Saturday, October 17, 2015

Ajali ya Helicopter Iliyomwua Mh. Deo Filikunjombe

Wadau, wengi mnafahamu kuwa asili yangu ni Manda, Ludewa, mkoa wa Iringa. Huko kuna usemi, ukiwa Mbunge, lazima ufe ukiwa umeshika wadhifa huu.  Wanaonya wanaotaka kugombea nafasi hiyo wasigombee. Nilikuwa nasema ni maneno tu, na coindence. Lakini sasa ninawaza kuwa wazee walisema kweli.  Maana, waliokufa wakiwa wabunge wa Ludewa ni binamu wa baba yangu, Mh. Horace Kolimba (1939 -1997), na baba yangu mdogo Mh. Prof. Crispin Che-Mponda Hauli (1941-2000).  

Sasa amefariki mh. Deogratius Haule Filikunjombe. Duh!  Amefariki katika ajali ya Helikopta katika mbuga ya wanyama ya Selous. Alikuwa akitokea Dar kwenda Ludewa kwenye shughuli za kampeni. Katika ajali hiyo amekufa rubani wa helikopta hiyo Capt. William Silaa, ndugu wa Filikunjombe, Plasdus Haule, na mfanyakazi wa Halmashauri ya Ludewa. Mtoto wa rubani alisema kuwa  helikopta hiyo ilipata matatizo ya injini kabla ya kuanguka kwake na kuteketea kwa moto.

Mwenyezi mungu alaze roho zao mahal pema mbinguni. Amen.

Close-up (Picha ya karibu) ya helicopter aliyokuwa anatumia Mh. FIlikunjombe kwenye shughuli za kampeni.


Mwili wa Deo Filikunjombe ukitolewa Eneo la tukio baada ya kuteketea kwa Moto kufuatia ajali ya helkopta.
Mabaki ya Ajali ya Helicopter. Mh. Deo Filikunjombe na wengine watatu walifariki katika ajali hiyo Selous Reserve
Mabaki ya Ajali ya Helicopter. Mh. Deo Filikunjombe na wengine watatu walifariki katika ajali hiyo Selous Reserve
Rubani Maarufu Captain William Silaa (enzi za uhai wake) ndiye alikuwa anaendesha helicoopter hiyo
Helicopter Aliyokuwa anaitumia Mh. Deo Filikunjombe ikiwa anagani
Helicopter aliyokuwa anaitumia Mh. Deo Filikunjombe
Mh. Deo Filikunjombe (enzi za uhai wake) akiaanga na wananchi wa Ludewa
Mh. Deogratius Filikunjombe (1972 -2015)

13 comments:

Zawadi L said...

Leo nimeelewe wa Tanzania walivyojisikia 12/04/ 1984 alipo fariki Sokoine. Deo Filikunjombe mungu wa mbinguni akupokee na fungu lako akupe, pumzika kwa amani.

Anonymous said...

Aisee, hivi vifo vya wanasiasa vinatisha!!!!
Wana maombi tuombe sana Mungu

Anonymous said...

Tanzania , inabidi tuombe mungu sio bure , viongozi wanakufa mfululizo , kuna mahali tumekosea kama taifa , mungu anatuonyesha

Anonymous said...

Hili ni ghalika! Uwepo wa Mungu unahitajika sana.. R.I.P.

Anonymous said...

Deo umeondoka! Hakuna tena ambae atashawishi watu kuipenda ccm ww ulikuwa ni wa pekee hakuna wa kufananishwa na ww ndani ya ccm Mwakyembe, alisha potea hivyo bc ccm inazidi kuzama !

JFK said...

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe sababu ni katika kufa ndipo tunapata uzima wa milele RIP Deo.

Anonymous said...

Wote tutakufa/ Kila mtu ataondoka na staili yake. Rest in peace.

Anonymous said...

Wengine walikuwa kwenye timu ya operation bao la mkono.
Pia huyu ndugu yetu Deo Filiku hali akijua udhalimu wa ccm bado akaendelea kuwaunga mkono,basi mimi ninaamini hii ajali ni Mungu ametaka kuwaonya wale aliowapa ufunuo wa udhalimu wa CCM kwa wa-Tanzania.
Mapenzi yake yatimizwe.
Amen.

Anonymous said...

Pumzika kwa Amani Kiongozi wa kweli,hakika pengo lako halitazibika.

Anonymous said...

Pumzika kwa amani Deo , kazi aliyokutuma Bwana umeimaliza.

Anonymous said...

Kule mwanza wenyewe wanaendelea kukata viuno.....pumzika kwa amani kamanda...poleni wana-Ludewa na watanzania kwa ujumla

Anonymous said...

Dah ni pigo kubwa kwa Taifa, R.I.P. Kaptain Slaa na Jembe letu Deo Filikunjombe, tutamkumbuka daima jamani

Gideon said...

Tanzania inalia,Njombe tunalia,na Ludewa wanalia zaidi.Ndani ya miezi 6,mungu kailiza jamii ya wana-Ludewa mara tatu.Mungu katuchukulia wapendwa wetu:Dr.Alec che Mponda,Rev.Christopher Reuben Mtikila na kijana wetu,mchapa kazi na kipenzi cha watu Deogratius Haule Filikunjombe.
Poleni sana Ludewa,barabara,migodi ya makaa na chuma na umeme alivyovileta Deo,mvitumie vema kwa manufaa ya maendeleo endelevu,kwenu na kwa watoto wenu,huku AKIILAZA MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MPENDWA WETU Deo Haule Filikunjombe.