Binafsi sioni shida ya kuvaa nguo ya harusi ya mabega wazi, ndo fesheni sehemu nyingi. Mbona, tunavaa khanga na vitenge na tunakuwa mabega wazi? Lakini kama umeambiwa mapema kuwa nguo hiyo haifai kanisani basi msikilize Padri au tafuta Kanisa lingine!
***************************************
KUTOKA GAZETI LA HABARI LEO
***************************************
KUTOKA GAZETI LA HABARI LEO
VAZI LA NUSU UCHI LAZUIA NDOA KUFUNGWA JIJINI DAR....PADRI AGEUKA MBOGO NA KUWATIMUA WAPAMBE
KIVAZI cha ndugu wa maharusi, kimesababisha patashika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Peter, baada ya Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Padri Paulo Haule, kusitisha ibada mpaka mhusika atoke akavae vizuri.
*“Ninatoa dakika 10 kwa aliyeingia na mavazi ambayo hayatakiwi kanisani humu kutoka mara moja akavae vizuri, la sivyo ndoa yao haitafungwa,”* alisema Padri Haule wa Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.
Awali vurugu hizo zilizotokea Jumamosi iliyopita, zilianzia nje, wakati Katekista wa Parokia hiyo, Yohane Maboko, alipotangazia wanandoa na ndugu zao waliokuwa mabega wazi au kuvaa nguo fupi, kutafuta nguo za kujifunika au wasiingie kabisa kanisani.
Maharusi walikubali kutekeleza ombi hilo, wakavishwa vitambaa mabegani vya rangi tofauti na gauni jeupe la harusi, wakaruhusiwa kuingia kanisani, tayari kufunga pingu zao za maisha.
Aliyegoma kutoka na nguo yake ya nusu uchi |
Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa maharusi hao ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipotaka kulazimisha kuingia na kivazi chake cha mabega wazi, alizuiwa na Katekista Maboko. Katekista huyo alimfuata mwanamke huyo ili kumrudisha akavae vizuri, lakini aliibua zogo na kulazimisha kuingia na
vazi hilo.
Zogo hilo lilipoendelea, wanandugu waliingilia kati, wakitetea vazi hilo ambapo mmoja wa wanandugu, alimvua miwani Katekista Maboko na kuipiga chini ikavunjika huku yeye na wenzake wakimtolea maneno makali ya kumtaka asimzuie ndugu yao kuingia kanisani.
Wakati ndugu hao wakimdhibiti Katekista Maboko, mwanamke huyo alitumia mwanya huo na kupenya hadi ndani ya Kanisa, ambamo Padri Haule, alikuwa akijiandaa kuanza ibada.
*Baada ya Padri Haule kupata taarifa, alitangaza kuwa ndoa ya maharusi wa msichana huyo, haitafungwa hadi awe ametoka. *
Licha ya Paroko kutangaza hivyo, bado ukaidi uliendelea jambo lililomfanya Katekista Maboko kumfuata tena dada huyo na kumwamuru atoke nje, ambapo aliendelea kupinga na baadaye akatekeleza amri hiyo ya Paroko.
Baada ya hapo shughuli za kufungisha ndoa ziliendelea kwa amani na utulivu hadi mwisho maharusi wakatoka kwenda kuendelea na mambo mengine.
Akizungumza na mwandishi wetu, Katekista Maboko alisema waumini hao walikiuka maadili ambayo Kanisa lina wajibu wa kulinda na kuyasimamia ili waumini wake wayafuate.
Alisema miwani yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya Sh 90,000 na baada ya ibada hiyo, aliyetenda kosa hilo alimwendea na kumwomba radhi na kulipa Sh 50,000 na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki wakati wowote.
Maboko alisema uvaaji wa mavazi yasiyotakiwa kanisani hapo, umekuwa ukipigiwa kelele mara kwa mara, na hata katika mafundisho ya ndoa huambiwa lakini ukaidi unaendelea.
*“Maharusi wakati wa mafundisho ya ndoa tunawaambia kuhusu mavazi yao na hata ya ndugu zao watakaowasindikiza kanisani, kuwa wavae kistaarabu lakini hawasikii,”* alisema Katekista Maboko.
Makanisa mengi siku hizi yamekuwa yakipiga marufuku uvaaji wa nguo fupi na zinazoacha mabega wazi kwa wasichana na wanawake, wakati wa ibada za kawaida na za ndoa.
Habari Leo
Hii fesheni inapendwa na vijana wengi |
17 comments:
Wehu tu wa wadada na wamama sometimes, hakuna dhehebu linaruhusu kwenda kwa ibada bila kujisitiri. Western life inatuzuzua tukadhani ndio bora. Heri kurudi kwa majani ya migomba na ukili sijui?
bora Katekista kasaidiwa na padre yangekuwa mengine hapo. Duh mdada mwenyewe mnamwona hapo? utadhani anataka kupigana !!!! kweli wanawake wa kikristo uvaaji kwenye ibada umetutoka. hadi ngumi ndio tuvae vizuri? kunani? au Me ndio mkituona hivyo ndio mnavutiwa?
Yesu alikuwa akiwahubiria makahaba, sasa tukiwafukuza kanisani waliovaa 'kikahaba' ambao kama tunawachukulia kuwa watenda dhambi wakuu ni wapi watapata khabari njema maana Yesu anadai ya kuwa aliyemzima (asiyevaa kikahaba) hahitaji daktari kama huyu mgonjwa (aliyevaa kikahaba)
paadri naye hasiruhusiwe ukumbini maana ni kama anategeka kirahisi saaaaana!
Si wangemhonga padri bahasha anyamaze! Sh. 50,000/- angekuwa haioni!
Sheria za wanawake wajihifadhi kwa nguo ndefu kaziweka MUNGU hapa duniani kupita maandiko yake
Sasa huko kukubalika kwa yule Dada mvaa nusu uchi mbele za MUNGU ni kupi huko ?
Au ndio umeanza kuwa kama Mtume Paulo anayesema Upumbavu wa MUNGU ni busara kwa Wanadamu ?
Subhanallah..
Wabongo tumezidi ushamba!!!!
Wanaume Bwana! Wadhaiiiiiifu .... sasa hata wakiona bega wamekwisha.
Yesu aliwafukuza wafanya biashara kwenye hekalu sio wanawake na nguo zao. Aliwafukuza maana kwa ufisadi na unyonyaji wao walinajisi sehemu takatifu. Sisi je? Siku hizi tunaendesha minada ndani ya kanisa? Sehemu za ibada tunawahusudu wenye pesa bila kujali pesa hizi zimetoka wapi. Tumekuwa Mafarisayo.
Sasa kuondoa strap ya gauni ndio nusu uchi? Ha ha ha ha Kastrap tu?
Mbona hawakuonyesha chini, maana hayao mabega sio tatizo zana, sensitive area zote hazionekani. siwezi kumuhukumu mdada wa watu
Mbona mimi sioni kama hilo ni tatizo, maana kuhesabiwa dhambi au mema hakutegemei mavazi,.
Mimi nionavyo Katekista aliingilia uhuru wa mtu na maamuzi ya Mungu ,Katekista au padre walienda mbali mno kiasi , hata kama nisheria za kanisa mtu hutakiwa kujifunza mwenyewe, sio shuruti ya namna hiyo, Tutajuaje mwanadada huyu huenda alikuwa anakubalika kwa Mungu kuliko waliokuwa wanampinga .?, kwa hiyo mimi naona kanisa ni kimbilio la kila mtu bila kujali amejisitiri vipi.? Maana Mungu huchunguza nafsi ya mtu si sura au kujipamba.
Khaa! Nyoko! Ndo maana Tanzania haitaendelea! Sasa huyo Padri ana mamlaka kuliko Bwana Yesu.
hilo ndio kanisa katoliki la roma bwana. anayelipinga atafute la kwake. shida nini. kuna sheria za Mungu na za Kanisa. huyo dada anazijua. kama hazijui kwa umri huo, inatia shaka. kama hawezi kuzifuata, atafute kanisa lingine. juzi juzi Padre we Parokia yetu alikumbushia wanawake kutia lipstiki. akasema hawawezi kuvumilia hata saa 2 tu za kwenda kanisani. wanamkwaza, mkate unabaki na lipstiki kisha anamlisha mwingine. si vyema. kwa nini tukwazane hadi kanisani. Namsifu Katekista yule. alionesha ukomavu, alizuia hasira. picha zimemwonesha alivyocontain hasira. ingekuwa balaa.
Tatizo ni nguo gani uvae wapi
Vaa chupi tu club hakuna wa kukuuliza
Vaa chupi beach hakuna wa kukuuliza
Vaa chupi hiyo hiyo na uende sokoni au ofisini au baa uone kitatokea nini kama hautaitwa chizi jiandae kulala lupango labda ahueni ya bar utaitwa kahaba tuwe wa kweli kwenye matumizi sahihi ya nguo
Over-zealous, HYPOCRITICAL padres!
Mabega SIO uchi! Damn!
Jamani~ tangu lini mabega yakawa uchi wa kule chini? Tunazisikia habari za mapadri ambao ni wanafiki~ wanatembea na watoto wadogo, na pia wake za watu. Halafu wanajidai watakatifu!!
Siku moja hao mapadri wataanza kuwaambia wanawake wavae BUIBUI au HIJAB wakienda kanisani... eti imeandidwa kwenye biblia! Aiiiiii karamba!
Labda padri alitaka huyu dada avae kama mtawa.
Karne za mawe zinarudi. Amri za Hitler au, amri za 'fundamentalism' zinakuja. Jamani Jamani!
Unafiki mtupu!
Post a Comment