Blowing Point Beach. Beach zote za Anguilla ziko wazi kwa kila mtu, hata kama kuna hoteli ya kifahari. Lazima waruhusu watu kwenda bila kiingilio.
Hapa nakata tiketi ya kupanda boti kwenda kwenye uwanja wa ndege St. Maarten ili nipande ndege ya kwenda Boston.
Kimbunga ikikaribia Anguilla.
Hiyo ferry ilienda St. Maarten ingawa kulikuwa na mawingu na dalili ya kimbunga. Lazima baadhi ya walikuwemo walitapika shauri ya mawimbi makali.
Mimi na baba yangu mzazi, Dr. Aleck Che-Mponda nje ya ofisi ya Uhamiaji ya Anguilla. Ndani Air Condition safi, na huduma nzuri.
Nikienda kupanda ferry kwenda st. Maarten.
Niko kwenye ferry.
Hapa niko Beach nikijiandaa kwenda snorkeling. Niliona samakai wazuri kweli, wenye marangi rangi. Tena walikuwa karibu na ufukwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Unatutamanisha, kipi ambacho sisi wabongo tunaweza kujifunza toka huko, lakini kisihitaji wafadhili, manaka hapa bongo kila kitu wafadhili hata kufagia barabara
Da Chemi maelezo ya picha hapo juu sikuyaelewa vizuri, umemaanisha, 'mimi na baba yangu, ama mimi na baba yenu.' Na kama ni wewe na baba yetu ina maana tayari umeshachukuliwa tena jumla jumla? Samahani kama nitakuwa nimekubore.
Anonymous wa 1:01AM, asante, ilikuwa typo. Kwa kweli nilipokuwa huko sikuona mabango ya eti Funded by Danish Government. Wanajitegemea sana. Pesa wanapata kutokana na kuvutia watalii na watalii wao si kamchape class. Kuna villas ambazo wanakodisha akina Beyonce, Mariah Carey na Oprah huko! Nilishangaa mdogo wangu aliponiambia kuwa Sharon Stone alikodi Villa jirani yake. Lakini uzuri wa Anguilla hakuna usumbufu wa watu kudai 'chai'/bahasha kila kona!
mimi dada kwa kweli nakupenda umekaa vizuri,vipi naweza wasiliana nawe?
Nakupenda sana Da chemi...huwa uko mkweli na unaonekana unaroho nzuri sana. Mwenyezi mungu aendelee kukupa zaidi
Post a Comment