Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Shughuli za
Bunge, Bwana Anselm Lyatonga Mrema amefariki Dunia.
Habari
kutoka Dodoma zinasema kuwa Mrema amefariki usiku wa tarehe 10 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma
alikokuwa amepelekwa kwa matibabu akisumbuliwa na shinikizo la damu
Aidha
kufuatia msiba huo mkubwa uliolikuba Bunge Rais Jakaya Kikwete amemtumia Spika
wa Bunge, Anne Makinda salamu za rambirambi akionesha kusikitishwa sana na
msiba huo.
Katika
salamu zake kwa Spika, Rais Kikwete amemwelezea marehemu kuwa alikuwa ni
mtumishi Mwaminifu, Mwadilifu na mchapakazi hodari aliyejituma kikamilifu
katika utekelezaji wa majukumu yake.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa
taarifa za kifo cha Mtumishi wa Ofisi yako ya Bunge, Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Shughuli za Bunge, Bwana Anselm Lyatonga Mrema kilichotokea usiku wa
tarehe 10 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amepelekwa
kwa matibabu akisumbuliwa na shinikizo la damu”, amesema kwa masikitiko Rais
Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
“Nilimfahamu Marehemu Anselm Lyatonga Mrema,
enzi za uhai wake, kama Mtumishi Mwaminifu, Mwadilifu na Mchapakazi Hodari
aliyejituma kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yake, sifa ambazo
zilimfanya apande cheo kutoka kuwa Katibu Msaidizi Mwandamizi wa Bunge na kuwa
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Shughuli za Bunge”, alisema Rais Kikwete.
Anselm Lyatonga Mrema ni mdogo wa Mbunge wa Vunjo mkoani Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment