Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye, na migu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wote wawili kufariki dunia.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa kumpata daktari bingwa wa mifupa . Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-
Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
2 comments:
Wataalamu nisaidieni; kuna umuhimu gani ya kupima kwa both CT Scan na MRI?
Kuvunjika mifupa sioni kama kunahitaji vipimp vyote hivyo. Na kukaa muda wote pale rufaa mbeya nini kilikuwa kinafanyika, MNH wamefanya nini?
Sasa tunachunguza nini? Mfupa uliovunjika muda huo au itakuwa malunion au osteomyelitis tunalenda nini hasa?
Nashauri kama inawezekana arudu rufaa au anaye msaidia aende rufaa amuone daktari bingwa wa x-ray Dr, Humfrey amabaye ni naibu mkurugenzi, ajaribu kujua nini hasa ikibidi mueleze nimeombwa na Rukoma, namba ya simu yangu ipo hapo chini
Post a Comment