Thursday, July 12, 2007

Dar es Salaam

Salamu nyingi sana kutoka Dar es Salaam. Kwa kweli hali ya hewa siyo joto kama iliyokuwa nilivyokujwa mwaka jana Novemba. Kwa sasa hali ya hewa siyo mbaya. Kwa mara ya kwanza umeme umekatika hapa kwetu Mbezi Beach. Hii cafe wana generator, ila air condition haifanyi kazi ni joto balaa.

Ila bado kuna mavumbi na msongamano wa magari umezidi kuwa mbaya mno. (TRAFFIC JAMS). Nimekwisha shuhudia accident za magari kama nne hivi. Bahati hakuna aliyeumia, ila magari yao ndo yaliumia.

Filmming ya Bongoland II inaenda vizuri sana. Tuko na wasanni maarufu wa hapa Mzee Olutu, Shafii, na mama mjatta. Wanafanya kazi nzuri sana. Bongoland II itakuwa safi sana.

Ila bado nalalamika, internet connection nayo tumia ni mbaya. Niko Mbezi Squre, Silver cafe, na naona kila mtu anapta shida kufungua site wanazotaka, mpaka watu wana hama hama computa. Bado sijaweza kufungua site ya Michuzi, na site yangu ila naingia kupitia blogu moderation.

Nina picha nyingi za kubandika. Haya siku nyingine. Leo nilikuwa na mapumziko kidogo. Kesho naendelea na shooting ya Bongoland II.

7 comments:

Anonymous said...

chemi mimi sikufahamu lakaini nakuomba mkonvince brother kibira hapo kabla hajaondoka basi akishirikiana nawewe na wengine wenye uwezo wa kuyaona mapungufu ya wanasinema wa hapa nyumbani mfanye kaworkshop kadogo japo kwa siku moja tuu chagueni eneo moja ambalo wanasinema wetu hapa linawasumbua
ni maoani yangu binafsi
aksante

Anonymous said...

Da chemi samahani naomba kukuuliza unamume wewe au boy frend?

Anonymous said...

Chemi acha hizo internet connection Dar iko bomba tu!sijui unaenda cafe gani wewe!!usisingizie connection hakuna connection hakuna!!!..siku hz hata wireless connection zipo hapo Bongo nenda kaulize ttcl utapata!!.
na usitake kulinganisha bongo na Massachussets!!

Anonymous said...

hi chemi, i hope you are doing fine, sory for your problems with some computers and that sometimes you have to move from computer to computer, well, i want to advice to come and see ours here at New Africa Hotel, at the Business Centre, we have very high speed computer conection, of pentium 4,3.06, 608MB of RAM VERY FAST I TELL YOU, So you are wellcome our price for an hour not bad due to the speed! hope to see you soon,
your mwanablogu!

Anonymous said...

Dada yangu naomba usisahau kupiga picha ya Tangi bovu sokoni nione pana fananaje siku hizi nilikuwa nakaa maeneo hayo . Na yale ma landrover ya kwenda Goba yanayopita pale mbele ya kwenu

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 7:32am, juzi kwenye ile barabara ya kwenda Goba, lorry iliyokuwa umejaza watu wengi mno wakiwemo wanafunzi ilipinduka. Nilikuwa nimeenda kununua chapati na vitumbua za kunywea chai na nikaiona inashindwa kupanda mlima kwa vile ulikuwa umejaa. Watu wengine walishuka kwenye hiyo gari hapo iliposhindwa kupanda. Kumbe huko mbele ilipinduka! DUH! Naikia watu waliumia wengi kweli hasa wanafunzi.

Anonymous said...

NYIE hamumjui Chemi kwa kujifanya mwenyewe.
Bongo ina internet Cafe zenye huduma safi na zenye kila kitu ndani kama alivyosema huyo mwanablogu hapo chini wa New Africa Hotel.
Utasemaje Dar kuna vumbi wakati miaka nenda, rudi vumbi Africa ni kitu cha kawa!
Mengine ni matusi kama vile hajui hali halisi ya Afrika wakati vitu kama hivyo ni kama dini. Nadhani rekebisha kauli yako na siyo kulaumu kishambashamba tu.