Thursday, October 29, 2015

Ushindi wa Rais Mteule Dr. John Magufuli Katika Vyombo Vya Habari Vya Kimataifa

Na Mdau Msema Kweli
http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/10/MAGUFULI-1.jpg
Rais Mteule Mh. John Pombe Magufuli
 USHINDI WA RAIS MTEULE DKT JOHN MAGUFULI WAFUNIKA KIMATAIFA

Ushindi wa Rais Meteule wa Tanzannia John Magufuli aka Tingatinga (The Bulldozer) umefunika vianzo vya habari vya kimataifa katika kila kona ya dunia.
Kufunika kwa ushundi wa mgombea wa CCM katika kiti cha urais Dkt.John Magufuli inadhihirisha wazi kuwa nchi ya Tanzania ni kioo cha amani duniani,
kwani watanzania wamefanya mahamuzi sahii kwa amani bila kuwapo na uvunjifu
wa amani,tofouti na nchi nyingi duniani kila panapokuwa na uchaguzi basi raia wataishi kwa mashaka.
Mungu Ibariki Tanzania tupia jicho baadhi ya link:


BBC-London

New York

 Kenya


UGANDA:

Germany:


AUSTRIA:

Rwanda:

UAE;

Honourable John Magufuli wins Tanzania Election

   DAR ES SALAAM, Tanzania (AP) - Tanzania's ruling party has won the country's presidential election, defeating an opposition alliance that had hoped to end the party's five-decade grip on power, the country's election commission announced on Thursday.

   John Magufuli, the Chama Cha Mapinduzi (Revolutionary Party) candidate, won with 58 percent of the votes cast. Edward Lowassa of the Chadema party and who was also backed by three other parties, got 40 percent of votes, said Damian Lubuva, the head of the election commission. He made the announcement in Tanzania's commercial capital, Dar es Salaam.

   Magufuli has been serving as public works minister in the government of the outgoing president, Jakaya Kikwete. Lowassa, who served as prime minister from 2005 to 2008, used to belong to the ruling party but defected after failing to become its presidential candidate.

   Both candidates drew crowds during campaigns across the country and it was the country's closest election.

   Lowassa said Wednesday he is disputing some results and wants a recount, and accused the election commission of posting some false results in favor of Magufuli.

   The semi-autonomous island archipelago of Zanzibar also voted for its own president and other local leaders, but the results were nullified Wednesday over allegations of voting irregularities. The opposition Civic United Front had claimed victory in Zanzibar's presidential election.

   International observers said in a joint statement Thursday they were concerned by the decision to annul the Zanzibar results after what they said was a credible election.

   "Democracy, peace and unity in Zanzibar is at stake," the statement said.

   Tanzania was formed when Zanzibar and Pemba island united with mainland Tanganyika in April 1964, three months after the islands' black majority overthrew the traditional Arab rulers.  For years, many have felt that Zanzibar, and its ancient capital, Stone Town, have been relegated to second-class status.

Saturday, October 24, 2015

"Magufuli Asipopita Sitombwi! "- Mshabiki wa CCM


Ushabiki wa Uchaguzi safari hii ni balaa! Watu watanyimnana uroda kweli mtu wao asipopitwa!

Uchaguzi - Tanzania 2015 - Tunaomba kuwe na Amani Tanzania

Wadau,  WaTanzania wa Disapora wanaomba Uchaguzi 2015 upite kwa AMANI.

Mungu awabariki wagombea na waTanzania.

May the Best Man win!


Wagombea Wakuu ni Mh. Edward Lowassa (UKAWA) na Mh. John Pombe Magufuli (CCM)

2,177 Dead in Hajj Stampede including 20 Tanzanians

   DUBAI, United Arab Emirates (AP) - The crush and stampede that struck the hajj last month in Saudi Arabia killed at least 2,177 pilgrims, a new Associated Press tally showed Monday, after officials in the kingdom met to discuss the tragedy.

   The toll keeps rising from the Sept. 24 disaster outside Mecca as individual countries identify bodies and work to determine the whereabouts of hundreds of pilgrims still missing. The official Saudi toll of 769 people killed and 934 injured has not changed since Sept. 26, and officials have yet to address the discrepancy.

   Crown Prince Mohammed bin Naif bin Abdul Aziz, who is also the kingdom's interior minister, oversaw a meeting late Sunday about the disaster in Mina, according to the official Saudi Press Agency. The agency's report did not mention any official response to the rising death toll.

   "The crown prince was reassured on the progress of the investigations," the SPA report said. "He directed the committee's members to continue their efforts to find the causes of the accident, praying to Allah Almighty to accept the martyrs and wishing the injured a speedy recovery."

   King Salman ordered the investigation into the disaster, the deadliest in the history of the annual pilgrimage. It came after a crane collapse in Mecca earlier that month killed 111 worshippers, and the twin disasters marred the first hajj to be overseen by the king since he ascended to the throne at the start of this year.
Hajj Pilgrims

   The Saudi king holds the title of "Custodian of the Two Holy Mosques," and the monarchy's supervision of the hajj is a source of great prestige in the Muslim world. Riyadh has rejected a suggestion by Shiite power Iran, its main regional rival, to have an independent body take over planning and administering the five-day hajj pilgrimage, which is required of all able-bodied Muslims once in their lifetimes.

   Iran has repeatedly blamed the disaster on the Saudi royal family, accusing it of mismanagement and of covering up the real death toll, which Tehran says exceeds 4,700, without providing evidence.

   "The lying and hypercritical bodies, which claim to (be promoting) human rights, as well as the Western governments, which sometimes make great fuss over the death of a single person, remained dead silent in this incident in favor of their allied government," Iran's Supreme Leader Ayatollah Ali Khamenei said Monday, according to a transcript on his website.

Bodies of Hajj Stampede Victims
   "If they were sincere, these self-proclaimed advocates of human rights should have demanded accountability, compensation, guarantee for non-recurrence and punishment for the perpetrators of this catastrophe."

   Iran and Saudi Arabia are deeply divided on a host of regional issues and back opposite sides in the wars in Syria and Yemen, where a Saudi-led coalition has been at war with Iran-backed Shiite rebels, known as Houthis, since March.

   Saudi Arabia has meanwhile been targeted in gun and bomb attacks by an affiliate of the extremist Islamic State group, which holds a third of Iraq and Syria in its self-declared "caliphate." Like al-Qaida before it, the IS group views the Saudi royal family as illegitimate because of alleged corruption and its alliance with the United States.

   The AP count of the dead from the Mina crush and stampede comes from state media reports and officials' comments from 30 of the over 180 countries that sent citizens to the hajj.

   Iran leads all the affected countries, saying it had 465 pilgrims killed. Many of the dead also came from Africa. Mali said it lost 254 people, while Nigeria lost 199, Cameroon lost 76, Niger lost 72, Senegal lost 61, and Ivory Coast and Benin both lost 52.

   Others include Egypt with 182, Bangladesh with 137, Indonesia with 126, India with 116, Pakistan with 102, Ethiopia with 47, Chad with 43, Morocco with 36, Algeria with 33, Sudan with 30, Burkina Faso with 22, Tanzania with 20, Somalia with 10, Kenya with eight, Ghana and Turkey with seven, Myanmar and Libya with six, China with four, Afghanistan with two and Jordan and Malaysia with one.

   The previous deadliest-ever incident at hajj was a 1990 stampede that killed 1,426 people.

Push - Ups za Wagombea 2015

Mh. Magufuli anaonyesha vitu vyake

 
Mgombea Mwenza, Mama Samia Suluhu Aonyesha naye yumo!
Mgombea ubuge jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha mwenye shati la njano akipiga push up sambamba na wagombea Udiwani.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni ...
WaTanzania wanashangaa viongozi wakipiga push-ups hdharani. Mbona hata Rais Obama anapiga push-off kuonyeshs yuko fiti!
Power Toto naye anaonyesha vitu vyake!

Friday, October 23, 2015

Ewe Mgombea, Wekeza Katika Kuwalinda Watoto Wachanga na Wasichana dhidi ya VVU



Maendeleo makubwa yamepatikana katika kupunguza kuenea kwa VVU.
Hata hivyo, ambukizo moja katika kila maambukizo kumi mapya huwapata watoto wanaozaliwa japokuwa asilimia 90 ya maambikizi haya yangeweza kuzuilika. Wasichana pia wamo hatarini zaidi kuambukizwa VVU kuliko wavulana. Kila ambukizo jipya la kijana aliye chini ya miaka ishirini linadhihirisha kushindwa kuwapatia vijana elimu ya afya ya uzazi, taarifa, stadi na huduma zitakazowawezesha kujilinda. Unyanyapaa na ubaguzi vinaendelea kudhoofisha uwezekano wa wanawake kupata huduma.
Fanya kazi pamoja na washiriki wote katika kupanua huduma na matibabu yatakayoangamiza kabisa maambukizi ya VVU ya mama kwa mtoto ifikapo mwaka 2015. Hakikisha kuwa watoto wote wenye VVU na UKIMWI wanapata matibabu wanayoyahitaji.
Toa ahadi ya kuongeza rasilimali katika kuwakinga vijana, hasa wasichana dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kuunga mkono mpango wa kitaifa wa kuzuia VVU.
Saidia katika kuanzisha huduma za afya zinazowalenga vijana na mipango madhubuti ya stadi za maisha ambazo zitawapa taarifa na kuwawezesha, hasa wasichana kupunguza uwezekano wao wa kuambukizwa VVU na UKIMWI.

Saturday, October 17, 2015

Ajali ya Helicopter Iliyomwua Mh. Deo Filikunjombe

Wadau, wengi mnafahamu kuwa asili yangu ni Manda, Ludewa, mkoa wa Iringa. Huko kuna usemi, ukiwa Mbunge, lazima ufe ukiwa umeshika wadhifa huu.  Wanaonya wanaotaka kugombea nafasi hiyo wasigombee. Nilikuwa nasema ni maneno tu, na coindence. Lakini sasa ninawaza kuwa wazee walisema kweli.  Maana, waliokufa wakiwa wabunge wa Ludewa ni binamu wa baba yangu, Mh. Horace Kolimba (1939 -1997), na baba yangu mdogo Mh. Prof. Crispin Che-Mponda Hauli (1941-2000).  

Sasa amefariki mh. Deogratius Haule Filikunjombe. Duh!  Amefariki katika ajali ya Helikopta katika mbuga ya wanyama ya Selous. Alikuwa akitokea Dar kwenda Ludewa kwenye shughuli za kampeni. Katika ajali hiyo amekufa rubani wa helikopta hiyo Capt. William Silaa, ndugu wa Filikunjombe, Plasdus Haule, na mfanyakazi wa Halmashauri ya Ludewa. Mtoto wa rubani alisema kuwa  helikopta hiyo ilipata matatizo ya injini kabla ya kuanguka kwake na kuteketea kwa moto.

Mwenyezi mungu alaze roho zao mahal pema mbinguni. Amen.

Close-up (Picha ya karibu) ya helicopter aliyokuwa anatumia Mh. FIlikunjombe kwenye shughuli za kampeni.


Mwili wa Deo Filikunjombe ukitolewa Eneo la tukio baada ya kuteketea kwa Moto kufuatia ajali ya helkopta.
Mabaki ya Ajali ya Helicopter. Mh. Deo Filikunjombe na wengine watatu walifariki katika ajali hiyo Selous Reserve
Mabaki ya Ajali ya Helicopter. Mh. Deo Filikunjombe na wengine watatu walifariki katika ajali hiyo Selous Reserve
Rubani Maarufu Captain William Silaa (enzi za uhai wake) ndiye alikuwa anaendesha helicoopter hiyo
Helicopter Aliyokuwa anaitumia Mh. Deo Filikunjombe ikiwa anagani
Helicopter aliyokuwa anaitumia Mh. Deo Filikunjombe
Mh. Deo Filikunjombe (enzi za uhai wake) akiaanga na wananchi wa Ludewa
Mh. Deogratius Filikunjombe (1972 -2015)

Friday, October 16, 2015

Tanzia - Mh. Deo Filikunjombe na Captain William Silaa


RIP Mbunge wetu wa Ludewa, Mh. Deo Filikunjombe. Doh! Nimepokea habari za msiba kwa masikitiko makubwa.  Poleni wanakunyumba.

Mwenyezi Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. Amen.

Saturday, October 10, 2015

Faida ya Kuzeeka!

Ukizeeka, kweli unajali maneno ya watu???!!!!

Saturday, October 03, 2015

Mwanaume si Lazima Ashindane na Mbwa!

Uwe na mwanamke moja na uheshimu! Si lazima utembee na wengi ili kuonyesha wewe eti ni dume!

Wednesday, September 30, 2015

Tanzia - Mama Betisheba Ketangenyi

Bettisheba Pole Ketang'enyi enzi ya uhai wake

Tunasikitika kutangaza kifo cha mama Betisheba Ketangenyi, mama yake Yvonne Matinyi, Felicia Simms, Fredderek Ketangenyi pia ni Dada yake na Rossie Musika, Neema Musika, Daudi Musika, Sijaona Musika kilichotekea 9/30/15 katika hospitali ya NIH Maryland mipango ya kusafiri mwili wa marehemu inaendelea kwa mdogo wa marehemu Daudi Musika
3819 Gateway terrace Burtonsville MD 20866
Unaweza kuwasiliana
Rossie Musika 240 408 2693
Neema Musika 571 991 9819
Specioser Musika 571332 2215
Sijaona Musika 202 487 8412

Panya ni Mbogo huko China!

Mchina akitayarisha mboga ya Panya buku!

Wadau mnaopenda kula kwenye Chinese Restaurant, halahala! Wachina wanapenda sana kula panya. Utaagiza pork fried rice kumbe unapata panya fried rice.  Au unaagiza Chicken Chow Mein, unapata, Panya Chow Mein.  Angalia vile vyakula vyenye nyama zisizojulikana kumba ni nyama ya paka au pamya.

Tuesday, September 29, 2015

Uzazi wa Majira Usiohitaji Dawa- Akina Dada Mpoooooo!


Wasichana wengi Sekondari waliponea kupata mimba kwa kutumia njia hii ya Uzazi wa Majira (Rhythm Method) enzi zileeee.   Unahesabu siku zako.  Pia kupima ute. Pia tulionywa kuwa shahawa za mwanaume zinaweza kukaa ukeni siku nne zikisubiri yai!!!!

Mo Dewji Kuanzisha Benki Kwa Ajili ya Wafanyabiashara Ndogo ndogo

DSC_0316

CEO wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.

Na Modewjiblog team

Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015) amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group, hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia kuajiri wafanyakazi zaidi ya Laki moja.

Dewji maarufu kama MO amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum ya moja kwa moja yaliyorushwa hivi karibuni na kituo cha BBC kupitia kipindi cha BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA ambapo alibainisha hayo.

Kupitia kipindi hicho cha BBC Swahili, MO aliweza kuelezea mafanikio aliyofikia ikiwemo siri ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma.

Ambapo ameeleza kuwa, alianza biashara akiwa mdogo sana kwani wakati huo Baba yake alikuwa akimfundisha kazi na yeye kujituma zaidi bila kuchoka.

Aidha, MO amebainisha kuwa, yupo mbioni kuanzisha Benki ya kuweza kutoa mikopo midogo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujiendeleza.

DSC_0310

Salim Kikeke aliweza kumuuliza swali juu ya vijana wengi wanapenda kufanyabiashara lakini hawana mitaji ambapo MO alifunguka kuwa:

“Unajua na mimi mwenyewe nataka kuanzisha ‘Micro credit bank’, ya kuweza kutoa mikopo midogomidogo kwa wafanyabiashara wadogo. Kwa sasa hivi kuna benk nyingi sana zimezidi ukilinganisha mwaka 1998, nilipotoka Marekani, benki zilikuwa ndogo sana kwa hiyo nimeanza kutafuta pesa kutoka benki za Afrika Kusini” ameeleza MO na kuongeza kuwa mtu unapokuwa na wazo la kuanzisha biashara unaweza kushirikiana na mwenye pesa ama kukopa kwa mtu mwenye pesa. alifafanua MO .

Katika mahojiano hayo, MO alibainisha kuwa, mapato katika akaunti ya MeTL GROUP ina kiasi cha dola bilioni 1.3 huku akiwa ameajiri watu zaidi ya 24,000 huku lengo hadi kufikia mwaka 2022, kuwa na wafanyakazi zaidi ya Laki moja huku mapato kuwa zaidi ya dola bilioni 5.

Tuzo aliyopata MO alikabidhiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.

MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.

Friday, September 25, 2015

Mkuu wa Majeshi CDF Jenerali David Mwamunyange Yu Buheri wa Afya - Yupo Italia Kikazi

 Taarifa zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali  Davis Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hazina ukweli wowote.Ni uzushi.

Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kama anavyoonekana pichani na hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.
Hii ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kuthibiti uongo kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.
Wananchi wengie waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji endapo kama kweli TCRA ipo na kama ipo ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber Law) iliyoanza kutumika.
"Endapo kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu ya Jamii katika maoni yake.

Thursday, September 24, 2015

Ibada ya Kiswahili Katoliki - Dayosisi ya Cleveland East

IBADA YA KISWAHILI KANISA KATOLIKI DAYOSIS YA CLEVELAND EAST
 
KARIBUNI
 
Wapendwa wakristo mnkaribishwa kushiriki sherehe ya kutimiza mwaka
mmoja wa ibada ya Kiswahili kanisa letu Katoliki Dayosis ya Cleveland.
Ibada itaanza saa kumi jioni, na baada ya ibada kutakuwa na chakula na
vinywaji, pia kubadilishana mawazo.
Ibada hii itafanyika;
 
St Adelbert Church
East 83 Street,
Cleveland Ohio 44103
 
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu zifuatazo;
Father. F. January 216 650 2734
Father Rogerio. 267 206 2613
Tumaini. 216 645 5171

Iddi Mbaraka!


Nawatakia wadau wote waislam Iddi Mbaraka!

Tuesday, September 22, 2015

Mke Atalakiwa baada ya kuondoa Make-Up Usoni. Kumbe ana sura mbaya!

Yaani nimecheka. Jamaa kaoa mwanamke huko Arabuni kwa sababu ya uzuri wake. Kumbe alikuwa ana paka make-up kibao na kupachika nyusi bandia!  Jamaa alifunga ndoa na mrembo wake. Asubuhi baada ya harusi waliyoamka alishngaa huyo mwanamke ni nani.Kumbe ni mke wake bila make up. DUHHHHH! Danganya toto kweli kweli!  Lakini huyo mwanamke siyo mbaya, na jamaa mshamba hajui kazi ya make-up.