Wednesday, September 14, 2011

Mgonjwa Muhimbili Anatafuta Ndugu Zake

PRESS RELEASE FROM MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL - DAR ES SALAAM, TANZANIA
(Unidentified Patient in ICU at Muhimbili Hospital in  Dar es Salaam)

Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipokea mgonjwa toka Hospitali ya Mwananyamala tarehe 18/08/2011 akiwa mahututi na hajitambui. Inasemekana kuwa mgonjwa huyu aliokotwa na wasamaria wema barabarani akiwa amegonjwa na gari usiku wa kuamkia tarehe 18/08/2011 ambao walimpeleka Hospitali ya Mwananyamala. Kwakuwa alikuwa ameumia sana Hospitali ya Mwananyalama iliamua kumleta Hospitali ya Taifa Muhimbili ili aweze kupata huduma na uchunguzi mkubwa zaidi.


Mgonjwa huyu hajulikani jina lake kwani hawezi kuongea toka alipoletwa kutokea Mwananyamala. Mgonjwa huyu alifanikiwa kuonwa na madaktari bingwa siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 na kufanyiwa uchuguzi wa vipimo mbalimbali ikiwemo X-Ray ya tumbo, kichwa, kifua na kiuno. Matokeo ya vipimo hivyo yalionekana kuwa kichwani kulikuwa na damu kidogo iliyoganda kutokana na kuvujia kwa ndani, picha za kifua na kiuno zilionyesha kuwa hakuna tatizo.

Picha ya tumbo ilionyesha kuwa bandama lilipasuka hali iliyopelekea kufanyia upasuaji siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 ili kuondoa bandama. Baada ya upasuaji mgonjwa alipelekwa moja kwa moja chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) siku hiyo hiyo ya tarehe 18/08/2011.

HALI YAKE:

Tangu apelekwe ICU hali yake bado ni mbaya, hajitambui. Aidha tangu tarehe 18/08/2011 hakuna ndugu au jamaa aliyejitokeza kuulizia hali ya mgonjwa huyu.

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unaomba yeyote anayemfahamu mgonjwa huyu atoe taarifa kwa ndugu na jamaa zake ili waweze kuja kumtambua ndugu yao. Tunaendelea

Imetolewa na:


Aminiel Aligaesha,
Afisa Uhusiano,
Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Septemba 2, 2011.

1 comment:

Anonymous said...

Maskini! Kutokana na shepu ya kichwa itakuwa rahisi kupata ndugu zake. Mungu awabariki waliomsaidia. Pia tuombe apone.