Monday, July 30, 2007

Konyagi Part II

Kaka Michuzi alinipiga picha na chupa ya Konyagi. Nilitoka kuinunua kwenye kiosk pale City Centre. Duh, hizo chupa kubwa za Konyagi mbona zilikuwa adimu safari hii. Niliona chupa ndogo nyingi lakini kubwa mmmhh sikuziona!

Konyagi Juu!

Kwa habari zaidi ya Konyagi, kinywaji kikali cha aina ya pekee bofya hapa:

KONYAGI

9 comments:

KakaTrio said...

DaChemi mie nilizani KaMichuzi ndio alikuwa amekununulia Konyagi kumbe ulijinunulia weye mwenyewe, kha KaMichuzi kumbe bahiri ivo! kwa jinsi alivopozi kwene blog yake kule nilifikiri yeye ndio alikula bili ya shoping yako yote Dar.

Anonymous said...

Da Chemi, hivi mzee wetu Dr. Che Mponda ameachana kabisa na siasa? kama ameacha hivi anajishughulisha na nini sasa hivi? Maana kuna kipindi kama sikosei nilikuwa namsikia sana kwenye siasa za upinzani! Shukrani endapo utanipatia jibu............

Anonymous said...

kuna utata hapa daChemi,eti jina konyagi is a foreign name,sisi tumefanya kuiga,please tumalizie ubishi wetu

Anonymous said...

mmmmmh! aibu zake michuzi alisema amekununulia hicho kinywaji, haaaaa alivyojisifia kuwa amelipa fadhila ngoja nimfate huko huko kwenye blog yake hana aibu kabisa alaaaaa!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 8:36PM, baba alikwisharudi CCM.

Anonymous wa 11:06PM, navyoelewa Konyagi ni swahilinization ya neno la kizungu, Cognac.

Anonymous said...

sasa we dada ma unene yote hayo na konyagi juu, huoni ya kuwa unaelekea kwenye matatizo kabisa. Tafadhali punguza mwili la sivyo mchungaji atakukimbia kabisa maana utakuwa haujiwezi tena. Labda kama we ni mfuasi wa kifo cha mende. Ni ushauri wa bure tu.

Anonymous said...

Konyagi haitokani na cognac, kwani kila kitu lazima kitoke kwa wazungu tuu?
K-unywa
O-ngeza
N-guvu
Y-ako
A-ngalia
G-ongo
I-naua

Konyagi za awali zilikuwa zinatengenezwa kutokana na Gongo "local spirit" baadaye watengenezaji wa konyagi walivyopata utaalamu zaidi wakaanzakulitukana gongo ndiyo waka "coin" hilo neno konyagi.

Anonymous said...

Halafu swala la baba kurudi CCM nalo kama ni kweli basi hii inaonyesha u-vihiyo wa wanasiasa wetu. Jana walikuwa wa-sosyalisti, kesho wanakuwa conservative. wakinyimwa nafasi ya kugombea ubunge wanaazisha chama kingine cha ki-liberal. Wakishinda uchaguzi wanakuwa "wameula" wanakwenda "far-right" wanavuka u-dikteta mpaka wanakuwa "ma-fascists" Wakienguliwa madarakani wanageuka "wakomunisti"

Ili mradi upuuzi tuu.

Anonymous said...

anon hapo juu chukua tano!!

Ila CCM huna budi kuirudia la sivyo familia ingeandamwa kama ya Lamwai hata Da Chemi wangenyanganya passpoti angekuwa anauza gongo manzese saa hizi. Wafanya nchezo nini!