Wednesday, May 23, 2012

Central Line Kigoma

Central Line (Reli ya Kati) inafufuka. Lakini jamani ni mabehwa yale yale ya tangu nasoma Tabora Girls 1980's! Duh! Sikuamini macho yangu nilipoona picha. Nikajiona kama nimeweka begi kwenye rack, na nakaa kwenye kiti kurudi shule! Duh!  Lakini cha muhimu kuliko behewa ya kisasa ni kufika salama. Next time nikienda Bongo nitasafiri na Central Line nijikumbushe enzi za udenti!  Asante Kaka Maggid.

**********************************************

Kutoka Mjengwa Blog

Kaka Maggid ndani ya Behewa.

Kaka Maggid Mjengwa jana kwenye behewa la Central Line Kigoma

Behewa la First Class Central Line ilipoanza kazi 1914.

... Usafri wa treni utakuwa wa uhakika zaidi kuliko ilivyo sasa. Kwamba wengi tutachagua kusafiri kwa treni kwa vile ni nafuu zaidi na salama zaidi. Na ni usafiri rafiki kwa mazingira.


Siku hiyo inakuja kwa vile tunachoshindwa sasa ni kuwepo kwa wachache ' wanaohujumu' kwa makusudi usafiri wetu wa njia ya reli.

Mapato yanayopatikana yanapotea. Kuna abiria wanaosafiri bila nauli zao kuingia kwenye Shirika bali kwenye mifuko ya wanaojiita wajanja. Kuna mizigo pia inayosafirishwa bila mapato yake kuingia kwenye Shirika, bali, kwenye mifuko ya wanaojiita wajanja. Hali hiyo ni kwa reli ya kati na reli ya Uhuru pia, kwa maana ya Tazara.

Na hao wanaojiita wajanja wengine ni viongozi tuliowapa dhamana za kusimamia mashirika yetu ya umma.

Siku hiyo inakuja tutakapokuwa na mfumo utakaohakikisha mwisho wa wanaojiita wajanja.

Hivyo basi, siku hiyo inakuja tutakapoona fahari kusafiri kwa njia ya reli yanayooendeshwa na mashirika yetu ya umma chini ya uongozi wa wazalendo wa nchi hii watakaokuwa tayari hata kutoa fedha za mifukoni mwao kuhakikisha treni zinatembea kwenye reli zetu.

Naam, siku hiyo inakuja....

Na hili ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,
Kigoma.
0788 111 765

1 comment:

emuthree said...

Hivi wadhungu wasingelijenga hiyo reli, wakaleta hayo mabehewa....waka, waka...tungelikuwa wapi, maana sionikitu kipya, kila kitu cha maendeleo,tulikikuta na tunashindwa kukiendeleza,....kazi kweli kweli