Thursday, December 31, 2015

Heri ya Mwaka Mpya!

Nawatakia wadau wote Heri ya Mwaka Mpya!

Mkesha wa Mwaka Mpya DMV

 Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini akihesabu sekunde zilizoslia kuelekea mwaka mpya kwenye sherehe ya mkesha wa mwaka mpya 2016 iliyofanyika Lanham, Maryland siku ya Alhamisi Desemba 31, 2015 iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania DMV na kuwakutanisha wana DMV na familia zao wakiwemo marafiki kutoka majimbo mengine huku wengine wakiokea Tanzania. PICHA NA KILIMANJARO STUDIO
Wafuangaji champagne wakiwa tayari kama kikosi cha mizinga wakisubilia sekunde zilizobaki kuingia mwaka 2016 kuachia mizinga yao ikiwa ni sehemu yakusherehekea mwaka mpya wa 2016.
 Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini akifuahia kuuona mwaka mpaya, wapili toka kulia ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly pamoja na Asha Hariz (kulia) wakifurahia kuuona mwaka 2016.
WanaDMV wakikumbatiana kama familia moja na kupongezana "tumeuona mwaka 2016"
 Wanafamilia wakipongezana.
 Ni furaha ya mwaka mpya
Wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja kusherehekea kuuona mwaka,

Ni 2016 hiyo ni furaha kwa kwenda mbele.
Kwa picha zaidi bofya HAPA

Saturday, December 26, 2015

Mzee Njemba Atoweka Nyumbani kwake Magomeni, Ndugu Zake Wanamtafuta

Ndugu na jamaa wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani)  ametoweka nyumbani kwake Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya Alhamisi tarehe 24/12/2015. 
Alionekana mara ya mwisho kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
Wanafamilia wanaomba mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf  anayepatikana katika namba 0784 606 262.
Wanatanguliza Shukurani za dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.


Friday, December 25, 2015

Krimasi Njema!

Nawatakia wadau wote Krismasi Njema!

Saturday, December 19, 2015

Afrika Haikuwa Maskini


Two Congolese Warlords Jailed


Germain Katanga



Thomas Lubanga



ICC Sends 2 Convicted Warlords to Congo Prison

   THE HAGUE, Netherlands (AP) - The International Criminal Court has sent two militia leaders convicted of committing war crimes in the Democratic Republic of Congo to that country to serve the remainder of their prison sentences.

   The court announced that Thomas Lubanga and Germain Katanga were transferred to a Congolese prison on Saturday.

   Lubanga was sentenced in 2012 to 14 years for using child soldiers in his militia during fighting in the mineral-rich eastern region of Ituri. Katanga was sentenced in 2014 to 12 years for crimes including being an accessory to murder.

  Katanga's punishment was reduced by appeals judges and he is due to complete his sentence Jan. 18.

  

Friday, December 18, 2015

Walioghushi Vvyeti ili Kupata Kazi Serikalini, Kiama Chao Hiki Hapa!



PICHANI JUU: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) ameiagiza Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI kuwachukulia hatua watumishi waliobainika kutumia vyeti visivyo vyao kupata ajira Serikalini.

Mhe. Kairuki aliyasema hayo jana alipotembelea Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu–UTUMISHI ikiwa ni muendelezo wa ratiba yake ya kutembelea Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

“Watumishi wote waliobainika kupitia Mfumo Shirikishi wa Malipo ya Mishahara ya Watumishi wa Umma (Payroll) kutumia vyeti visivyo halali kwao wachukuliwe hatua stahiki” Mhe. Kairuki amesema.

Aidha, Mhe. Kairuki amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Emmanuel Mlay kutafuta Ufumbuzi wa kumalizana na tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya kughushi.

“Muwasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao” Mhe. Waziri alisisitiza.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Leonard Mchau alisema kuwa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma imehakiki jumla ya watumishi 704 ambao kati ya hao watumishi 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani wamegundulika kuwa waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.

Bw. Mchau aliongeza kuwa baadhi ya watumishi hao walioonekana kughushi vyeti ili kujipatia ajira Serikalini wamekimbia vituo vyao vya kazi.

Bw. Mchau aliwaasa wananchi kuepuka mchezo wa kughushi vyeti ili kujipatia ajira Serikalini.

“Ni kosa la jinai kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia kazi hivyo endapo utagundulika umeghushi vyeti utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.”  Bw. Mchau alifafanua.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inaendelea na zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wote wa Umma nchini na matarajio ni kuwahakiki watumishi wote.


***************************************************
 KUTOKA HABARI LEO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, ameiagiza Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu (Utumishi) kuwachukulia hatua watumishi waliobainika kutumia vyeti visivyo vyao, kupata ajira serikalini.

Kairuki amesema hayo jana alipotembelea idara hiyo katika muendelezo wa ratiba yake ya kutembelea Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
“Watumishi wote waliobainika kupitia Mfumo Shirikishi wa Malipo ya Mishahara ya Watumishi wa Umma (Payroll), kwamba wametumia vyeti visivyo halali wachukuliwe hatua stahiki,” amesema Kairuki.

Amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu Utumishi, Emmanuel Mlay kutafuta ufumbuzi wa kumaliza tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya kughushi.

“Muwasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao,” alisisitiza.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa RasilimaliwatuUtumishi, Leonard Mchau, alisema kuwa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imehakiki watumishi 704 na kati ya hao, watumishi 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani, waligundulika waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.

Hata hivyo, Mchau aliongeza kuwa baadhi ya watumishi hao waliobainika kughushi vyeti ili kujipatia ajira serikalini, wamekimbia vituo vyao vya kazi. Mchau aliwaasa wananchi kuepuka mchezo wa kughushi vyeti, ili kujipatia ajira Serikalini.

“Ni kosa la jinai kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia kazi, sasa endapo utagundulika umeghushi vyeti, utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,” alifafanua Mchau. Kwa sasa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inaendelea na uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma nchini mpaka kila mmoja atakapohakikiwa.

Thursday, December 17, 2015

Term Limits Lifted for Rwanda

By IGNATIUS SSUUNA
Associated Press

   KIGALI, Rwanda (AP) - The head of Rwanda's electoral commission said late Friday partial results show Rwandans have voted to lift term limits in order to allow President Paul Kagame extend his rule.

   More than 98 percent from 21 out of 30 districts, representing 70 percent of registered voters, voted to lift term limits for Kagame, Mbanda Kalisa said. Kagame's supporters celebrated the announcement in the capital, Kigali.

   Kagame, 58, is ineligible to run in 2017 because the Rwandan constitution limits a president to two terms. But if Rwandans approve the referendum, Kagame would be able to run for an additional seven-year term and then two-five year terms, which means he could possibly stay in power until 2034.

Rwanda President Honourable Paul Kagame

 Kagame became president in 2000 after being Rwanda's de facto leader since the end of the country's genocide in 1994. He is credited with stabilizing the country and promoting economic growth after the mass killings, but critics say he is an authoritarian ruler who does not tolerate opposition and he is accused of human rights abuses.

   Rwanda's political opposition criticizes the referendum as undemocratic and the U.S., a key Rwandan ally, has opposed Kagame's bid to stay in power.

   The Chairman of the National Electoral Commission Mbanda Kalisa said partial results will be released later Friday.

   Many of the 6.4 million registered voters are expected to participate in the referendum.

   Kagame voted at Rugunga polling station in the capital, Kigali, accompanied by his wife and daughter.

   "What is happening is people's choice. Ask people why they want it," he said maintaining that it's the wish of the Rwandan people that he extends his term. He said he would announce his candidature "any time."

   Ninety-two per cent of Rwandans want President Paul Kagame for third term, according to a survey conducted by Ipsos, a global research firm, that was released this week.

   "President Kagame is a hero and statesman like former Tanzania President Julius Nyerere," says Dan Gatera, a voter in Nyamata, east of the country. "The constitution should not be used to limit presidents who have talents."

   Western diplomats voiced concerns about the vote. The European Union is worried that the opposition was not given adequate time to campaign against the referendum, said Michael Ryan, head of the EU delegation to Rwanda.

   "There should have been adequate time for debates, and educating people about the changes made in the constitution," Ryan told journalists.

   The Democratic Green Party of Rwanda is the only opposition party which rallied Rwandans to vote against changing the constitution to extend presidential term limits.

   Erica Barks-Ruggles, the U.S. Ambassador to Rwanda, said she is concerned because the referendum was organized very quickly.

   The move to change Rwanda's constitution was prompted by a petition signed by more than 3.7 million people. The petition was endorsed by the Senate and the lower house of Parliament last month and later by the country's Supreme Court.

   If Rwanda's term limits are changed and Kagame runs again, he will join a growing list of leaders in East and Central Africa whose governments have prolonged their rule by changing the limits on presidential terms.

   In 2005, Ugandan lawmakers changed that country's constitution, allowing President Yoweri Museveni to seek re-election in 2006 and 2011. He is running again in 2016.

   Neighboring Burundi has political unrest that started earlier this year when President Pierre Nkurunziza run and won a third term that many oppose saying it goes against the two five-year term limit imposed by the constitution.

   There have also been protests in Congo over efforts by President Joseph Kabila, who has been in power for 15 years, to prolong his time in office.

  

Wednesday, December 16, 2015

Nunua Tiketi ya Ndege Kwa Njia ya Installments Kupitia Tuzola



Tuzola ni kampuni ya waTanzania wanaoishi Marekani.  Kama huna hela  kamili ya kununua tiketi ya ndege unaweza kununua kwa kulipa kiasi awali, na baadaye ulipe hela iliyobaki (installments).  Kama unakaa Marekani unaelewa vizuri mambo ya kulipa bili kwa installment.

Saturday, December 12, 2015

Namba za Simu za Kuripoti Wanaofuja Hela za Serikali!



Maana ya MAGUFULIFY!


Uvaaji wa Chupi - Afya ya Uzazi



Na Mdau Joyce Masika

Leo naomba nikukumbushe somo la Afya ya uzazi. Somo hili litafafanua faida na hasara au madhara yatokanayo na uvaaji wa nguo za ndani hasa Chupi.
Uvaaji wa chupi kihistoria ulianza karne ya 19 baada ya uvumbuzi wa viwanda na mapinduzi yake yaliyoambatana na mapinduzi ya teknolojia.
Enzi za mama zetu na babu zetu uvaaji wa chupi haukuwepo hapa Tanzania. Uvaaji wa chupi uliletwa na wamisionari na wakoloni wakati wanaleta dini Africa. Kabla ya hapo waafrica hatukuwa na utamaduni wa KUVAA chupi.
Mtoto akizaliwa hakuvalishwa chupi kamwe kama ilivyo Leo.
Mwanamke pia enzi hizo alikuwa havai chupi. Mwanaume naye pia alikuwa havai chupi? Watu wote walikuwa hawavai chupi. Mwanamke alikuwa hachuchumai chini pindi akijisaidia kutokana na kwamba hawakuwa wanavaa chupi hivyo wakitaka kujisaidia haja ndogo walikuwa wanasimama tu na kupanua miguu na kuanza kukojoa.
Nyakati za leo ambapo uvaaji chupi kwa wanaume na wanawake uko juu sana kuanzia watu tunapokuwa watoto wadogo hali ya Afya ya viungo vya uzazi imeendelea kuwa mbaya sana. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya kuvaa chupi :

1. Magonjwa ya "Urinary tract infection" au UTI hayataisha kwako.

Hii hasa ni kwa wanawake wanavaa nguo nyingi kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu zaidi ya saa kumi. Unavaa chupi, lakini tight, suruali ya jinzi, nk halafu unashinda na hizo nguo kuanzia asubuhi unapoenda kazini hadi saa mbili usiku unaporudi home. Hiyo ni hatari sana.
Mwanamke anayefanya kazi zinazompasa kuwepo kazini zaidi ya masaa 8 namshauri asiwe anavaa chupi kabisa. Chupi ivaliwe nyakati za hedhi tu. Kama hauko kwenye siku zako vaa suruali tu bila chupi. Au vaa underskirt pekee yake kwa ndani na ndoo uvae nguo yako ya kawaida. Hii itakuepusha na kuugua UTI. Ukiacha sababu za ngono UTI husababishwa na bacteria wanaopendelea mahali penye unyevu na joto. Kwa hiyo mwanamke akivaa nguo nyingi bacteria hao hujipatia joto la kutosha kuzaana.
Mwanamke ni vyema ukaepuka kuvaa nguo za kubana mwili sana ili kuepukana na uwezekano wa kupafanya ukeni pawe na joto sana na ikitokea bacteria mmoja tu akaingia humo atazaa haraka sana na kujikuta UTI inakuwa rafiki yako. Vaa sketi bila chupi au kama kuvaa suruali ni lazima hakikisha unavaa suruali peke yake. Jizoeze tu utazoea. Na ukizoea kuvaa nguo bila chupi utainjoi sana.

2. Magonjwa ya kuvu au fungus hayatakoma kwako.


Bado niko kwa wanawake, kama nilivyoeleza mwanzo hapo magonjwa ya fungus yanasababishwa pia na kuvaa chupi kwa muda mrefu. Chupi inayovaliwa kwa zaidi ya saa 8 lazima italeta ukungu au uvundo sehemu nyeti. Huo uvundo waweza kuleta fungus ukeni. Fungus za ukeni hazina tofauti na zile za miguuni kwa wanaume wanaovaa viatu kwa muda mrefu bila usafi miguuni wa kutosha.
Chupi inakuwa kama socks za wanaume. Mwanamke avaae chupi muda mrefu bila kuruhusu upepo upite ndani ni watapata fungus ukeni sawa na mwanaume anayevaa socksi zisizofaa kiafya. Chupi au socks zinazofaa ni zile za pamba au cotton.

Of course sababu za kupata ugonjwa wa fungus kwa mwanamke siyo tu kuvaa chupi inayobanaaaa kwa muda mrefu ni pamoja na kutawadha kwa kutumia maji ambapo maji hayo huacha unyevu ambao hutengeneza uvundo unaopelekea fungus ukeni.
Wanawake wengi hawajui kutawadha kwa kutumia maji. Wengi wamalizapo kujitawadha haja kubwa ndipo hurudi kujisafisha ukeni. Hii ni hatari sana kwani bacteria watokanao na kinyesi unawahamisha kutoka nyuma na kuwaleta mbele.
Mwanamke unapaswa kutawadha kwanza mbele kisha umalizie nyuma. 🐓🐕
Yaani hakikisha kuwa uchafu wa nyuma unaoweza kuwa umebakia kwenye vidole vyako usiuingize ukeni kwa namna yoyote ukijarib kuchunguza wanawake wengi hufuga kucha tena mkono wa kushoto iwje akitawadha uchafu usibaki kwenye kucha? tena kwa usahaulifu anajifashia mkono huo huo wenye kucha ndefu ambazo tayari zipo contaminated?. Tawadha pande zote lakini uhakikishe kuwa haviingiliani mbele na nyuma. Sawa dada yangu?? Uko poa hapo??
Kikubwa hapa ni usafi wa mbele na nyuma. Usafi wa chupi zetu. Uvaaji chupi wetu.
Kwa mfano uwapo safarini tena safari ndefu ya zaidi ya saa 8 ni vyema ukasafiri bila kuvaa chupi isipokuwa tu kama uko kwenye siku zile za adabu. Hata kama uko kwenye siku za adabu ni vyema ukasafiri bila kuvaa manguo mengi sana yanayobana mwili. Vaa chupi na sketi au suruali isiyoubana sana mwili wako.



3. Chupi husababisha ugumba kwa wanaume.

Sababu nyingi za ugumba tunaweza ukizipata kutoka kwa madaktari wetu wa hospitali zetu. Lakini kwangu mimi sababu nyingine ya ugumba wa wanaume kuwa ni kuvaa chupi zinazobana sana.
Mwanaume wengi siku hizi hawavai chupi. Anavaa kaptura au boxa badala ya chupi. Tena havai kaptura inayobana sana. Anavaa isiyobana viungo muhimu kwa uzalishaji wa watoto. Mbegu za kiume huzalishwa kwa wingi wakati wa baridi. Kuvaa chupi inayobana kwa muda mrefu husababisha korodani kuchemka sana na kushindwa kuzalisha mbegu nyingi. Mwanaume mwenye mbegu chache hushindwa kutungisha mimba kwani mbegu zake zinakwenda ukeni huku zikiwa dhaifu na kushindwa kuogelea ukeni.


4. Chupi husababisha miwasho sana kwenye mapaja ya mwanaume na mwanamke.

Epuka kuvaa chupi zinazobana ili kuepukana na miwasho.

Sunday, December 06, 2015

Kesi ya Rufaa ya Talaka ya Thadei Mtembei Imeahirishwa

wooden gavel and books on wooden table,on brown background

Na Mwandishi wetu

KESI ya rufaa ya madai ya talaka dhidi ya mfanyabiashara na Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya St Mathew, Thadei Mtembei imeahirishwa baada ya wakili wa Mtembei, Mussa Kyoboya kudai mrufaniwa yuko India kwa matibabu.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Tarimo.

Katika kesi hiyo, mpeleka rufaa, Magreth Mwangu anawakilishwa na wakili Chacha Mrungu. Kesi hiyo ilikuja mahakamani juzi ambapo mrufaniwa alitakiwa kupeleka majibu ya rufaa.

Hata hivyo, wakili wake alisema majibu hayako tayari kwani kuna vipengele ambavyo alitakiwa kusaini, lakini ilishindikana kutokana na kuwa nchini India kwa matibabu. Kesi hiyo imepangwa kuendelea Desemba 16 mwaka huu.

Awali, kesi hiyo ilisikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo Kizuiani mbele ya hakimu Rajab Tamaambele, ambapo Mwangu na watoto wake walionekana hawana haki, kwa madai sio mke halali na watoto hao ni wa zinaa kutokana na kuzaliwa nje ya ndoa.

Katika madai ya msingi, Mwangu anataka talaka, mgawanyo wa mali na matunzo ya watoto.

Katika sababu za rufaa, mrufani alieleza kusikitishwa na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo Kizuiani Septemba Mosi mwaka huu, kwa hakimu kukosea kisheria kwa kutosaini nakala ya hukumu ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa saini za wazee wa baraza.

Sababu nyingine ni Mahakama kukosea kisheria kwa kunyang’anya haki ya watoto kwa kutotoa matunzo ya watoto kwa mama, ambaye anaishi na mrufaniwa kwa miaka 20 na kuvunja Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009. Maamuzi ya Mahakama ya Kizuiani yalishindwa kufuata sheria kwa wazee wa baraza kushindwa kutoa maoni yao.

Balozi Wilson Masilingi Aanza Ziara ya Kutembelea Vyama Vya Siasa DMV

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi leo Jumamosi Desemba 5, 2015 alihudhuria mkutano wa Halmashauri ya CCM tawi la DMV ikiwa ni moja ya ziara zake anazotarajiwa kuzifanya kutembelea matawi ya vyama vya siasa nchiMarekani yenye lengo la kudumisha mshikamano na ushirikiano wa Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.

Akiongea kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV Mhe. Wilson Masilingi amesema lengo kuu ni kuwa karibu na vyama vya siasa kwa lengo la kuleta umoja na mshikamano ndani ya Jumuiya za Watanzania nchini Marekani na pia kuvitambua kama sehemu na sura ya Diaspora na kutoa wito kwa Watanzania waishio Marekani kuelekeza nguvu katika kuwekeza nyumbani bila kujali ufuasi wa chama unachoamini au kushabikia, wote ni Watanzania.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliiomba Halmashauri hiyo ya CCM DMV kusaidia katika maendeleo ya Tanzania kwa kupanua wigo wao pamoja na kwamba lengo lao ni siasa na siasa ni sehemu ya maisha ya jamii na maendeleo ya jamii yanategemea siasa, kwa hiyo basi mnaposikia kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza Tanzania msisite Ubalozi upo wazi na utafanya kila liwezekanalo kuhakikisha muwekezaji huyo hapati vikwazo vyovyote.

Mwisho Balozi Wilson Masilingi aliwashukuru Watanzania kwa kuwa mabalozi wazuri nchini Marekani na kuwaasa kuishi kwa kufuata misingi na sheria za nchi ya Marekani.

 Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiongea jambo na mwenyekiti wa tawi CCM DMV Bwn. George Sebo kwenye mkutano wa Halmashauri ya CCM DMV siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 mkutano uliofanyika Hampton Inn, College Park, Maryland. Picha na Kwanza Production/Vijimambo Blog
Mkutano ulianza kwa sala na kuwakumbuka wote waliotangulia mbele ya haki.

Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn. George Sebo akifungua kikao cha Halmashauri ya CCM DMV kilichofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 katika ukumbi wa Hampton Inn, College Park, Maryland.

Saturday, December 05, 2015

Friday, December 04, 2015

Wanyonya Ume wa Mchungaji Wao Ili Wapone Maradhi Yao!

http://www.eurweb.com/wp-content/uploads/2013/02/valdesi-sobrino-picanto.jpg
Pastor Sobrino Valdeci Picanto wa Brazil
 
Mchungaji huko Brazil  Rev. Sobrino Valdeci Picanto, wa kanisa la pentecostal (walokole) aliwadanganya waumini wa kike kuwa wakinyonya ume wake (mboo) watafaidi maziwa maalum ambayo yatapona maradhi yao. Wengine aliwaambia watatajrika. Alisema kuwa ume wake unatoa maziwa enye nguvu na baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu!  Alisema ni lazima dawa imwagwe mdomoni ndo iwe na nguvu.

Jamani, tangu lini maziwa ya baraka yanatoka kwenye ume? Sana sana utapata ugonjwa wa zinaa au mimba! Huyo jamaa alipenda anyonywe tu! Mchungaji Picanto yuko gerezani kwa kosa la ubakaji sasa.

Acheni kundangayika!

Kusoma habari kamili BOFYA HAPA!

Serikali Mpya ya Rais Magufuli! - Katuni