Saturday, June 20, 2015

Tanzia - Florence Dyauli, Mtangazaji wa TBC

 Nimesikitika sana kusika habari ya kifo cha Dada Florence Dyauli.  Nilifanya kazi naye nilipokuwa Practical Training RTD nikiwa mwanafunzi Tanzania School of Journalism. Pia tulikuwa pamoja kwenye shughuli za TAMWA.  Rest in peace Dada Florence.

*************************************************

KUTOKA LUKWANGULE BLOG:


The Late Florence Dyauli (1961-2015)

MWANDISHI wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa upande wa Televisheni Florence Dyauli amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Rabininsia memorial iliyopo jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kutokana kusumbuliwa na maradhi ya Nimonia

Taarifa iliyotolewa jana na ofisi za TBC ilisema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Nimonia na alilazwa kwa ajili ya matibabu hadi jana usiku mauti ilipomfika.

Taratibu za mazishi zilikuwa bado hazijafanyika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo ya Rabininsia ukisubiria taratibu za mazishi kutoka kwa ndugu wa familia.

Florence alizaliwa Julai 27, 1961 ambapo alipata elimu yake ya msingi kuanzia 1968 hadi mwaka 1975 katika shule ya Msingi Chang’ombe iliyopo jijini Dar es salaam.

Alifanikiwa kujiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Kisutu girls kati ya mwaka 1976 hadi 1979. Baadae alijiunga na chuo cha Tabora secretarial College kuanzia mwaka 1980 hadi 1981 na kujipatia mafunzo ya cheti cha ukarani.

Mnamo mwaka 1986 hadi 1988 alijiunga na chuo cha uandishi wa habari kwa ngazi ya stashahada ya uandishi wa habari.

Aliniajiriwa kama mwandishi wa habari msaidizi katika kituo cha Radio Tanzania Dar es salaam kuanzia 1982 hadi Novemba 1999.

Kisha mwaka 1994 hadi Novemba 1999 alikuwa Shift Editor .

Hadi mauti inamkuta, marehemu alikuwa mwandishi wa habari daraja la kwanza kwa upande wa Televisheni ya Taifa TBC.

No comments: