ambazo huashiria kuwa unaupungufu wa aina moja au zaidi ya chakula fulani, au mwili wako unahitaji aina moja au zaidi ya chakula ili kuleta uwiano katika mwili wako.Labla kabla sijaanza moja kwa moja kutaja aina hizo za choo (haja kubwa), ningependa kutoa dokezo moja kuhusu dalili zinazojionesha wakati tunapojisaidia haja ndogo, lakini tunashindwa kutambua ni dalili ya kitu gani. Haja ndogo ya rangi ya njano au kahawia, huashiria upungufu wa maji mwilini, hivyo kunywa maji ya kutosha, hata kama husikii kiwi. Hakikisha siku zote mkojo wako ni mweupe.


1. CHOO KIGUMU CHENYE UMBO MFANO WA KARANGA


Unapotoa choo cha aina hii, ni dalili kwamba una upungufu wa vyakula vyenye ‘faiba’ (ufumwele), huna maji ya kutosha na usagajwi wa chakula tumboni ni wa taratibu. Suluhisho ni kuongeza kiasi cha maji unachokunywa, kunywa chai ya viungo (herbal tea), matunda na mboga mboga kwa wingi.Vile vile ongeza ulaji wa vyakula vya nafaka, kama vile wali, (brown rice), ugali wa mtama na ulezi. Epuka ulaji wa nyama, mayai, ngano, sukari na bidhaa zitokanazo na maziwa.


2. CHOO UMBO LA ‘SOSEJI’ LAKINI YENYE VIGOLOLI


Aina hii ya choo inaashiria kwamba choo kimekaa muda mrefu sana kwenye utumbo mkubwa. Maji mengi na chakula chenye faiba ya kutosha, kama maharage, wali, ugali vinahitajika. kama ilivyoelezwa hapo juu, ongeza kiwango cha maji unachokunywa, kula matunda na mboga, pia epuka kula vyakula vyenye wanga na sukari nyingi.


3. CHOO MFANO WA ‘SOSEJI’ LAKINI YENYE NYUFA


Choo cha aina hii si dalili ya kitu kingine bali ni upungufu wa maji mwilini, hivyo kunywa maji mengi kwa siku. Kutegemeana na kazi unazozifanya, lakini kiwango cha chini cha maji unachopaswa kunywa kwa siku, ni lita moja na nusu.


4. CHOO MFANO WA ‘SOSEJI’ LAKINI LAINI NA HAKINA NYUFA


Ukitoa choo cha aina hii, ambacho hata wakati wa kujisaidia kinatoka taratibu, jipongeze, kwani ni dalili kuwa uwiano wa vyakula unavyokula na maji uko sawa. Hongera!


5. CHOO CHA MABONGE YENYE NCHA, KINACHOTOKA KIRAHISI


Hii inaweza kuwa dalili kwamba chakula kinasagwa haraka sana tumboni, hali hii inaweza kusababisha ukosefu wa virutubisho na maji mwilini. Ongeza mlo wako wenye ‘faiba’ ya kutosha, hasa kula wali, ugali wa mtama, ulezi na hata virutubisho vingine unavyoweza kuvipata kwa njia ya vidonge (food supplements)


6. CHOO CHA VIPANDEVIPANDE NA LAINI MFANO WA UYOGA


Halikadhalika choo cha aina hii kinaashiria kuwa hakuna maji ya kutosha mwilini, usagaji wa chakula ni wa haraka sana na kuna unyonyaji duni wa virutubisho. Hali hii inasababishwa na mlo duni au mwili kukataa baadhi ya vyakula. Kula vyakula vyenye ‘faiba’ ya kutosha kama ilivyoelezwa hapo juu, acha kula matunda, juisi na mboga kwa muda.


7. CHOO CHA MAJIMAJI MATUPU


Choo cha aina hii siyo kizuri, mara nyingi kinaashiria uambukizo wa ugonjwa fulani. Nenda hospitali kafanyiwe uchunguzi wa kiafya. Kula vizuri, hasa vyakula vya nafaka, supu halisi ya mbogamboga ili kurejesha virutubisho vilivyopotea kutokana na kuharisha. Hakikisha unarejesha maji yaliyopotea mwilini kwa kunywa maji ya kutosha na chai ya viungo (herbal tea).



Uchambuzi huu wa choo, umefanywa hivi karibuni na Dk. K. W. Heaton, ambaye ni msomaji wa tiba katika Chuo Kikuu cha Bristol, Uingereza.


Wednesday, April 09, 2008

Wenzetu huko Afrika Magharibi

GHANA photo from big foto

TOGO Photo from Hobo Traveler

Haya huko Afrika Magharibi nako wanachoshwa na tabia ya watu kujisaidia haja ndogo na kubwa ovyo!

Tuesday, April 08, 2008

Acheni Tabia Mbovu!!!


Nami nakemea vikali hiyo tabia ya wanaume kujisaidia hapa na pale bila hata kujali nani anapita au watoto watacheza hapo!


*******************************************************************************

DC akoromea Wanaosumbua wenzao kwa Mikesha

2008-04-08

Na Abdul Mitumba, Magomeni

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jijini, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, ameagiza watu wote wanaokesha wakipiga na kucheza muziki wa rusha roho na aina nyingine za muziki kwa sauti ya juu kiasi cha kuwasumbua wengine wakome kufanya hivyo na kwamba kuanzia sasa wawe wakiburuzwa kortini kwani wanavunja sheria za nchi.

Kadhalika, DC Massawe amechukizwa na tabia ya wanaume wengi kujisaidia aja ndogo kila sehemu akisema ni baadhi ya dalili za kuporomoka kwa maadili miongoni mwa jamii. Bw. Massawe ameyasema hayo wakati wa mkutano wake mmoja na wananchi wa Kata ya Ndugumbi hivi karibuni.

Mkuu huyo amesema sheria za namna watu wanavyoweza kufanya sherehe majumbani mwao na hata zile zinazoelezea utaratibu wa shughuli za starehe ziko wazi na kila mmoja anapaswa kuzifuata. Akasema kamwe hairuhusiwi watu kukesha wakicheza muziki usiku kucha, tena kwa sauti ya juu kiasi cha kuwasumbua wengine.

Mbali na hayo, DC Massawe pia alikemea tabia ya baadhi ya watu wanaotiririsha maji machafu na kinyesi katika mifereji ya mvua. ``Matukio yote hayo ni mwanzo wa matatizo katika jamii. Kupiga muziki usiku kucha katika makazi ya watu ni tatizo linalokemewa kila siku na ninasisitiza kuwa sasa sheria zifuatwe... kujisaidia ovyo mitaani ni aibu nyingine ambayo jamii inapaswa kuikemea ili kujenga kuwa na kizazi kilichostaarabika,`` akasema DC Massawe.

Agizo la Kanali Massawe limekuja kufuatia baadhi ya wananchi kutoa kero mkutanoni hapo, ambapo kero iliyotawala mkutano ni tabia ya baadhi ya watu kukesha wakipiga muziki katika makazi ya watu.

SOURCE: Alasiri

Saturday, March 15, 2008

Mwanamke akaa kwenye choo miaka miwili!

Trailer ya Tukio huko Wichita, Kansas


Wadau hii story itakutia kichefuchefu, hivyo halahala mkisoma.
Juzi tulisikia habari ya mwanamke fulani huko Kansas aliyekutwa amekaa kwenye choo miaka miwili. Pam Babcock (35) alikutwa kwenye choo ndani ya trela ya boyfriend wake. EMT's walipofika kumhudumia walikuta trela inanuka harufu mbaya mno na huyo Pam kaganda kwenye choo hawezi hata kuinuka! Kumbe nyama ya matako yake ilianza kuota kuzunguka hiyo kiti cha choo!
EMT's walipofika alikataa kuhudumiwa akisema ni mzima na hana shida. Baadaye alikubali msaada wao.

Ilibidi wabandue kiti kwenye choo na kumpeleka hospitalini hivyo hivyo imenasa matakoni! Wanasema kuwa huyo mama aliuwa hajaoga wala hajaosha nywele zake muda wote huo hivyo harufu ilikuwa balaa.
Pia matako yake yalikuwa yamejaa vidonda! Madaktari wanasema kuwa miguu yake ime 'atrophy' yaani misuli imekwisha maana alikuwa hatembee. Wanasema huenda hatatembea tena na itabidi atembee kwa kiti maalum.
Boyfriend wake alisema kuwa eti alikuwa anatoka kwenye choo anaoga na kubadilisha nguo zake, lakini kwa hali wale EMT's na polisi waliyokuta wanampinga! Boyfriend wake anasema kuwa alikuwa anamwomba atoke chooni kila siku na alikuwa anajibu, "labda kesho". Ina maana alikuwa anakula chakula na kulala hapo hapo kwenye choo!

Sasa jamani, hicho choo kilikuwa hakisafishwi hivyo ilikuwa imejaa vinyesi na wadudu! Huyo boyfriend wake alikuwa anajisaidia wapi miaka yote miwili?

Huenda huyo boyfriend atafunguliwa mashitaka kwa kutomkutafutia huyo mwanamke msaada mapema!
Kwa habari zaidi someni:


Kuona video BOFYA HAPA