Jamani! Bongo kuna nini siku hizi wanafunzi wanamwua mwalimu wao!!! Khaa! Na hivyo wana miaka 18 watawasaidia polisi na uchunguzi wao mpaka wana miaka 50!
*******************************************************************
Kutoka Michuzi Blog:
Wanafunzi mbaroni kwa tuhuma za kuua mwalimu wao
Habari toka Singida zinasema polisi mkoani humo wanawashikilia wanafunzi wanne wa shule ya sekondari ya Chemchem katika wilaya ya Iramba kwa tuhuma za kumuua mwalimu wao wa nidhamu, Rajabu Dude (49).
Kamanda wa polisi mkoani humo afande Celina Kaluba amewataja watuhumiwa hao mbele ya waandishi wa habari kuwa ni Shani Mtua (18), Mohamed Salum (18) and Emmanuel Daud (18) wote wanafunzi wa kidato cha tatu pamoja na Michael Msengi (18) wa kidato cha nne.
Kamanda Kaluba amesema kwamba tukio hilo lilitokea alhamisi usiku majira ya saa mbili unusu wakati marehemu akiwa anatoka kwenye matembezi katika kilabu moja cha pombe kijijini hapo.
Amesema wakati mwalimu akiwa anarejea kwake akiimba kwa furaha, alivamiwa na kukatwakatwa na kichwani na kuchomwa kisu kifuani, kabla washambuliani hawajatokomea gizani.
Kamanda huyo amesema mwili wa marehemu uligunduliwa na wanakijiji wenzie ambao waliuarifu uongozi na taarifa kupelekwa kituo cha polisi ambako upelelezi ulianza mara moja. Ndipo watuhumiwa hao wanne, ambao amesema wamekiri kuhusika na shambulio hilo, walipotiwa mbaroni.
Kamanda huyo pia alisema baada ya kukamatwa wanafunzi hap waliisaidia polisi kukipata kisu kinachosadikiwa kutumika katika shambulio kikiwa kimetupwa kichakani karibu na eneo la tukio.
Haikuweza kufahamika sababu ya shambulio hilo, lakini Kamanda huyo wa polisi amesema huenda lilisababishwa na kulipizwa kisasi kufuatia adhabu aliyopewa mmoja wa watuhumuwa siku chache zilizopita.
Amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika. Hakutaja itakuwa lini zaidi ya kusema upelelezi unaendelea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Kun mwalimu mkali alipigwa Tambaza! Vijana walimpiga mawe kichwani! Ingawa alitoka madamu jamaa alipona na kuendelea kuwa mkali!
Post a Comment