Sunday, May 05, 2013

Mlipuko wa Bomu Katika Kanisa Katoliki Arusha


 HABARI KWA KIFUPI:Mkuu wa Mkoa Mulongo nae yumo kwenye hili sakata. RPC Anatoa hotuba.
Anasema ni tukio la kighaidi.

Anasema alihusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu.

Anasema wanawasaka waliohusika. Anomba mwenye taarifa yo yote aisaide polisi.

Waliojeruhiwa ni 30 majeraha ya kawaida, na 3 wamejeruhiwa sana.

Mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano



Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Tanzania Field Force Unit (FFU) on site of Catholic church bombing
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahim Kilongo.


JESHI la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia mtu mmoja ambaye anahusishwa na kutokea kwa mlipuko uliotokea katika kanisa la Katoliki la St Joseph Olasiti Arusha leo asubuhi.

Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Papa kutoka Vatican akizindua Parokia hiyo mpya ya St Joseph Olasiti ya Jijini Arusha.
Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMRQWe-3DwwaUndhYh1ip8NOsy0SUDnS9ZaDT4mkleioWUxd9pwcn58XwJEoIty_6JpgECCFiBJrCcsQ3dQoNHKMVOYKG_Ov_IeEUNXNFszp3wwIvmBnDmaMwcziTz4a6MJJKIWA/s1600/IMG_20130505_130432_0.jpg
Waumini pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki wasiamini nini kilichotokea kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea asubuhi ya leo.






6 comments:

Anonymous said...

Kwa sasa hali ya kawaida inaanza kurudi. Vyombo vya usalama vinaendelea kuchunguza ili kujua mlipuko huo ni nini hasa. Balozi wa papa nchini na viongozi wa juu wa jimbo wameondoka eneo la tukio salama na balozi hajadhurika kabisa ingawa mlipuko huo ulilipuka karibu nao.

Mkuu wa mkoa alikuja na sasa ameondoka. Wananchi wameanza kupungua eneo la tukio na wengi wanaelekea Mount Meru ili kuwatambua majeruhi. Hivyo idadi ya watu wanaondoka eneo la tukio na kwenda hospitali. Polisi wamekamata pikipiki ambayo inasadikiwa imetumika katika tukio hilo.
Shughuli ya uzinduzi wa kanisa hilo imeahirishwa hadi tarehe ambayo haijatajwa Mungu awajalie majeruhi wapate nafuu haraka.

Anonymous said...

Mlipuko ulipotokea Boston tukatoa maoni upesi kuwa ni wale wale wanaofanyaga milipuko ndio wamelipua. Watu wakabisha.

Sasa na hapa ngoja tusiseme nani kalipua, lakini mwisho wa siku itaonekana ni wale wale wasiku zote. Sasa wasipokosolewa watabadilikaje?

Anonymous said...

Duh! Sasa mbona hatusikii tena habri za kintelejensia kama tulivyokuwa
tunasikia Chadema wakitaka kufanya maandano? Au hizo habari huwa
zinahusu Chadema tu? It's as if we are lost!

Anonymous said...

Sio tetesi ni tukio halisi vyombo vya nje imiwemo BBC, wametangulia kuripoti kuwa Kuna mtu mmoja kafa na majeruhi 50! Mwakilishi wa Papa nchini alikuwa akiongoza misa! Wenye zaidi watujuze! Hali sass ni tete!

Anonymous said...

Serikali ya Tanzania inaonekana kuwapuuza hawa wahalifu, inawajua na kuwaona wakitembeza CD na kufanya mikutano au hadhara zenye uchochezi tena kwa kibali halali, eti kwa kuhofia kupewa kura.......jamani Tanzania inaanza kuzama kama mnavyoona ya Zanzibar na Arusha.

Serikali ituambie kama uwezo wa kutulinda hautoshi ili tuanze kujilinda wenyewe. Mimi kama mlipa kodi.....nimechoka na ngonjera za serikali ambayo kila kukicha inakuwa inaonesha mianya ya udhaifu kede kede.

Anonymous said...

Ithink hiyo ni infiltration some people from out side the country wanajaribu kuiweka nchi katika hali tete for their future plan. ikuumbukwe tupo na hali ya utata na nchi ya malawi, pia tunapeleka majeshi Congo DRC kuwang'oa M23,who allied with them? matukio haya na yale ya kulipuliwa kwa maghala ya kijeshi mbagala na gongo la mboto pamoja na kualibika kwa Rada ni ishara mbaya kwa usalama wa nchi.