Swali uliulizwa:
Hawa najiuliza, kwanini mabibi harusi wengi wanapenda kulia siku ya ndoa?
1. Jee! Ni uchungu au furaha kwa kupata mume?
2. Ni uchungu au kufaraha ya kuondoka mazingira ya nyumbani kwao?
3. Ni furaha ya kwenda kuanza kumiliki kitanda na mumewe mfululizo na
kwa muda anao upenda (lile tendo)?
3. Au wanaogopa fedheha kwa kuwa wanaolewa /anaolewa akiwa si bikra?
4. Ni uoga wa kuanza kulala bila nguo ya ndani akiwa kwenye ndoa na mumewe?
Kwa nini mabibi harusi wengi huangua vilio?!
Dada Leila Sheikh kajibu hivi:
Kwetu sisi uswahilini usipolia wafinywa na kungwi.
Seriously huwa tunalia kwa sababu tunaondoka kwa wazazi wetu na kwenda kujiunga na koo jingine.
huwa
tunafundwa- "Mama Mkwe ndiyo Mama Yako sasa. Ba Mkwe ndiyo Baba Yako
kuanzia leo. Hawa usiwachukulie kama mawifi au mashemeji bali ndiyo
ndugu zako kuanzia leo. Mume akiwa kachacha, gongesha vikombe majirani
wafikiri munakunywa chai kwa bajia. Chakula kikikosekana, hakikisha
unachoma iliki ili majirani waamini unapika pilau. Mume akichelewa
kurudi, mlaki mlangoni kwa tabasamu. Akikukaripia, mwimbie wimbo wa
mapenzi "Sabalkheir (ishakuwa asubuhi anaporudi) Mpenzi, waonaje hali
yako?".
Na kwa nini nisilie baada ya kuambiwa hivyo?Unaondoka kwenu ulipodeka wenda ugenini.
Leila Sheikh
4 comments:
Kuna mtu kasema mtoto akizaliwa analia kwanini...kwasababu anatoka sehemu aliyoizoea na kwenda sehemu ngeni, halikadhalika ni kwa mke, anatoka sehemu ya wazazi wake anakwenda kwa mume....ni hisia asilia, hazikwepeki, na ndio maana wengine wanafikia kulazimishwa kulia, ili kuazimisha hiyo hisia,...ni wazo langu
Wanaogopa mpambaja tuu.
Wanawake wengi hulia siku wanapoolewa simply because they think they are stepping into the known. Hata mimi nakumbuka mke wangu alilia sana tulipooana 1997. Kila ndugu zake walipombembeleza ndio alizidi kulia. Jambo zuri ni kwamba hizo huwa ni hisia za muda mfupi.
Nikweli hata mimi nililia sana kilichoniliza nikwamba nilihisi mamy wangu angepata tabu kuwa nae mbali nikifikiria jinsi alivonizoea hakuwahi kuwaza kuwa mbali na mm na hata kipindi nasoma nikichelewa kurudi alikua akinitafuta na kunambia nisichelewe ananikumbuka sana hicho ndicho kiliniliza tena sana nilijua atapata tabu bila kuniona kupenzi chake
Post a Comment