Sunday, August 29, 2010

KITAMBI/UNENE: Ni dalili ya Utajiri au Ugonjwa?

(Picha kwa hisani ya Michuzi Jr.)

Imeandikwa na Malkiory William Matiya

Katika baadhi ya jamii zetu nyingi hasa kutoka bara la Afrika, kumejengeka dhana kuwa kitambi /unene huashiria utajiri. Mila, imani na desturi hii kwa kiasi fulani huchangia watu kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora, pengine hii inatokana na mwamko mdogo wa elimu ya afya jamii.

Wakati hali ikiwa hivyo miongoni mwa watu toka bara letu la Afrika, kwa upande wa nchi zilizoendelea, watu huamini kuwa unene/kitambi ni dalili tosha ya ugonjwa. Siyo hivyo tu bali pia historia ya magonjwa katika fani ya elimu afya jamii inatueleza hivyo.

Kuna unene wa aina kuu mbili, kwanza ni ule unaosababishwa na kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora / balance diet. Kwa mfano ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta na wanga, unywaji wa mara kwa mara wa pombe kama vile bia pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo. Aina ya pili ya unene ni ule unaotokana na urithi japo kwenye mada hii msisitizo zaidi ni kwenye aina ya kwanza ya unene.


Kuna matatizo mbali mbali yanayo ambatana na unene/kitambi. Mosi, madhara ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari aina ya pili /diabetes type II. Pili, madhara ya kisaikolojia, hasa pale mtu anapojishuku kupoteza mvuto/ aesthetic beauty. Hali imeshamiri sana hasa katika nchi zilizoendelea ambapo watu huchukulia unene/kitambi kama ulemavu fulani wa kimwili.

Pamoja na hayo, nadhani wakati mwingine tunafanya makosa kuwahukumu binadamu kulingana na mwonekano wa maumbile yao, kwani hakuna hata moja kati yetu anaweza kuingilia kazi ya uumbaji, ninasema hivi kwasababu hatuwezi kujua ni nini chanzo hasa ambacho kinapelekea mtu kuwa mnene au kuwa na kitambi. Kama nilivyosema awali, kuna aina ya unene/kitambi kinachotokana au kusababishwa na urithi.

Namna ya kukabiliana na matatizo yatokanayo na unene/kitambi, wakati watu katika mataifa yanayoendelea, hujikita zaidi kwenye matumizi ya magari hasa magari binafsi, kidogo hali ni tofauti katika nchi zilizoendelea ambapo msisizito kwao ni kwenaye matumizi ya usafiri wa umma, matumizi ya baiskeli na hata matembezi ya miguu kwa sehemu zinazofikika. Kwa hili wenzetu wa mataifa yaliyoendelea wamefanikiwa vya kutosha kwa kuwekeza na kutenganisha barabara za magari na zile za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu.

Mwisho, njia pekee ya kukabiliana na changamoto hii ya unene/kitambi, ni kwa kuzingitia kanuni za lishe bora kwa kujisomea majarida yanayohusu elimu ya afya kwa jamii na kujijengea tabia ya kufanya mazoezi ya mwili na viungo. Muhimu kuliko yote, kama itawezekana ni kupunguza ulaji wa nyama choma na unywaji wa bia wa mara kwa mara.



Malkiory William Matiya

Mtebelee Blog yake: http://malkiory-matiya.blogspot.com/

9 comments:

Anonymous said...

wataka kuniuuuaa sasa maaana hayo makitu kwangu ndo mwake.laga plus nyamaz kama sijapata kitu hicho lazima ni hisi kuishiwa nguvu.jamani tujiadhari unene unauwa ilaa midayati pia nomaa hizo ni mila za wakoloni myili yetu na yao tofauti jamani.asante anti ze chemi

Anonymous said...

Bongi watu wanatamba na vitambi vyao wanashindana na ana kitambi kikubwa zaidi! Khaa!

emu-three said...

Unajua hiyo ni kama ile wasemayo ukiwa na upara ni dalili kuwa wewe ni tajiri, au mwanamke akiwa na ndevu ni `dalili ya utajiri'
Mimi kwa uonii wangu watu waliamua kusema hivyo kwasababu nii nadra watu kuwa a vitu hivyo , na ili hawa watu wasijisikia vibaya, ikabidi mabadiliko hayo yapewe sifa, vinginevyo wengine wangejisikia vibaya!
Haya watu wakaanza kuwa na vitambi, hii mwanzoni ilikuwa ni kama `ka-aibu fulani' una tumbo kama mama mja-mmmh' sasa ili kuiondoa hiyo dhana, wakazuka watu kuivika chati kuwa ukiwa na kitu kama hicho wewe unaashiria unazo!
Mhhh, kama umewahii kuwa na kitambi mmmh, sijui lakini mimi naona kama ni kaugonjwa ka namna fulani ambako hakaumizi sana kwa papohapo, lakini kwa marefu kuna athari

Anonymous said...

katika aina mbili za unene ulizotaja jee chemi wewe upo katika kundi lipi?

unene wa kula sana au unene wa kurithi?

Anonymous said...

Mie ninachompendea dada chemi yupo comfortable na mwili wake. Mie nadhani unene wake ni wa urithi.

Peace

Anonymous said...

kwa nchi za Magharibi vitambi ni uchovu kwa Bongo kuna baadhi watu wanaona sifa

Anonymous said...

Kitambi si afya jamani. Mawazo finyu ndo yanatufanya tuwe na mortality rate ya ajabu! Fikliria ukifikisha umri 45 wewe ni mzee Bongo unangojea kwenda kwa Bwana siku yoyote!

Anonymous said...

Kitambi Oyee! Sasa nisipokuwa na kitambi watajuaje kama nimekuwa lodi?

Anonymous said...

"Kifriji" muhimu....kama huna pole yako!