Thursday, January 30, 2014

Tamko la Mh. John Malecela Kuunga Mkono Kauli ya Paul Makonda

 
Mh. John Samweli Malecela


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI --30/01/2014

Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.

Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.

Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.

Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?

Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.

Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.

Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?

Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.

Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.

Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.

Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.

Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.


JOHN SAMWELI MALECELA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

4 comments:

Anonymous said...

Mwaka 1995 sio mbali kwamba John hatambui makosa aliyoyafanya tena pia akiwa mtu mzima mwenye akili timamu zaidi ya sasa,unapotuambia kwamba katoa mchango wake kama mtu mzima ndipo binafsi nasema anazani tumesahau/tumesamehe??

Kwa kuwa njia anayosema sio sahihi na yeye alitaka kupita huko huko na anajua kwamba haikuwa sahihi na hajawahi kuomba radhi watz kwa uhuni aliotaka kutufanyia,sasa amepata wapi ujasiri leo wa kuikemea hadharani kwamba ni makosa, Kunyara unajua fika kwamba hapa jukwaani hakuna watoto na kama hizi ndio dalili za utu uzima basi inaleta shaka kwamba katika uzee wetu wengi wetu tutakuwa wendawazimu na useless katika jamii. Kuwa mtu mzima sio maana yake kila mchango unaotoa utakuwa na umuhimu.
Ikiwa pamoja na wewe unaetetea uhuni wa kitoto aliofanya huyu musee katika umri wake, naona kuna tatizo la busara ndani yenu. Mniwie ladhi kwa lugha

Anonymous said...

msingi mimi hapa sioni tatizo kwa John Malecela wala kwa ENL. Hizi ni mojawapo ya mikakati ya kila mtu katika kutafuta kitu Fulani. Unaweza kuwa na mkakati ambao wengine wanaweza kuuona kama ni threat kwa hiyo lazima upingwe kwa nguvu zote. Lakini pia unaweza kuwa na mkakati ambao ni legelege watu hawatashughulika na wewe.

Katika nadharia ya mikakati ipo mibaya na mizuri, kanuni kuu ni kutokata tama na kuwa na anti muda wote. Unapanga utakavyofanya na unaweka na possibilities za kupingwa na jinsi utakavyoshughulika nazo.

Hili ndilo limetokea hapa, ukiwa kwenye mkakati wakati mwingine huoni upande wa pili, sasa ukiwa muungwana lazima pia uwe na utaratibu wa kupata feedback na uwe na mkakati wa jinsi ya kushughulika nao.

Mkakati wa ENL kuingia NEC siyo tatizo wala hauwezi kuwa kigezo cha kukubaliwa na NEC yenyewe au wengine wapinga kura there after. Kuna hatua kubwa zaidi inatakiwa kupigwa kwa strategist wanajua hilo.

Wengine wana mkakati wa kimya ambao katika political scientist mara nyingi wanausema haufai na hauzai matunda matunda ya haraka japokuwa ukifanikiwa huwa unatoa matokeo ya muda mrefu kuliko mkakati wa kutaka kujulikana haraka.

All in all Samweli katoa mchango na mtizamo wake kama mtu mzima, mtu anapoubeza kwa ukweli ana matatatizo na akili yake. Mniwie radhi kwa lugha hiyo.

Alfred said...

ah nae yumo kumbe....mzee malechela hakuna cha kumbuka, saana alichokifanya kipindi chake ni kutaka kuvunja muuunganio......hana hoja huyu mzee, naona na kauzee kanamfanya achemke, hakuna kipya hapo
kiukwweli kampeni za kisasa lazima pesa na mbinu zitumike, friends of lowassa si jambo baya hata kidogo...kumbukeni jamanai friend of slaa, friend s of obAMA NK
PESA zinatoka wapi ni kwa wale wanamtaka Rais awo awe lowassa, kwani ni siri....tunamtaka kwasababu anafaa, sasa nani wa kumzuia? ajitokeze tumwone

Anonymous said...

Dah! Watu wa Lowassa wako kila mahali. The web is crawling with Lowassa's foot soldiers. Kazi ipo.