Tuesday, July 03, 2007

Wazazi Wangu safarini Boston

Kutoka Kushoto, Mhesimiwa Frederick Sumaye, Dr. Aleck Che-Mponda, mimi na mama yangu. Tulienda kumsalimia Mheshimwa Sumaye, ambaye kwa kweli alikuwa mkarimu sana. Msaidizi wake alitupikia mishikaki mitamu kama nyumbani. Mheshimiwa Sumaye amemaliza masomo yake Harvard University hivi karibuni.


Baba akiagana na Mheshimiwa Sumaye ambaye alikuwa jirani yangu hapa Cambridge, Ma. Ndo siku nilikabidhi kanda za sinema ya Tusamehe na Bongoland.

Baba na Mama wakiwa South Station, Boston Ma. kuelekea New York City ambapo walienda kusalimia ndugu na marafiki.


Dr. Aleck Che-Mponda akicheki sanamu ya mbwa aina ya St. Bernard huko Mohegan Sun.

14 comments:

Anonymous said...

Sumaye ni mtu simple na mkarimu sana. Mimi nampongeza kwa kujiendeleza na kuonyesha mfano kwa watoto/vijana kuwa elimu haina mwisho. Kila la heri Mhe Sumaye!

Anonymous said...

Picha nzuri chemi
hivi dingi (Baba) yako aliachana na siasa?? simsikii kabisa siku hizi. Good for him...

Anonymous said...

Da chemi, asante kwa kutuonyesha picha za wazazi wako, nimefarijika kwa kweli. Bahati mbaya, kwa mapenzi ya Mungu, mie wazazi wangu wote wawili walifariki nikiwa bado mdogo sana. Hivyo sijapata mapenzi ya wazazi wangu. Mungu awazidishie afya njema na Umri tele hadi wawe wikongwe wazazi wetu hao! MUNGU AWABARIKI JAMANI.

Anonymous said...

Kumbe yule mwanasiasa ndo baba yako ila siku hizi simsikiii au alisharudi CCM?

Hivi Chemi, US unasoma au unakula mzigo ingawa naona kwa mwili wako huwezi beba maboksi lakini waweza kuosha vizee hahahahahaha

Cheers ila ingia gym mama mwili mkubwa

Anonymous said...

Da Chemi, nimefurahi kuwaona wazazi "wetu".. maana mzazi wa mwenzio naye wako.

Majirani zetu Chuo though long time. Inakumbusha mitaa ya Mlimani, Sinza Road, Simba road, Darajani , UDASA etc. jamani... hakuna awali iliyo mbovu..

Mlimani kina mwl. Mndolwa, Elia, Mujwahuzi etc Mungu awabariki sana walimu hao kwa kututoa tongotongo.

Anonymous said...

Chemi naona ulikuwa na ugeni mzito. Hongera sana. Wazazi wako wamependeza.

Anonymous said...

Yaani ulimpeleka kucheza kamari...CHEKA!

Unknown said...

Chemi your blessed, your parents (ours too) look strong and they should be nice too. My God bless the family.

Vijana chukueni mfano ndoa zenu siku hizi ni za miezi tu na mnashindana eti harusi iwe ya gharama sana lkn za baba zetu zilikuwa simple, cheap na "hadi kifo kitutenganishe!"

Anonymous said...

Mswali mawili:

(a) Sumaye alikuwa na msaidizi wa kumchomea mishikaki? Mbona alitangaza kuwa alikuwa akijipikia na kujifanyia kila kitu mwenywe bila msaidizi yeyote, na kwamba kila mtu alikuwa akimwita Freddie. Je huyu alikuwa msaidizi wa namna gani ambaye angemwita Freddie?


(b) Baba yako Dr. Che-Mponda yuko wapi siku hizi? Nakumbuka aliondoka UDSM na kuanzaisha chama chake kwa kishindo. Tangu uchaguzi wa 1995 sijamsikia tena katika siasa, je kaamua kurudi kwenye chaki pale UDSM?

Safari njema huko Dar.

Usikose kuniletea konyagi. Mimi nipo Amherst; tutawasiliana.

Anonymous said...

Kumbe huyu mzee yupo, nakumbuka chama chake kilikuwa kinaitwa CCM-B sababu alikuwa hapingani na matakwa ya CCM.

Anonymous said...

Ila Chemi usije ukawa wewe ndo ulikuwa msaidizi wa Sumaye, na mimi Sumaye ninavyomwelewa kwa totoz lazima hukukatize kwenye anga zake. Any way sio mbaya lakini

Anonymous said...

Hivi Baba Che Mponda anafanya kazi gani? Historia yake ni mwanasiasa siyo? Hebu nieleweshe kidogo.
Matt

Chemi Che-Mponda said...

Anonymopus wa 11:57PM, usiwe na wasiwasi. Sumaye alikuwa na msaidizi wa kiume.

Anonymous said...

Ni lini utajibu haya maswali?? Mengine ni so private hata usipojibu wengine hayatuhusu labda uombe e-mail address za waliouliza ili uwajibu. Lakini yote yaliyomuhimu tunaomba majibu