Friday, June 27, 2008

Picha ya Rais Kikwete

Kassim Mpenda akionyesha picha ya zamani (kulia) na ya sasa (kushoto)

Kutoka Ippmedia.com

Picha ya Rais yabadilishwa 2008-06-27

Na Lucy Lyatuu

Serikali imebadilisha picha rasmi ya Rais Jakaya Kikwete kutokana na kubainishwa kuwa kwa kiwango kikubwa inaonyesha dalili za msongo wa mawazo ya kampeni za uchaguzi mkuu 2005.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Kassim Mpenda alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam. Alisema uamuzi wa kubadili picha hiyo umefikiwa kufuatia ushauri wa wataalam kwamba picha ya sasa haifai kuendelea kutumika kwa sababu hizo.

Alisema picha inayotumika hivi sasa ilipigwa baada ya Tume ya Taifa ya uchaguzi kumtangaza Rais Kikwete mshindi wa uchaguzi huo. Aliongeza kuwa makatibu wakuu na maofisa wafawidhi wengine wote wa ofisi za serikali kuu, serikali za mitaa, wakala na asasi nyingine zote za serikali wameshauriwa kuanza kutumia picha mpya ya Rais.

``Kila nakala ya picha hiyo itauzwa sh. 15,000 na zitapatikana mwanzoni mwa Julai katika Idara ya Habari. Wakati huo huo, serikali kupitia wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, imekamilisha uchapishaji wa bango la baraza jipya la mawaziri. Alisema nakala zake haziuzwi zinatolewa bure na ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) kuanzia jana.

SOURCE: Nipashe

1 comment:

Anonymous said...

Hii picjha ya sasa inaonyesha kuwa katika kipinid cha miaka miwili kazeeka. Ile picha ya kwanza mbona siyo mbaya.