Wadau, huyo ngedere aliyeshika kitoto cha paka ni Dume tena ana mandevu. Inakuwaje anakuwa na hisia za mwanamke za kumtunza mtoto? Cheki alivyompakata na kumbeba paka...kama vile mwanae. Huyo paka inaelekea ni yatima na ni bahati tu
aliingia kwenye hiyo hifadhai na kukutana na ngedere mwenye huruma. Wengine si wangemwua au kumla? Wanasema ndegere dume anafanya kazi nzuri ya kuinda usalama was huyo paka. Huyo ngedere yuko katika hifadhi ya manyani huko Bali, Indonesia.
Mnaweza kuona picha zaidi hapa:
http://www.guardian.co.uk/environment/gallery/2010/aug/25/bali-animals#/?picture=366113732&index=5
************************************
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Shoga!
Kutunza mtoto sio hisia ya mwanamke/kike tu. Kuna wanaume/madume mengi tu yana hisia hizo. Je, umepata wahi kumuona samaki mpiganaji kwa jina 'Siamese Fighter'? Dume la samaki huyo ndio linatunza na kulinda watoto tena kwa kutumia mdomo!Mfumo dume ndio unatughilibu tuamini utunzaji wa watoto sio hisia ya kiume/kidume!
Fikiria kama wanyama wanafikia hali hiyo ya kupendana na kumlea mtoto hata sio wa aina yake, kwanini sisi wanadamu ambao tumepewa akili ya kutafakari tunashindwa?
Watu hawapendani eti kwasababu ya sura, rangi , dini au kabila, basi itafika muda wanyama wao watakuwa na amanikutushinda sisi binadamu, na hapo tutanyang'anywa utawala wa dunia na kupewa wanyama
Hapo ndio kwa mwanadam kujifunza na kufikiri, ni jinsi gani, hata mnya asiekua na utashi wa kujua baya na zuri, lakini bado anaonyesha upendo, tena upendo mukuu, na wa ajabu, kwa kiumbe ambae wanatofautia kabisa kwa mtazamo hata kibaologia.
Ngedere dume anajua sana kulea watoto. Anapokuwa ana nyege huwahonga majike kwa kujitolea kuwalelea watoto kusudi wao wakajichane kokote wapendako, mradi tu wakirudi apate mgao wake mara moja.
Post a Comment