Friday, June 29, 2012

Ogopa Magari enye Madirisha Tinted!

Nimepata kwa email, lakini hii kali!  Mambo ya ushirikina yataisha lini!!!!


*************************************************************

Dear Friends:

Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita. Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya biafra.

Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja. Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu. Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, ma baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na taarifa zake.

Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata.

Wakati huo huo ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku.

Kilichokuwa kinatia wasiwasi zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho.

Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango, alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana, ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya mwananyamala. Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana, pale kituoni walikuwa abiria wawili
yaani yeye na mama mmoja. Baada ya dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver. Gari hiyo hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu
moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi pia ana miaka 32.

Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu.

Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize kazi. Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga.

Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na walikuwa wamevaa gloves.

Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu kingine. Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa lazma ziwe za mtu wa miaka 40 na kuendelea.

Mwenzao mmoja akasema cashier alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila waliendelea kumkung'uta kwa hasira. Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya sayansi.

Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote, siku iliyofuata alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea vizurr. Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia
abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata vyeo na utajiri wa haraka.

1 comment:

Anonymous said...

story hii ya uongo. lengo ni kuzuga watu ili ionekane Dr. Ulimboka alitekwa na watekaji na namna hii.

Mbona hakuna jina la aliyetekwa wala ofisi yake.

Mbona watekaji walikuwa wanapigia simu jamaa zake huyu anayedai kutekwa?

Kama Lengo ilikuwa ni ushirikina iweje waanze "kumpiga na kumrusha kichura?"

Iweje wamrudishe kutoka kibaha mpaka sayansi?

Kwa nini wahangaikie kiasi hicho kwa mtu waliyekuwa wanataka kumuua.

Story hii haijatulia.

Kwa nini vyombo vya habari hapa hazijainasa hii habari?