Friday, May 04, 2012

Orodha ya Mawaziri na Naibu Maaaziri

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)

Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)

Ndugu George Mkuchika, Mb.,


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)

Ndugu Celina Kombani, Mb.,


2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)

Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)

Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,


3. OFISI YA WAZIRI MKUU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)

Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)

Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,


4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,


Waziri wa Ujenzi

Dr. John P. Magufuli, Mb.,


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,


Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Dr. David M. David, Mb.,


Waziri wa Kazi na Ajira

Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,


Waziri wa Maji

Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,


Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum

Prof. Mark Mwandosya, Mb.,


Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Eng. Christopher Chiza, Mb.,


Waziri wa Uchukuzi

Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,


Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara

Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha

Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini

Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,



5. NAIBU MAWAZIRI


OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI



6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais

Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,


7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,


8. WIZARA MBALIMBALI


Naibu Waziri wa Kazi na Ajira

Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,


Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

Ndugu Adam Malima, Mb.,


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,


Naibu Waziri wa Ujenzi

Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,

Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi

Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji

Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini

Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha

Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012

7 comments:

Anonymous said...

Rais Kikwete akitangaza baraza alilolisuka upya amesema au kudokeza kuwa Tanzania sasa inayo mafuta.

Ingawa watu wengi tumevutiwa na uteuzi wa mawaziri na kusahau taarifa hizi rasmi, kuna umuhimu taarifa zaidi tuzipate kuhusu mafanikio haya ambayo yanaweza kuleta matumaini ya uchumi mzuri kwa taifa kama sio balaa (oil curse).

Uvumbuzi huu utapelekea wizara ya Madini na nishati kugawanywa na kuwa wizara mbili kwenye bajeti ijayo.

Anonymous said...

Kuna sura mpya ambazo hazikuwahi kuonekana hapo kabla.

Kuna watu ambao mchango wao kwa taifa na kwa ulimwengu huu unaheshimika jambo linalonifanya binafsi niamini kuwa hata kwa nafasi walizopewa watafanya mambo mapya mazuri kwa watz.

Anonymous said...

Mawaziri Wapya ni Mwakyembe - Uchukuzi, Abdalah Kigoda - Viwanda na Biashara, Mgimwa - Fedha, Kagasheki - Maliasili; Dkt. Fenela - Habari; Chiza - Kilimo,
Manaibu niliowapata wapya ni Saada Mkuya - Fedha; Simbachawene - Nishati; Makamba - Sayansi&Teknolojia; Benelith Mahenge - Maji&Uvivu; Masele - Madini; Angela Kairuki - Katiba; Janeth Mbene - Fedha; Makala - Habari; na Dkt Seif Rashid - Afya

Anonymous said...

Kama JK amewaondoa ina maana tuhuma zao zilikuwa ni za ukweli. Sasa kama wameiba wanatakiwa warusishe na wakiri kwa watanzania wote kwamba walituibiwa. Kuachwa tu ina maana hata hao waliongia wanaweza kula alafu wakaachwa lakini wameshajinufaisha bwana. So tukiwaka utamaduni wa kuwajibishana inakuwa powa zaidi ili mtu ajue kuwa hata akifukuzwa bado atawajibishwa pia.

Hii ni nzuri jamaa waligoma kujiuzuru wakitegemea huruma ya Kaka Mkuu lakini kawatosa, Kinachofuata ni kwamba hawa jamaa wafikishwe Mahakamani na mikataba walioingia pale penye maslahi yao pabomolewe.

Sefu Saidi said...

Wamezdi!!!
1. BARAZA NI KUBWA MNO- ( toka 50 hadi 55) hapa tunaongea kuongezeka kwa magari mapya matano, mishahara ya mawaziri wapya watano, posho kwa watu wapya watano, bila shaka watapewa na wasaidizi nyumba na umeme wa bure na wataongeza kiasi cha pesa ya serikali inayopotea

2. SURA ZILEZILE - baadhi ya matu waliorudishwa ni wale waliokuwepo wakavurundaau wengine wamerudi kwenye utamaduni wa zamani haribu hapa utapewa sehemu nyingine. Sitegemei Maghembe, Kombani, Malima walete mabadiliko wanajaza nafasi tu

3. KUTOKUZINGATIA SHERIA - Tunategemea kama kawaida kutakuwa na semina elekezi nyingi, Mimi nashangaa ni Magufuli peke yake anayesoma sheria na

kuzisimamia wengine wanakuwa na visingizio kibao. Kwa ufanisi anaokuwa nao Magufuri kila nakoenda inaonesha wizara zote zina utaratibu mzuri wa kuleta tija ila wanaoteuliwa kuzisimamia wanaenda kuuza sura tu.

Nategemea haya mambo matatu yameleta dosari kubwa katika baraza zima la mawaziri ukizingatia kuwa Kaka Mkuu alisema kuongeza mshahara kwa wafanyakazi kunategemea sana makusanyo wakati kuna watu wanachukua makusanyo yote kupeleka nyumbani kwao bila hata kuchangia kujenga barabara ya mtaa itaka kuwakomoa majirani.

Naamini hili baraza litavunjwa tena kabla ya mwisho wa mwak huu.

Anonymous said...

Huu ni upuuzi nakubaliana na Mdau aliyesema Baraza ni kubwa na mimi nasema ni Mzigo kwa Walipa Kodi.Huu mfumo umepitwa na wakati Wizara nyingine hazina maana,mfano Utawala Bora,toka wizara hii ianzishwe nchi imeingia mikataba mibovu kibao,ufisadi na wizi.Hii kutokana na KATIBA MBOVU iliyopitwa na WAKATI ambayo haina MANUFAA kwa WANANCHI.Karne hii ya 21 hatuhitaji BARAZA la mawaziri,manaibu,makatibu wakuu wote hawa,pesa zote za kodi zinaishia kwenye matumizi.

Anonymous said...

Nakubaliana na Sefu Saidi Watawala wetu nivichekesho baraza toka 50 hadi 55 nisawa na mtu anayebeba mzigo wa kuni mzito anaposhindwa anautua chini badala ya kuupunguza anaongeza kuni zaidi nakujaribu kuubeba tena.Watawala acheni kuiga ya utawala wa nchi kubwa nchi kubwa ni sawa na bara lote la Africa wakati nchi yenu nisawa na Majimbo tuu.Waswahili wanasema JIKUNE unapofikia.