Saturday, November 07, 2015

George Masaju Ateuliwa Tena kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

GEORGE  MASAJU ATEULIWA  TENA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
Na
Happiness Katabazi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju
RAIS  Dk.John Magufuli ambaye leo ameapishwa kushika wadhifa wao kuwa Rais , Leo amemteua George Mcheche Masaju Kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ataapishwa Kesho Ikulu Dar Es Salaam.

Rais Dk.Magufuli ameitisha Bunge Novemba 17 mjini Dodoma na Novemba 19 atapendekeza jina la Waziri Mkuu. Leo ni mara ya pili Masaju kuteuliwa kushika wadhifa huo ,mara ya kwanza ilikuwa ni serikali ya awamu ya nne  Januari 2 Mwaka huu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amestaafu
wadhifa wa Cheo cha Rais , alimteua Masaju Kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali baada ya siku Chake aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kujihudhuru wadhifa
huo.

Oktoba 20 Mwaka huu, nilimtembelea ofisini kwake Mtani wangu Masaju na kufanya nae mahojiano
ambayo niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha Habari  ( MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ATOA SOMO LA SHERIA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU).

Masaju ni miongoni mwa Wanasheria wa serikali wazalendo na wanaowaaminiwa kiutendaji na ndiyo maana zilipokuwa zikifunguliwa Kesi ambazo zilikuwa zikivuta hisia za watu
Wengi Masaju alikuwa akivaa suti na gauni lake la uwakili na kutinga Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu na kuiendesha Kesi hiyo yeye Mwenyewe akisaidiwana na vijana wake.

Na nilipokuwa Mwandishi wa Habari za mahakamani,nilipokuwa nikimuona Masaju Kubeba gauni jeusi na begi lilokuwa na Nyaraka za kuendeshea Kesi basi nilikuwa Nasema Kimolo moyo Kuwa upande wa wa pili Katika Kesi hiyo ujiandae kikamilifu.

Ushahidi mchache wa haya ninayoyasema kuhusu Masaju ambayo nilikushuhudia kwa
macho yangu mwanzo hadi Mwisho ni Rufaa ya Kesi maarufu ya mgombea Binafsi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila Katika Mahakama ya Rufaa
nchini Masaju alikuwa kiongozi wa Mawakili wa serikali kuendesha Kesi hiyo ya kihistoria ambayo ikisikilzwa na jopo la Majaji Saba waliokuwa wakiongozwa na Jaji Mkuu wa wakati
huo , Agustino Ramadhani,  Masaju alifanikiwa Kujenga hoja na hatimaye jopo lilikubaliana naye na kutengua hukumu ya Mahakama Kuu ambayo iliruhurusu Mgombea Binafsi.

Ushahidi wa pili, ni Mwaka Jana , katika kesi ya Kikatiba Na.24/2013. Masaju aliwakilisha upande wa Mwanasheria Mkuu Katika Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Kituo ca Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)dhidi ya Waziri Mkuu iliyokuwa ukiomba Mahakama Kuu itoe Tafsiri ya Ibara ya 100 Kuwa wabunge wana Uhuru bila
mipaka kwani Pinda alitoa Kauli Bunge akitaka Polisi iwapige wanaovunja Sheria za nchi.
Juni 6 Mwaka 2014 , Jopo la Majaji wa Tatu wa Mahakama Kuu Dar es Salaam, Fakji Jundu, Dk.Fauz Twaibu na Augustine Mwarija walitoa uamuzi wa Kuitupa Kesi hiyo  kwa sababu Imeona walalamikaji walikuwa hawana Haki ya kisheria ya kushitaki Pinda.

Jopo hilo lilitoa uamuzi huo jana ambapo jaji Jaji Jundu alisema anakubaliana na pingamizi la
awali lilowasilishwa na wakili wa mdaiwa (Pinda), Ambaye ni Naibu Mwanasheri Mkuu wa Serikali,  George Masaju, ambalo  lilikuwa likiomba  Mahakama itoe amri ya kuifuta Kesi hiyo kwasababu walalamikaji hawana Haki a kisheria ya kuwashitaki wadaiwa na kwamba Waliokuwa na Haki ya kushitaki Pinda ni wananchi na siyo Taasisi hizo za walalamikaji.OLHRC na TLS walimshtakiwa Waziri Mkuu Pinda pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kauli aliyoitoa bungeni Juni 20 mwaka 2013. Ilidaiwa Katika   kipindi cha maswali ya papo kwa papo Waziri Pinda akijibu alisema, ‘ukifanya fujo…unaambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi, utapigwa tu, muwapige tu
sababu tumechoka’.

 Jaji Jundu alisema, Masaju Aliwasilisha  pingamizi la awali akiomba  kesi hiyo itupwe
kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kuisikiliza, waliofungua hawakustahili kuifungua na iko kwa ajili ya kupoteza Muda wa Mahakama. Katika uamuzi huo, majaji walikubaliana na hoja tatu za pingamizi kuwa walalamikaji katika kesi hiyo hawakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo na
kwamba walikosea taratibu za ufunguaji wa kesi kama hizo kwa kuwa walikiuka amri na kanuni zinazoongoza Mashauri ya Madai (CPC).

Katika hoja ya kwanza kuwa Pinda kama mbunge analindwa na Katiba, jopo hilo lilisema kuwa ni kweli wabunge wanalindwa na Katiba Ibara ya 100 (1) kuhusu haki na upendeleo (Previledge), yaani haki na uhuru wa mjadala na maoni. Hata hivyo, lilikataa hoja za utetezi kuwa wabunge wana kinga isiyo na mipaka ya kutokushtakiwa kwa kauli au jambo lolote walilolitamka bungeni. “Ibara ya
100(1) ya Katiba haiwezi kujadiliwa mahali popote ikiwemo mahakamani, ibara hiyo inasema kwamba, kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo
hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

“Ibara ya 100(2) inaweza kujadiliwa mahakamani, inasema kwamba bila kuathiri katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yoyote hatashtakiwa au kufunguliwa
shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

“Mwananchi mmoja mmoja aliyeathika na jambo lililozungumzwa na mbunge bungeni anaweza kushtaki lakini si taasisi kama ilivyo katika kesi hii,”alisema.Alisema kutokana na sababu hizo,
mahakama inatupilia mbali kesi hiyo kwa sababu waliofungua kesi, LHRC na TLS hawakustahili kisheria kufungua kesi hiyo kwa sababu hawakuathirika. Kesi ya Tatu ni Kesi iliyofuta hisia
za watu Wengi ni Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa Mwaka Jana na Mwandishi wa Habari Saed Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Kubenea alikuwa anaomba Mahakama hiyo itoe amri ya muda ya Kuzuia Bunge  Maalum la Katiba lisiendelee na kazi kwasababu linavunja Sheria .Hata hivyo Masaju aliwasilisha mapingamizi
mawili  ambayo yaliomba Mahakama hiyo itupilie Mbali Maombi ya Kubenea Kwani hayana Msingi na Mahakama hiyo ilitupilia mbali Maombi ya Kubenea na Bunge linaendelea na kazi zake.

Mifano ni mingi ya Kuonyesha Masaju Kabla ya kuteuliwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Januari 2 na Novemba 5 Mwaka huu , kuna kazi nzuri ya kuiwakilisha upande wa serikali Katika Kesi mbalimbali mahakamani aliifanya hivyo anastahili. Ni neema ya Mungu na na rekodi yake
ya Utendaji Kazi ndiyo imesabisha rais mpya Dk.Magufuli amteue kushika wadhifa huo ili amsaidie kuchapa Kazi Kati serikali yake ya awamu ya tano.  Hongera sana. Wosia wangu wa
Masaju endelea na msimamo wako ule ule wa kusimamia haki na Kusema ukweli bila woga. Tunaokufahamu Tunaokufahamu Kuwa una sifa hizi. 

 Masaju ni mtu asiye penda kuburuzwa   na mambumbumbu wa Sheria, ni mtu anayejali utu,heshima na Kupenda watu watii Sheria za nchi na ni mzalendo kwa taifa lake.

Hongera Mtani wangu Masaju, mungu akuongoze katika uteuzi huu mpya ugaidi kulitumikia taifa
letu. Hapa Kazi Tu.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi0716

774494Blogg:www.katabazihappy.blogspot.com5/11/2015.

No comments: