Showing posts with label Wapenzi. Show all posts
Showing posts with label Wapenzi. Show all posts

Monday, October 07, 2013

Huyo Dada Anaomba Ushauri Wenu - Mazito

Nimepokea kwa E-mail:

 "Naitwa MARRY nipo chuo mwaka wa pili. Nna rafiki yangu mmoja ambaye nipo nae chuo ambaye ni family friend wetu maana parents wake na wangu wana ukaribu since muda mrefu kidogo. Huyo Baba wa best yangu aliwahi kunitokea kipindi cha nyuma na alikuwa akinipa zawadi za gharama sana ikiwemo laptop na simu ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwangu chuoni ingawa rafiki yangu hajui kuhusiana na hilo.

So ili kuzidisha ukaribu wa family zetu nikaona sikuona sababu ya kumnyima ila nilimuomba tufanye kwa siri sana ili tusije gundulika, na hadi leo tunaendeleza uhusiano wetu. Sasa juzi wakati nipo nae hotelini wakati amekwenda kuoga nikachunguza simu yake nikakuta picha za mama yangu akiwa kapiga nae faragha na jumbe nyingi za kimapenzi walizochat kupitia WhatsApp, Viber na sms. Kitendo cha Mama yangu kumsaliti baba yangu, na pia kutaka kunipokonya bwanaangu kimeniuma sana sio siri. Naomba mnishauri cha kufanya ili niweze kuwatenganisha kwa amani ili familia zetu ziendeleze ukaribu bila wengine kugundua kinachoendelea. Please I need your help on this."

 

Sunday, June 30, 2013

Kwa nini Wanaume Wanalala Baada ya Tendo la Ndoa?

Haya akina mama/dada. Nadhani wote tumekutana na hii tatizo la wanaume kulala wakimaliza shughuli yao katika tendo la ndoa!  Hebu soma hii habari.

************************************************************

Na Mdau Mtambuzi wa Jamii Forum




Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.

Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.

Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.

Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.



Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.

"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.

“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.

Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….

Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe…… 


 

Tuesday, April 24, 2012

Wednesday, July 15, 2009

Unapoona Aibu Kuogozana na Mpenzi Wako


Da Flora Wingia Wiki Hii!



Mpenzi msomaji, leo ngoja nikumegee kituko fulani ambacho hata wewe pengine umekishuhudia mtaani kwako, lakini kinaonekana cha kawaida kabisa.

Mtu anapokuwa na mpenzi wake ama mke au pengine mume, huona fahari sana kuandamana pamoja pale wanapokuwa wanakwenda mahali fulani. Iwe ni kwenye mialiko, kazini na kadhalika.

Lakini msomaji wangu ni jambo la kushangaza kwamba wapo baadhi ya watu, ni mara chache sana utaona wanaongozana na wenzi wao(mke, mume au rafiki kutokana na sababu mbalimbali ambazo naweza kusema zimejificha.

Ipo sababu moja nimeigundua ambayo imeniacha hoi, hivyo nikalazimika kuwamegea wasomaji wangu ili nao kama waliwahi kujiuliza niweze kuwapa jibu mojawapo.

Eti wapo watu wanaofahamika kuwa ni marafiki lakini huona aibu kuongozana wanapokuwa barabarani, wakihofia ama kuchekwa au kusemwa vibaya. Kisa ni kwamba eti mmoja ni mtu mzima sana kiumri huku mwingine ni kijana mdogo au wengine huita ‘chekibobu’.

Hivi majuzi jamaa yangu mmoja alinisimulia kisa cha rafiki yake ambaye ni kijana mtanashati aliyefikisha umri wa kuoa lakini amemganda mama mmoja mtu mzima ambaye alishazaa watoto wawili na wanaume tofauti na watoto hao kuchukuliwa na baba zao.

Anasema, kijana huyu mfanyabiashara, amemfungulia grocery ya vinywaji mwanamama huyo na kila inapofika majira ya saa tatu usiku, huenda kumchukua mchuchu wake huyo kwenda zao nyumbani.

“Ajabu ni kwamba, muda wa biashara ukimalizika hapo usiku, bwana huenda kumfuata mwenzake. Ajabu ni kwamba kijana yule siku zote hutangulia mbele kwa umbali fulani, kisha mwanamama humfuata kwa nyuma. Yaani hawataki watu wawaone eti wakiongozana pamoja…sijui wanahofu nini”, anasema jamaa yangu huyo.

“Sababu kubwa niionayo mimi ni utofauti wa umri, kijana ana umri wa miaka 24, mama yule ni mtu mzima anakaribia miaka 48”, anaongeza kusema.

Mpenzi msomaji, ipo misemo mingi inayoweza kuendana na kituko hicho. Kwa mfano, ‘kila shetani na mbuyu wake’…sikio la kufa halisikii dawa… ndege hutua katika mti aupendao…inzi hufia kidondani na kadhalika.

Siku zote, katika mambo ya mahusiano, kila mtu anazo hisia zake katika jambo fulani. Yupo mtu anayempenda mwenzake kwa kuvutiwa na umbile lake, mwingine sura, mwingine namna anavyoongea, tabia yake, ukacharamu wake na kadhalika. Ili mradi kipo kitu kinachouvuta moyo wake na hatimaye kumpenda.

Sasa katika maamuzi ya aina hii, siyo rahisi kumbandua mtu pale alipoukita moyo wake. Yupo anayependa vibinti vidogo vidogo tu.(ndivyo ibilisi wake anavyomtuma). Yupo anayependa mahusiano na watu wenye umri mkubwa kama kijana niliyemzungumzia na yupo anayechagua wanayekaribiana kiumri ili kuweka mizani ya kimaisha sawa. Yote haya ni maisha anayochagua mtu.

Pamoja na yote hayo, bado maamuzi mengine yana athari mbalimbali katika maisha ya kila siku. Tuchukulie kijana niliyemzungumzia. Hajaoa lakini amejichimbia kwa mama mtu mzima ambaye alishazaa watoto wawili kwa wanaume tofauti.

Kijana huyu hajapata mtoto na mama huyo siyo ajabu hana mpango tena wa kuzaa hasa ikizingatia umri nao umesonga mbele. Kijana penzi la utu uzima ndio limemkolea. Je, ataweza tena kuanzisha mahusiano na binti ambaye ni kijana mwenzake na kuachana na mama huyo?

Inanipa shaka kwamba anaweza kujinasua upesi toka kwa mama huyo mtu mzima hasa kwa jinsi baadhi ya kinamama wenye tabia ya kurubuni vijana wadogo walivyo wajanja. Hawa wanajulikana kama mashugamami.

Vijana walioangukia mikononi mwa mashugamami, wengine wameharibikiwa kabisa. Wapo wanaorubuniwa na kinamama wenye uwezo mkubwa, wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo. Huwavuta kwa fedha na wengine wamediriki hata kuwanunulia magari.

Lakini usaliti huu hufanyika kwa siri kwani huwezi kuona warubuniwa wakiambatana na mashugamami hao. Na kwa kuwa hivi sasa kuna simu za viganjani ndiyo kabisa mambo ni kimya kimya. Watendao haya wamuogope sana Mungu. Hukumu iko mbele yao.

Hakika, Maisha Ndivyo Yalivyo. Mimi natoa dokezo tu kwamba tusione watu wanaambatana kwa umbali fulani, kumbe hiyo ni janja tu ya kuficha mambo. Hata hivyo, hebu tujiulize, kama wanayofanya ni halali, kwanini wasishikane hata mikono mashuhuda wakawaona? Au ni yale mapenzi ya wizi tunayoambiwa mitaani?

Mpenzi msomaji, kwa leo niishia hapa nikupe fursa nawe uchangie maoni au kisa chochote unachodhani tunaweza kujadili kwa pamoja. Kila la kheri.

fwingia@yahoo.com

Wasalaam

Saturday, February 14, 2009

Happy Valentine's Day!



Leo ni siku ya Wapenzi! Tupendane na mpende anayekupenda. Kama umepania kuoa basi leo u-propose kwa mpenzi wako. Na akina mama muandae vitu vizuri huko chumbani leo!

Wednesday, August 29, 2007

Wapenzi na Wivu


Mara nyingi tunasikia habari ya mtu kumpiga mpenzi wake kwa ajili ya wivu. Mwanamke kasalimiwa na mwanaume mwingine, kibao! Mwanamke anapiga simu nyumbani kumwulizia mtu, mke anampiga na sufuria na mengine. Lakini wakati mwingine wivu unazidi mpaka watu wanafanya maajabu.

Nimesikitika sana kusikia habari ya jamaa kujinyonga Gesti huko Tandika eti kwa vile mpenzi wake wa miaka 19 alikuwa na wapenzi wengi. Kitu gani kilimwingia marehemu Said Libonge mpaka kaamua kumchoma mpenzi wake kisu na yeye mwenyewe kujinyonga. Ni wivu au ugonjwa wa akili?

Mimi sikuwepo bali nimesoma tu hiyo habari ya kusikitisha. Na huyo dada lazima atajiuliza mara mbili tatu kabla ya kuingia gesti na mwanaume au kuwa na mpenzi mwingine.

Lakini nikikumbuka vituko wanavyofanya wapenzi kwa jina la wivu, nasikitika na nacheka. Haya tuchukue kesi ya mama fulani aliyemkuta mume wake yuko kwenye shughuli ndani ya gari eneo ya Mbuyuni Dar es Salaam miaka ya tisini. Yule mama alidai kuwa alifungua mlango wa gari kamkuta mume wake yuko juu ya howara wake anapampu na alidai kuwa mambo yao yalikolea kiasi kuwa alikuwa anampiga mume wake aliyekuwa ameshusha suruali matakoni na hakusikia kitu. Kwanza mtu wa kawaida angebakia anashangaa mdomo wazi, au angekimbia kwa aibu. Lakini hapa huyo mama na wivu zake kaweza kufungua mlango wa gari na kuanza kumpiga mtu shughulini.
Haya nakumbuka kisa cha mama mwingine miaka ya themanini. Mume wake alienda na howara wake kwenye gesti Manzese. Yule mama alijua yuko chumba gani. Kitanda kilikuwa chini ya dirisha. Basi yule mama alikesha pale kwenye dirisha na walipoanza mambo yao, yule mama kafungua dirisha na kuwamwagia chupa ya tindi kali. Kwa vile walikuwa uchi wote waliungua vibaya! Wivu jamani!

Nilivyokuwa nasoma Tabora Girls kuna dada fulani aliuliwa na mume wake. Sitamsahau yule dada. Alikuwa anakaa National Housing na mume wake, ndoa yao bado changa. Dada mwenyewe alikuwa mzuri kweli kweli. Mume wake alikuwa ni mwanajeshi mwenye cheo cha Kepiteni. Alikuwa mwembamba mwenye kipara. Kuna wenzangu walimuwa wanamvizia yule baba. Basi kuna siku yule baba alishikwa na wivu, kamfunga kamba mke wake na kumtia matambara mdomoni mwake kusudi asiweze kupiga kelele. Wanasema kuwa yule baba alimpiga raundi ya kwanza, kampiga raundi ya pili, kampiga raundi ya tatu mpaka yule dada kafa. Eti kapusuliwa bandama! Kisa cha kumpiga mke wake mpaka kafa kilikuwa eti alimwona anaongea na mwanume mwingine. Yule baba alihukumiwa kifo.

Niendelee? Kuna visa vingi, vya watu kuua au kuumiza wapenzi wao kwa jina la wivu.

Mimi mwenyewe nimeshikwa na wivu mara kadhaa lakini siyo kiasi cha kuua au kumwumiza mtu! Niwasimulimie kisa kimoja. Kuna jamaa nilikuwa nampenda sana. Lakini yeye hakunijali wala nini zaidi ya kusalimiana. Basi kuna siku nilimwona anakwenda kwenye deti mjini DSM na dada fulani! DUH! Nilijikuta naona kizunguzungu, Siwezi kusema, hasira zimejaa na nikaanza kulia! Watu waliniuliza nalia nini, nikashindwa kusema! Baadaye nikasema basi Mungu hakupanga niwe naye. Yaani nikikumbuka nacheka.



Mnasemaje kuhusu wapenzi na wivu?