(Mzee Kipara Majuzi akijaribu kutoka kitandani)(Mzee Kipara Mwaka 2007 Akipelekwa nyumbani baada ya kushuti Scenes zake katika Sinema, Bongoland II, katika sinema hiyo aliigiza kama Imam)
Wadau, sielewi nchi yetu Tanzania! Mzee Kipara aka. Mzee Fundi Saidi ni nyota na mkongwe katika sanaa za maigizo Tanzania. Lakini ona anavyoteseka na kuishi maisha ya dhiki! Wasanii wengi wa Tanzania wanaishia kuishi maisha ya dhiki na kusahauliwa kabisa!
Someni Malalamiko ya Mzee Kipara kwa KUBOFYA HAPA:
****************************************************************************
Kutoka Fundi wa Kombo Blog http://fundirkombo.blogspot.com/
Napenda nitoe masikitiko yangu kwa wasanii wa Sanaa ya Maigizo wote Nchini kwa kutoonyesha msimamo wa pamoja ili kuweza kumsaidia Mzee wetu Mzee Kipara (Fundi Said) ambaye kwa sasa ana afya ambayo sio nzuri pamoja na uzee lakini hali ngumu ya kimaisha ndio inayochangia zaidi.
Mzee Kipara ni msanii wa muda mrefu sana katika Tasnia hii ya sanaa ya Uigizaji, ni muigizaji mkongwe sana katika Taifa letu, kwa wale wasiomjua alianza kuigiza sanaa toka mnamo mwa miaka ya 1964 enzi za RTD (Redio Tanzania) kwa sasa TBC hii kwa faida ya vizazi vya sasa msio fahamu hili.
Baadae Mzee kipara walianzisha kikundi cha maigizo ambacho kikawa kinarushwa na TV ya ITV ambacho amedumu nacho kwa muda mrefu sana kikiitwa Kaole. Katika kipindi chote hiki cha Kaole aliwafundisha wasanii wengi sana ambao kwa sasa wengi mnawasikia au mnaziona kazi zao kwenye Luninga zenu.
Cha kunisikitisha wengi wao hawajaonyesha upendo wao hata kidogo kwa mzee huyu, nitakua mnyimi wa Fadhila kama sita mshukuru sana Stephen Kanumba nakumbuka alikua msanii wa kwanza kwanza kwenda kumsaidia huyu Mzee; namshukuru sana, najua wapo wengine ambao pia walikwenda kwa nyakati tofauti tofauti kuweza kumuona huyu mzee au hata kumsaidia kwa chochote kile.
Mimi binafsi kama mwakilishi wa KAPINGAZ Blog napenda kuwashukuru wote waliofanya hivyo, ila ombi langu kwenu ninyi wasanii wa sanaa ya Maigizo ni kwa nini msiandae tamasha lolote ambalo mnaweza mkakusanya kiasi kikubwa cha fedha kikaweza kumsaidia huyu Mzee wenu badala ya kwenda mmoja mmoja kumuona huyu Mzee, kumbukeni na nyie ni vijana kwa leo itafika wakati mtazeeka kama huyu mzee na watatokea wengine mmewafundisha hiyo sanaa naamini na nyie mnaweza mkasikitika kama mzee huyu.
Naomba niwape mfano wa Dada Asha Baraka, Mkurugenzi wa African Star (Twanga Pepeta) nampongeza sana huyu dada aliweza kuandaa tamasha la Dansi kwa ajili ya kukusanya michango ya kumsaidia Mzee Muhidin Ngurumo ili aweze kupata matibabu vizuri, na mpaka leo naandika masikitiko yangu, Mzee Ngurumo leo anapanda kwenye stage kuimba na wenzie katka tamasha la sikukuu ya Idd el Fitr.
Nawaomba wasanii wote katika sanaa ya maigizo muweze kulitazama hili la Mzee Kipara kama ni jambo lenu wote, na hata mnapokua mnakwenda kwenye vikao vyenu na BASATA muweze kuliongelea hili, ili muweze kua na umoja wenye nguvu wa kuweza kusaidiana kwenye matatizo kama haya. Tunawaona mara kwa mara mnaenda kufanya shughuli mbali mbali sehemu tofauti, hasa za kujipongeza katika mafanikio flani ni vema mnapokua huko mkumbushane la mzee huyu msimuache aishi maisha haya ni aibu kwenu wasanii wote hasa zaidi nyie mliopitia Kaole.
Naomba wana Blog wenzangu tushirikiane katika hili. Asante
************************************************************
Kama Unataka kuchangia Mzee Kipara tafadhali tembelea Blogu ya Kaka Michuzi:
au BOFYA HAPA
3 comments:
POLE MZEE KIPARA LAKINI PAMOJA NA HAYO LABDA NA WEWE ULICHEZEA MAISHA HUKUJIANDAAA VEMA, UTHIBITISHO NI KUOA NA KUACHA, MARA NYINGI WATU WENYE TABIA YA KUACHA MKE WA KWANZA HAWAFANIKIWI MAISHANI
Wasanii hilo ni somo tosha, acheni kujirusha jengeni nyumba ,nunueni mashamba ujana unapita upesi na majuto ni mjukuu, msianze kusingizia ooh serikali,, serikali yako ipo katika mipango yako, acha uzinzi, acha pombe na mtunze ndoa zenu, somesha watoto watakuja kuwasaidia baadae, msioe na kuacha, dunia hii imejaa wazuri wengi hamuwezi kuwamaliza,.
kwanini wasanii wa filamu wasimsaidie hata wakafanya harambee jamani mjifikirie huyu ni mwenzenu acheni kufanya starehe.
Post a Comment