Saturday, November 21, 2009

Siku ya Choo Duniani - World Toilet Day





Siku ya Alhamisi ilikuwa siku ya choo duniani. Ilikuwa siku ya kutambua umuhimu wa kutumia choo, kuwa na choo kisafi, na hata kuwa na choo. Nchi zingine watu hawana choo wanajisaidia wanapojiweza. Ni kero, hasa sehemu zingine Africa na hata Bongo unatembea njiani na kukutana na kinyesi cha binadamu, au unakuta sehemu inanuka mikojo, kumbe ndo 'unofficial' choo cha wanaume! Wanaume wanajisaidia haja ndogo popote bila aibu.
Kwa habari zaidi tembelea: http://www.worldtoiletday.com/

3 comments:

Nautikasi said...

Wallah tena Da Chemi, uzuri wa nyumba choo..!

Mbele said...

Naamini suala hili ni gumu na tata. Limefungamana na imani na utamaduni wa watu. Kinachoonekana bora na sahihi katika utamaduni fulani kinaweza kisionekane hivyo katika utamaduni mwingine. Tunahitaji utafiti wa kina wa kila utamaduni kuona kwa nini wanafanya wanavyofanya, badala ya kuwahukumu kwa kutumia vigezo vya utamaduni tofauti.

Suala la vyoo ni hivyo hivyo. Nilikuwa India mwaka 1991, kwa mwezi moja. Niliona kuwa kule watu wanaenda porini, na wala si mbali na njia, na wengine pembeni tu ya njia. Wazee, vijana, watoto, wanawake kwa wanaume, hali ni hiyo. Mwanzoni nilishtuka sana, lakini baadaye nilijaribu kupunguza mshtuko.

Katika tamaduni zetu sisi Wandengereko na Wamatumbi, ni mwiko kuwa na choo ndani ya nyumba. Lazima kichimbwe mbali na nyumba. Lakini kwa Wamarekani, kwa mfano, choo kinakuwa ndani ya nyumba.

Leo hii, Waswahili wengi wanaamini kuwa kuwa na choo ndani ya nyumba ndio maendeleo. Kumwiga mzungu ndio maendeleo. Hizi ni kasumba.

Jambo la msingi ni kufanya utafiti. Tuangalie huko kwenye makabila mbali mbali wana mtazamo gani kuhusu suala la kuchimba na kutumia vyoo. Tunaweza kugundua kuwa wana sababu zenye mantiki nzuri, ingawa hatukubaliani nao. Katika kila utamaduni wana mambo ambayo wanafanya ambayo ukiyaangalia kwa vigezo vya nje, yanaonekana ya ovyo, lakini kwa vigezo vyao wenyewe yanakubalika. Kwa mfano, huwa napata kichefuchefu ninapowaona Wamarekani wakimkumbatia na kumbusu mbwa. Lakini kwao ni sawa.

Je, kuchimba dawa porini ni kuchafua mazingira? Hili suala linahitaji mjadala. Binadamu ni viumbe kama viumbe wengine. Je, tembo, vifaru, na sungura ambao wanachimba dawa porini wanaharibu mazingira?

Ninauliza masuali haya kama changamoto. Tuyatafakari. Kule kwetu Umatengo tuna vyoo na tunavitumia, ila vinakuwa mbali na nyumba.

Naomba mwenye majibu ya masuali yangu anisaidie kunielimisha.

mdoti Com-kom said...

Si kila la wazungu ni zuri lakini hili la cho ni vizur tukaliiga vizuri.