Thursday, September 24, 2009

Maneno ya Wimbo 'Hongera Mwanangu'

Bibi Titi na Mwalimu Nyerere

Kuna mdau kaniomba nimtafutie maneno (lyrics) za wimbo, Hongera Mwanangu ambayo tulisikia sana Radio Tanzania enzi zile ukiimbwa na marehemu Bibi Titi Mohamed. Sasa naomba nisaidie, ni lugha gani wanaiyotumia. Naona maneno ya kiswahili na sijui ni kilugha gani.


******************************************************************

HONGERA MWANANGU

Hongera mwanangu eh hongera.
Nami nihongeree hongera.

Hongera mwanangu eh hongera.
Nami nihongeree hongera.

Mama uchungu, Mama uchungu.

Nyamara mwanangu. Oyee.

Nyamara mwanangu tumbo la udere linauma mno eh!

9 comments:

Mbele said...

Nimefurahi kuiona tena hii picha, ambayo niliiona zamani. Napenda kuwafahamisha wadau kuwa kuna kitabu maarufu kuhusu mchango wa Bibi Titi Mohammed na wanawake kwa ujumla katika harakati ya kupigania uhuru Tanganyika. Kitabu hiki kinaitwa "TANU Women." Kiliandikwa na marehemu profesa Susan Geiger, aliyekuwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Minnesota, Marekani. Kilichapishwa na Heinemann, mwaka 1997. Ni muhimu kwa yeyote anayetaka kujielimisha.

Fake Expatriate said...

is that kinyarwanda?

Anonymous said...

Ni Kimatumbi!

Anonymous said...

umenikumbusha zamani sana mama. nadhani kuna haja ya kuziweka nyimbo zote za vipindi vya RTD katika website moja ili tujikumbushe wakati tupo watoto.Nyimbo za vipindi kama mama na mwana,mchana mwema,rushwa ni adui wa haki,salamu kwa wagonjwa na nyimbo nyingi za vipindi vya zamani ambavyo nimevisahau.Hata kama watauza online mimi nipo tayari kununua.Nawakilisha mdau Sweden.

Anonymous said...

Sasa kama D kemi unaweza kuweka video kwanini usitutafutie huo wimbo ukatuwekea Audio hapa nasi tukajidai maana hiyo kitu ni zamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaanniiiiiiiii, wakati huo wengine tunafuta kamasi na BAPA la mkono. Uongooo!?!! Haahahaaa nimefurahi pia, Pro. Mbele Hiko kitabu kinapatikana wapi pengine kinaweza tusaidia kwa kiasi fulani. Natanguliza Shukrani Kwa Da K na Pro Mbele

John Mwaipopo said...

Nahisi ni kizaramo ama lugha inayoshabihiana kileksikolojia na kizaramo. kwa kizaramo 'kunyamara' ni 'kunyamaza'. ndio maana tukawa na vitongoji kama 'mwananyamala' ikimaanisha 'mtoto nyamaza'

Anonymous said...

Upo sahihi Mwaipopo,hicho ni Kizaramo hata hiyo tumbo la udele inamaana ni mimba ya kwanza!!

Anonymous said...

Those were the days

kats.com said...

Kizaramo hicho