Showing posts with label Singida. Show all posts
Showing posts with label Singida. Show all posts

Saturday, September 17, 2016

Mwenge wa Uhuru Wawasili Mkoani Singida na Ishara ya Uhuru wa Tanganyika

MWENGE wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Singida Mwenge huu ni ni kitu mfano wa kikombe chenye mpini mrefu na utambi ambacho aghalabu huwasha na kukimbizwa katika kusheherekea au kutukuza tukio fulani
Askari wa Jeshi la Polisi wakiulinda Mwenge ishara ya kuwasili muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Singida

Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo

Saturday, May 31, 2014

Serikali Kujenga hospiatli ya Rufaa Singida

DSC_0473

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Nathaniel Limu, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.

Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.

Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.

Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.

DSC_0429

Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.

Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.

Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).

Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.

DSC_0446

Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.

"Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia",amesema Kinana.

DSC_0453

Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.

DSC_0463

Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.

DSC_0481

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.

DSC_0499

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye hospitali hiyo ya rufaa.

DSC_0506

Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.

DSC_0496

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akisalimiana na Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman Mutani wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.

DSC_0522

Katibu Mkuu wa CCM Taifa akiongozana na mkuu wa Mkoa Kone, Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, wasaidizi wa Mbunge Duda Mugheny na David Mkufya wakimwongoza Kinana kutoka nje mara baada ya kukagua hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Saturday, November 16, 2013

Mazishi ya Martha Shani Tanzania

Na Swahili TV
Kwa niaba ya Familia, Kamati ya Mazishi Marekani na Tanzania na ndugu na jamaa wote kwa ujumla tumeona ni vyema nanyi mkaona matukio yote kwani mlishiriki katika msiba huu. Kwa mara nyingine tena tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wote mliofanikisha Shughuli zote Usafiri, Maandalizi mbalimnbali na hatimaye kuuhifadhi mwili wa mpendwa wetu, dada yetu, rafiki na kipenzi chetu Bi. Martha Shani.Mazishi yalifanyika Puma Sindiga siku ya Alhamisi ya Octoba 31, 2013. Video ya matukio yote tutaiweka soon hapa hapa Swahili TV Blog.

PICHA ZA MATUKIO YOTE
Alex akipewa pole na Shangazi wa Martha

Kushoto; Vincent Mughwai, Joseph, Alex akimshikia mtoto Chris beleshi akiweka udongo katika kaburi la Mama yake, huku Mchungaji Peter Ihema wa Kanisa la Pentekoste Puma akitazama . Mazishi yalifanyika Alhamis Oktoba 31, 2013 Puma-Singida.
Alex, Joseph, DMK, Muddy wakiwafuatilia shughuli za Mazishi Alhamis Oktoba 31, 2013 Puma-Singida.
AU INGIA

Tuesday, August 26, 2008

Wanafunzi wamwua Mwalimu wao Bongo!

Jamani! Bongo kuna nini siku hizi wanafunzi wanamwua mwalimu wao!!! Khaa! Na hivyo wana miaka 18 watawasaidia polisi na uchunguzi wao mpaka wana miaka 50!
*******************************************************************

Kutoka Michuzi Blog:

Wanafunzi mbaroni kwa tuhuma za kuua mwalimu wao

Habari toka Singida zinasema polisi mkoani humo wanawashikilia wanafunzi wanne wa shule ya sekondari ya Chemchem katika wilaya ya Iramba kwa tuhuma za kumuua mwalimu wao wa nidhamu, Rajabu Dude (49).

Kamanda wa polisi mkoani humo afande Celina Kaluba amewataja watuhumiwa hao mbele ya waandishi wa habari kuwa ni Shani Mtua (18), Mohamed Salum (18) and Emmanuel Daud (18) wote wanafunzi wa kidato cha tatu pamoja na Michael Msengi (18) wa kidato cha nne.

Kamanda Kaluba amesema kwamba tukio hilo lilitokea alhamisi usiku majira ya saa mbili unusu wakati marehemu akiwa anatoka kwenye matembezi katika kilabu moja cha pombe kijijini hapo.

Amesema wakati mwalimu akiwa anarejea kwake akiimba kwa furaha, alivamiwa na kukatwakatwa na kichwani na kuchomwa kisu kifuani, kabla washambuliani hawajatokomea gizani.

Kamanda huyo amesema mwili wa marehemu uligunduliwa na wanakijiji wenzie ambao waliuarifu uongozi na taarifa kupelekwa kituo cha polisi ambako upelelezi ulianza mara moja. Ndipo watuhumiwa hao wanne, ambao amesema wamekiri kuhusika na shambulio hilo, walipotiwa mbaroni.

Kamanda huyo pia alisema baada ya kukamatwa wanafunzi hap waliisaidia polisi kukipata kisu kinachosadikiwa kutumika katika shambulio kikiwa kimetupwa kichakani karibu na eneo la tukio.

Haikuweza kufahamika sababu ya shambulio hilo, lakini Kamanda huyo wa polisi amesema huenda lilisababishwa na kulipizwa kisasi kufuatia adhabu aliyopewa mmoja wa watuhumuwa siku chache zilizopita.

Amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika. Hakutaja itakuwa lini zaidi ya kusema upelelezi unaendelea