Thursday, October 01, 2009

JIHADHARI: Wizi wa mtandaoni nao wachukua kasi ya mabadiliko ya teknolojia!

Huu ni ujumbe uliotumwa kwangu (soma hapo chini) nami kwa vile nilivyoona maneno kadhaa ya KiSwahili, nikaazimu nisiufutilie mbali bali niusome pengine utakuwa umetoka kwa mtu ninayemfahamu. Baada ya kusoma mistari miwilitu ya mwanzo, nimejikuta naang'ua kicheko na kushangaa sasa kwa jinsi hawa majangili wa mtandaoni walivyoamua kutumia huduma ya Google ya kutafsiri lugha "Google Translate" na kubadili utapeli wao kutoka lugha kanganya ya Kiingereza hadi iliyovunjikavunjika ya Kiswahili ili waweze kuwaibia Waswahili wengi zaidi. Masikini we, laiti wangejua thidanganyiki!.

Subi, nukta77!

---------- Forwarded message ----------
From:
Date: 2009/10/1
Subject: huu ember kukuza lucky mshindi
To:

Sisi ni radhi kwa taarifa kwamba alishinda una jumla ya kutoka 485,000.00 GBP kutoka Yahoo! MSN (Windows Live) Awards mpango.

PAYMENT wa zawadi na kudai Vinnarna atalipwa kulingana na makazi Center. Tuzo ya Nobel yahoo lazima kutekelezwa no baadaye kuliko 15 siku kuanzia tarehe ya notification Draw. Gharama yoyote alidai kipindi hiki itakuwa waliopotea.

Alisema chini nambari yako ni kitambulisho:
Batch namba: YPA/07-43658
Reference number: 2007234522
PIN: 1206

ushauri wewe kurudi kwetu wasiliana na mtu Shining Rev Dr Robert kulabu kwa madai yake.

Wasiliana akiitwa / madai ya mwakilishi na taarifa zifuatazo.
Jina: Rev Dr Robert kulabu
E-mail: rev.dr.roberthooks@live.com
rev.dr.roberthooks@safat.us
Simu: +447024067872

Sincerely,
Mrs Carol Jones
Tarehe mstari mratibu

7 comments:

Anonymous said...

Hayo matapeli ya Nigeria hayajui Kiswahili.Hapo walichofanya ni kutumia Google Translator kupata hayo maandishi - tumekwisha. Ingawa kwa mjanja ni rahisi kugundua madudu hayo.

Simon Kitururu said...

:-)

Anonymous said...

Na ukijibu wanaweka kwenye Translator.

Anonymous said...

Hi Da Chemi,
i am not sure how to get this message to you, I'm watching ABC's 20/20 and there is a scathing report about albino killings in Tanzania...its unbelievable.

Anonymous said...

hahahaha duh nimecheka sana.Hicho kiswahili ni baaaab kubwa

Anonymous said...

kitu gani kinawafanya mdhanie kuwa hawa ni wa nigeria? Hii ni sawasawa na mzungu akiona maandishi yamechorwa ukutani anasema, black people have done it.

Pazi Kibamanduka said...

Kuna kitu gani hapo cha kuonyesha kwamba hao matapeli ni wa nigeria? Kwanini hamkudhania kwamba wanaweza kuwa waingereza? Kwanini waafrika tunachukiana hivi?
Hivi wa nigeria wanawazidi waingereza kwa utapeli? Waingereza wametutapeli waafrika kwa zaidi ya miaka miaka mia tano sasa, lakini bado tunawaamini waingereza na kuwatuhumu wa nigeria. BAE systems ni mfano mpya kabisa wa utapeli wa waingereza, lakini hakuna mtu yoyote anayewashutumu waingereza kwa utapeli. Kwa sababu wametuletea ustaarabu wa kuvaa suti, kuzungumza lugha ya kistaarabu, na wametuletea yesu mkombozi wa ulimwengu.

(pumbaf)

waafrika tumtambue adui wetu wa ukweli na tuache kuwaonea wa nigeria.