Wadau, baada ya kuona sinema, Lumumba, mwaka 2001, nilikuwa najiuliza mke wa Patrice Lumumba alikuwa wapi. Lumumba aliuwawa mwaka 1961 akiwa Waziri Mkuu wa Congo. Alikuwa ni mtu ambaye alipenda sana nchi yake na nadhani angeishi Congo ingekuwa mbali zaidi. Yuko Gombe, Congo.
Mama Pauline Lumumba mjane wa Waziri Mkuu wa Congo, Patrice Lumumba aliyeuwawa mwaka 1961. Amekaa mbele na Waziri Mark Mwandosya.
(Picha kwa hisani ya Michuzi Blog) Alipokuwa Kinshasa Prof. Mark Mwandosya pia alimtembelea Mama Pauline Lumumba, mjane wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Congo, Marehemu Patrice Emery Lumumba,nyumbani kwake Gombe. Katika picha, waliokaa ni Mama Pauline Lumumba na Prof. Mark Mwandosya. Waliosimama kushoto ni Mama Lucy Mwandosya na kulia ni Juliana Lumumba, binti wa marehemu Patrice Lumumba, aliyekuwa waziri wa Habari na Utamaduni katika serikali ya Marehemu Laurent Kabila.
Mama Pauline Lumumba na moja wa watoto wake, na shemeji yake mara baada ya kuuwawa kwa mume wake, Patrice Lumumba, mwaka 1961.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Hiyo picha ya chini, Mama Pauline ana huzuni mno. Nashukuru Mungu alimlinda na anaendelea vizuri huko Congo.
Post a Comment