Haya akina mama/dada. Nadhani wote tumekutana na hii tatizo la wanaume kulala wakimaliza shughuli yao katika tendo la ndoa! Hebu soma hii habari.
************************************************************
Na Mdau Mtambuzi wa Jamii Forum
Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza
maswali chungu mzima kama kuna mahali wamekosea au hawajawavutia wapenzi
wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi
punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.
Lakini utafiti uliofanywa hivi na wanasayansi unawapa wanaume ahuweni
katika kuepuka lawama hizo, kwamba, kumbe siyo hiyari yao, bali ni
maumbile.
Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa sababu za kimaumbile ubongo wa
wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi baada ya kushiriki tendo la
kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi hao walibaini kwamba, kwa
jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa, pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.
Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali ni tofauti, kwani wao hubaki
wakikodolea macho dari wakiwa wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali
lukuki, wakijihisi kutowaridhisha wapenzi wao.
Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha kipimo cha kumulika, maarufu kama
scan, ambapo kilitumika kuwamulika wanaume katika ubongo wao pale
wanapofanya tendo la kujamiiana na baada ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’ huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.
"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae Serge Stoleru.
“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.
Mwanasayansi huyo aliendelea kusema kwamba, wanawake hushangazwa sana na
jambo hilo na ndio sababu hubaki wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala
baada ya kumaliza tendo il hali wao wakitaka zaidi….
Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
12 comments:
Hahaha kesi kwa wakwe lol baba nanihiliu ye alala tu mpaka nimpige
miteke aku mie najiondoshea nyumbani. DAWA YAKE PRINTI HII KITU ukifika nyumbani unamwekea mama Koku asome mwenye then ruhusa kukoroma hasa kama umeweka viondoa mawazo vya maji ya rangi ya brown
Ndilo tatizo la wanawake: kwamba kulikua wakati mtu huyu huyu anayegeuka na kuzimia hakuzimia mara kadhaa, vipi leo anaishia usingizini round moja tu??
Wanawake wana hisia kali na kwa sehemu maisha yao huendeshwa kwa
kuhisi ambako mara nyingi pia wako sahihi kwa sababu ya asili yao kama
wenye hisia kali kuliko nguvu ya misuli....kwa hiyo wanaguswa na
nyendo, maneno ama vitendo fulani...wanafuatilia tangu mlipoanza kujuana mpaka mwisho wa maisha ama wa uhusiano...
Hapa kina baba mbadilike tu hakuna sayansi ya mapenzi mapya na ya
zamani - isipokuwa sayansi ya kumridhisha mwenzi wako ikiwezekana kwa jinsi anavyopenda pia maana ndiko kumridhisha hasa.
Mnakula mikuku ya kidhungu, michipsi mayai yenye rangi moja(sawa na ndoa ya jinsia moja!) .... hakuna mazoezi wala kutembea kwa miguu! Mmeenda shule kwa taxi, au daladala! Mnapokelewa mabegi ya shule na Hausi geli! Mibia na misuupyu kila jioni!! hamjui hata kwenda Uvinza!!
halafu mnategemea mkimbie maili tisa!
Mkishindwa mnadhania wengine!!
Ntafungua darasa rasmi kwa mabadiliko pekee, ngoja nimalize hili.
Ndio ujue sasa ushapoteza nguvu kiasi gani. Unafikiri kwa nn wanaume wanazeeka haraka miili yao? Kazi hiyo ni ngumu ila mwaipenda wababa kuliko zote. Punguza sasa Katu iwe ni mara moja kwa wiki ama kwa mwezi. Tehetehe utaweza?
Wanawake wanaodhania kwamba wanaume wanalala makusudi ni lazima watakuwa wanawake wajinga.
Wanawake tuna jukumu kabisa la kuwandaa wenzi wetu isipokuwa wenzi wetu kutokana na maumbile yao wanalegea mapema mno ni kama kumsukuma mlevi vile. Sasa kina mama tunachukua muda kidogo kutokana na tulivyoumbwa, tatizo linakuja pale wenzetu mkilashelegea hamna muda wa kuhakikisha na mwezio kafikia level yako wewe hapo unataka mchezo uishe ulale na kukoroma ukimuacha mwenzio anangalia dari.
Wanaume wa Bongo na Afrika kwa ujumla ni wachoyo sana katika mapenzi! Wanajifikiria wao tu!
Chemi leo nakupinga Binafsi ni Mwafrica halisi siyo mchoyo kabisa,nina hakikisha kwa Mwali wangu kafika ndiyo na mimi naanza ngoma zangu.Yote hii natoa asante kwa Mafunzo niliyopata Jandoni[Mwali ukimtayarisha na kumfisha kileleni]hukufuatilia kwa simu kila dakika.Asante Muhangaikaji wa Mid-South[Tennessee.
Sexually frustrated black women are the ones who come up with statements like "Wanaume weusi wachoyo wa mapenzi". If you chose a wrong guy for wrong reasons then you only have yourself to blame. Ask white women will tell you how generous we can be, and how much love we can give when our partners are prepared to reciprocate the favour.
Chemi, wanaume kulala baada ya tendo la ndoa ni kitu natural, hawafanyi makusudi. Kufikia tamati ya tendo la ndoa kwa wanaume huambatana na mwili kutoa aina fulani ya kemikali ambayo husafiri hadi kwenye ubongo na kumfanya mhusika kulala fofofo kwa hata kama ni asubuhi. Wataalam wanasema hii ni kwa ajili ya kuupumzisha mwili. Kwa hiyo hapa hakuna kitu kama uchoyo. This is a natural process. Kulazimisha kutolala ili kumfurahisha mwanamke na kujifanya unamjali kunaweza kuwa na madhara kwa wanaume.
Kwa wewe uliyejiita Askofu Zakri Kikobe, Miaka ya 1900's kulikuwa na "Unofficial Mjadala" kuhusu ngono pale UDSM. Midume ilikuwa inasema eti, Mwanaume Mwafrika anamfaa zaidi mwanamke mzungu na Mwanaume Mzungu anamfaa zaidi Mwanamke Mweusi!" Nadhani ulikuwepo katika mjadala huo. Lakini na pombe mnazaopenda kunywa nyie waBongo unachangia huo usingizi wenu!
Dada umetoa shule ya uhakika lakini generalize mno hasa hapa "kuna pia janja ya kuanzia mahali, halafu akaja kumalizia nyumbani! Hapo utategemea nini kama si kukoroma baada ya round moja tu, tena ya mara moja kwa wiki!"
Maumbile nayo ni shida mmoja mpaka iwe nondo ndio fanye kazi, mwingine iko wazi tuu sasa hapa napo panahitaji maelezo, push and receive they are not the same, no matter how swing
Post a Comment