Tuesday, September 27, 2011

Tanzia - Mama Wangari Maathai (Mama Miti)

Mama Wangari Maathai (1940-2011)
Mama  Prof. Wangari  Muta Maathai, raia wa Kenya aliyepata Tuzo ya Amani ya Nobel, na Tuzo kibao kwa kazi na jitihada zake za kuhifadhi ardhi na miti amefariki nchini Kenya. Habari zinasema kuwa alifariki mjini Nairobi siku ya jumapili kutokana na ugonjwa wa kansa.  Chama chake cha Green Belt Movement kitendeleza kazi aliyoanza.

Mama Maathai alipigania haki za akina mama na maskini nchini Kenya. Alitunga vitabu kadhaa. Alikuwa mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kupata Ph.D katika sayansi za biolojia. Alipoona jangwa inazidi kukuwa nchini Kenya alianzisha mradi wa kupanda miti ili kuepuka janga hilo na hasa kuanzishwa kwa Green Belt Movement. Aliwahi kuwa Mbunge Kenya na pia alifungwa mara kadhaa kutokana na msimamo wake mkaliw wa kutunza ardhi ambayo mara nyingi ilipingana na serikali ya Kenya.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.     

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:  

3 comments:

Simon Kitururu said...

R.I.P!

Anonymous said...

WANGARI MAATHAI: is the President and Government that Kenya seriously needed thirty years ago - in order to prepare our nation for the challenges of today - a missed opportunity now bearing very bitter harvests for ordinary Kenyans.

Beloved Older Sister - you will always be our most beautiful and precious diamond - may Almighty GOD bless the Horn of Africa with one million Wangari Maathais

PGR Nair said...

It was with a tinge of sadness I learned about the death of the Kenyan environmentalist and social activist Professor Wangari Maathai. In every sense she radiated charisma, conviviality and hope among millions of Africans and was the greatest African who ever lived and was one of my heroes.I drop a pearl from my eyes in her memory. May her radiant soul light our lives

PGR Nair
Cochin, India