Tuesday, June 10, 2008

Nyanya Adimu Marekani!


Sisi wapenzi wa kachumbari tulie tu! Kama unapenda kula nyanya na salad au kwenye hamburger ulie tu!

Kwa sasa haziuzwi supermarket na kwenye restarurant. Kisa eti zingine zina ugonjwa wa Salmonella! Na wataalamu wanasema hii siyo salmonella ya kawaida bali ni salmonella saintpaul!

Ukipata Salmonella unaumwa kwa masaa 12 hadi 72. Tumbo inauma sana na unaharisha na kutapika. Pia uinakuwa na homa. Watoto wadogo, wazee na pia watu wenya magonjwa yanayoathiri kinga ya mwili wanaweza wakafa.

Kwa sasa watu 150 katika majimbo 17 ya Marekani wameumwa. Hakuna aliyekufa.

Ila unaweza kununua zile grape tomatoes yaani zile nyanya ndogo ndogo ambazo zilaliwa nzima nizma.
Tunagojea all clear kwa hamu tuendelee kula nyanya. Zimejaa vitamin C na A!

Someni:



http://www.sfgate.com/cgi-bin/article.cgi?f=/c/a/2008/06/10/BAA51162BT.DTL

No comments: