Tuesday, July 09, 2013

Ofisi ya Ardhi Kahama Kuna Nini?

Nimepokea kwa Email: OFISI YA ARDHI KAHAMA KUNA NINI? Ndugu zangu,ninaomba mnisaidie kupata majibu sahihi kwa wanaohusika na suala hili. Mimi ni mwanchi wa Wilaya ya Kahama mtaka mabadiliko na maendeleo binafsi pamoja na Taifa zima.Mwezi wa tisa mwaka jana nilipeleka maombi yangu ya kuomba Hati milki ya kiwanja changu katika ofisi ya wilaya ya kahama.Wahusika wa ofisi hiyo walishughulikia suala hilo hadi kufikia mwisho wa upatikanaji wa Hati Milki.Baada tu ya kufikia mwisho wa hatua hiyo,kikajitokeza kizingiti cha mtu mmoja kuhitajika kuweka sahihi ya nyaraka hiyo ili baada ya hapo ipelekwe kwa Kamishna wa Kanda ili asaini na kuwa tayari Kabla haijasainiwa na Kamishna wa Kanda kuna mtu mmoja anaitwa Afisa Ardhi Mteule.Afisa mteule wilayani Kahama alishasimamishwa toka mwaka jana kwa matatizo yake yeye na waajiri wake na sikumbuki ni mwezi gani.Lakini cha Kusikitisha toka mwaka jana ofisi hiyo iko wazi hakuna mtu aliyewekwa hapo ili aweze kusaini nyaraka za wananchi wa Kahama.Kwa masikitiko makubwa ofisi hiyo haina hata kibali cha kuweka kaimu wa kukaimu kiti chake.Na kwa masikitiko zaidi mtu huyo mdogo hawezi kuteuliwa na mtu yeyote isipokuwa ngazi za juu sana. Huku chin yuko mwananchi ambaye alishafanya hatua zote za nyaraka zake pamoja na malipo ambayo tayari serikali ilishapokea na hata kutumia hela hizo kwa shughuli za serikali mimi mwananchi na mvuja jasho nyaraka zangu bado zimo ofisini kwa kisa cha kwamba Afisa Mteule hajateuliwa na wakubwa.Yanapofanyika haya,wapo tu watu mhimu kama vile Afisa Ardhi wilaya,Mkurugenzi,Mkuu wa Wilaya na hata kamishna wa Kanda kwa nini wasiteue mtu wa kuhudumia wananchi?Mimi ninajua yuko hapo kwa kusudi moja tu ni kuhudumia wananchi. Ukipata nafasi ya kuuliza jibu ni moja tu kuwa mtu huyo hajateuliwa,Je leo ni mwaka,atateuliwa lini ili huyo mwananchi naye apate nafasi ya kufanya maendeleo yake?jibu utapata kuwa hatujui,tunasubiri.Wakati huohuo serikali inahimiza maendeleo,bado serikali hiyo hiyo inazuia watu wasifanye maendeleo kwa kitendo cha dakika 10 tu mtu anakaa kwenye ofisi hiyo na anasaini kila kitu kwa siku moja lakini cha ajabu sahihi moja kwenye nyaraka unaingoja mwaka.Ndugu zangu wanamabadiliko hii ni kweli na sahihi kweli?Kwa picha hii inaonyesha wakubwa wana maslahi yao binafsi katika suala hili,maana kusingekuwa na maslahi,wakubwa wasingenyamaza katika suala hili kwa mwaka mzima huku mwananchi anaendelea kuumizwa.Au katika suala hili serikali iko wapi hapa?Kwa nini serikali inyamaze wakati mwananchi ametoa hela yake?Je sisi wananchi wa chini tukamuulize nani? Je nini kifanyike ili huyyo Afisa Ardhi Mteule Kahama ateuliwe ili wananchi waeze kupewa haki zao?Kama mimi nimmoja je wangapi wananchi wanaolia nyaraka zao hazijasainiwa kwa mwaka mzima? Je wakubwa hawalijui hili?na kama wanalijua kwa nini wako kimya kama kweli hawana maslahi katika hili? Ninaomba nipelekewe malalamiko na nipatiwe majibu toka kwa watu wafuatao; Mbunge wa Kahama mjini Waziri wa Ardhi na makazi. Naibu waziri wa Ardhi Kamishna wa Ardhi makao makuu Dar. Niwakilisha.

No comments: