Thursday, June 12, 2008

Sinema - The Surrogates

Huyo farasi naye yumo kwenye sinema
Kwa mbali unaweza kuona maiti (mdoli) juu ya vijiti maalum kabla ya kuchomwa. Nilikuwa kwenye basi nilivyopiga hii picha. Crew walikuwa kwenye mapumziko. Haturuhusiwi kupiga picha kwenye seti. Kwa mbali unaweza kuona makaburi feki.

Wadau, samahani kwa ukimya. Nilikuwa Taunton, MA kwenye shooting ya sinema, The Surrogates. Stelingi wake ni Bruce Willis na Ving Rhames. Mimi niliigiza mle kama Dread yaani binadamu wasiopenda Usurrogate. Ilikuwa poa sana, nilimpita Bruce Willia mara kadhaa kama mpita njia. Kumwona kwa karibu ni mrefu, mwembamba. Ving Rhames si mrefu kama nilivyotegemea lakini ni kibonge. Alicheza kama nabii wa Dreads.

Leo tuliangalia maiti inachomwa. Lakini haikuwa maiti ilukwa mdoli. Lakini ukiona utasema ni mtu huyo. Nakuambia kuna wataalamu wa special effects. Mdoli alichomwa kama wahindi wanavyochoma moto maiti. Walikuwa na zimamoto wa Taunton Fire Department pale kuzima baada ya wao kumaliza kuipiga picha. Nakuambia mdoli alitengenezwa kifundi kiasi kwamba walivyosima moto tuliona fuvu na mifupa!

Nadhani The Surrogates itakuwa sinema kubwa ya summer 2009.

4 comments:

Anonymous said...

Nitapenda kuiona hiyo picha/sinema itakapotoka hapo mwakani, pia nakupongeza kwa juhudi zako ktk fani. Endelea na moyo huo wa kijasiri. Nakutakia mafanikio zaidi. Mosonga

Anonymous said...

kwahiyo

Chemi Che-Mponda said...

Mosonga, asante sana kwa comments. Nina picha zaidi za soot, ila computer ilikuwa inagoma kuzi-upload nitajaribu tena baadaye.

Anonymous said...

Chemi, I like you, unatuonyesha nini unafanya ili kujiendeleza. Sio wa tanzania wengine huko, wakiweka picha basi ni kuonyesha GUCCI za kuazima!sisi tunataka watu wanaojituma. Hongera sana dada!!! ipo siku utapata Grammy. Nothing is impossible when you believe. Mama Chriss