TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13,
2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais
Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar
ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi
hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na
Taifa la Tanzania, Hayati
Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan
na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine
kujitawala ndani ya nchi yao
wenyewe.
Yalikuwa
ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya
kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar –
miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya
Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa
Michezo wa Amaan mjini Zanzibar
katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13,
2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment