Friday, September 02, 2011

Utapeli Bongo - Eti Anahitaji Mpishi

Nimepata kwa Email:

*********************************************************************************
Kitu kilichonikuta siku ya J'mosi iliyopita Agotsi 27, 2011.

Mimi ni mpishi (catering) katika shughuli mbalimbali, kama munavyojua biashara matangazo nikajitangaza kwenye gazeti moja linalo toka kila siku shughuli zangu.

iku ya J'mosi asubuhi wakati naelekea kazini nikapigiwa simu na baba mmoja akajitambulisha kwa jina moja la( ...................................) aksema kunajamaa yake mmoja anahitaji mpishi kwa ajili ya kupikia wafanyakazi wake, akaniambia baada ya dakika kumi nimpigie, ili anipe maelezo zaidi. Nami bila hiana nikampigia nikiamini ni mteja, akaniomba nimrushie vocha ya sh 2,000 ili awasiliane na huyo jamaa yake kwa sababu yeye yuko saiti maeneo ya Tegeta na hana sehemu ya kununua vocha.

Kiukweli nilishituka kidogo na kujiuliza kama anahitaji vocha kwa nini asinipe hiyo no. ili mimi niwasiliane naye moja kwa moja, ila nikayaondoa hayo mawazo potofu na kuamua kumtumia vocha ya sh.1,000, baada ya kama dk 5 akanipigia cm na kunipa namba ya huyo jamaa yake pia alinisisitiza niwasiliane muda huo huo na kila hatua nitakvyokuwa nawasiliana naye nimpe jibu.

Nilimpigia na akanielekeza tukutane MOVEN PICK, bila kuchelewa nilikwenda nilipofika nikampigia akaniambia yuko Kigamboni anavuka nimsubuli kama dk 20 na atakuwa amefika, kweli nilisubili na kam hizo dk alizosema alinipigia cm na kuniambia niingie ndani, niliingia na kumkuta amekaa kwa tabasamu kubwa aknipokea.

Alijitambulisha kwa jina la( ............................) umri ni kati ya miaka 60, akanionyesha identity card yake title yake ni mhasibu mkuu. Bila kuchelewa akaniuliza uzoefu wangu wa kazi nami nikajieleza bila woga wowote na uzoefu wa kazi zangu, naye pia akanieleza kuwa yeye anafanya kazi kwenye shilika lisilo la kiserikali lionahudumia watoto yatima, kituo hicho kinaitwa HUCE OF CANADIAN ORPHANS kipo Kigamboni jirani na kwa Abud Jumbe, mfadhili wa kituo hicho ni mzungu so wanahitaji mtu wa kuwapikia wafanyakazi 50 wa pale kituoni kila siku chakula cha mchana tu, canteen ipo palepale kituoni kwa ajilia ya kupikia, tutaingia mkataba wa miaka miwili.

Akaniambia huyo mzungu anatoa dolla 6 kwa kila siku kwa mtu mmoja, hivyo akaniomba mimi bei yangu isizidi sh 5,000 ila itakayobaki itakuwa ya kwake na hiyo pesa ikiingia kwenye akaunti yangu nitampa cha juu yake. hapohapo akampigia yule mzungu ili niongee naye kumdhibitishia kweli nikaongea naye maelezo ya yule mzungu hayakupishana hata kidogo na yule jamaa.

Tukakubaliana na akaniambia kikao cha bodi ni siku ya J'tatu na leo yaani siku ile wanakikao cha watu wachache hivyo bac inabidi niwakilishe paspoti 2, full adreas yangu na dolla 50, vitu hivyo nimpe kabla ya saa 8 ili apeleke kwenye kikao, hiyo pesa akasema ni ada. Kiukweli alivyosema pesa zile pale pale nikashituka na kugundua kumbe muda wote nilikuwa naongea na matapeli. Nilichofanya sikutaka kumuonyesha kama nimeshituka tulikubaliana tukutane saa nane na akasema sehemu atakayokuwa atanijulisha ili nimpatie hizo pesa na hivyo vitu.

Mimi nikampigia polis mmoja yuko pale makao makuu na kumuelezea ili tuwawekee mtego, akajipanga lakini ulipofika muda akaniambia atakuwa Agakhan Hospital anakwenda kuona mgonjwa na kunisisitiza niwahi, baada ya dk kama 10 hivi akaniambia ameondoka anawahi kikao, ila anwani zangu nimtumie kwenye msg na pesa nimtumie kwenye m- pesa
pesa sikumtumia na mpango wa kumkamatisha ukashindikana kabisa, aliendelea kuniforce nimtumie pesa ili akamiliske mipango.

cm na majina yao nimeyahifadhi kwa usalama zaidi .

MDAU SY

2 comments:

Anonymous said...

Pole sana Mdau SY. Lakini unajuaje kuwa wulikuwa unaongoea na mzungu? Bora ulishituka mapema!

Anonymous said...

Usingeita polisi, ungetuita sisi watoto wa magomeni. Tungemfira mkundu wake, kisha tungempiga picha wakati akifirwa na kuzisambaza magazeti yote ya udaku. Angeukimbia mji na kurudi kwao mwakareli haraka sana.