Tuesday, September 06, 2011

Mzee Kijana Mhe.Prof. Kapuya

Yaani siku hizi ukiwa Celebrity Bongo mapaparazzi wanakufuata kila uendapo! Hebu cheki Gazeti ya Udaku wiki hii! Huyo msichana anaweza kuwa binti au mjukuu wake. Huu mtindo wa densi unaitwa nini?

Nimepata kwenye email. Sijui ni gazeti gani huko Tanzania. Wadau, hebu nisaidie kujua hii ni cover ya gazeti gani,

7 comments:

Anonymous said...

Ukipewa uongozi wa Nchi lazima ujiheshimu!Na kama huwezi achia ngazi ili upate muda mzuri wa kuzunguka kwenye hiyo miziki na mabarabara. Hata hao Wazungu wakikosa kujiheshimu huwa Wanawajibishwa!

Anonymous said...

Duh!Mheshimiwa alijisahau nini? Mzee mxima anafana niniye klabu ya viajana? Huyo binti kafurahi huoata shugadaddy mpaka majassho yanamtoka!

Anonymous said...

Nchi kama Marekani ingebidi jamaa ajiuzulu!

Anonymous said...

Kuna hotuba moja ya Baba wa Taifa Julius Kambarage aliitoa wakati CCM wanatafuta mgombea wa uchaguzi nafkri 1995. Alisema tunataka kiongozi mwenye maadili.
Aliendelea kusema hatuwezi kuchagua mhuni na kumpa uongozi wa nchi. Akasema kama mtu ni mhuni aendelee kufanya uhuni wake huko mitaani ´lakini kiongozi anapaswa awe mtu wa mfano (role models). Sasa sijui kama viongozi wetu kweli wamepita huu mtihani wa maadili ili wafae kuwa viongozi au mradi liende.

Siku moja nilimwona askari moja amelewa sana alafu anafanya kazi, na araia wala hawajali lakini sijui kama kipindi cha mwalimu unaweza kumwona askari au kiongozi akiwa amelewa kwa kiwango kile muda wa kazi. Nilikuwa mtoto wakati Nyerere akiachia uongozi hivyo siwezi kusema ilikuwaje katika maadili kipindi chake.

Anonymous said...

Ni Global publishers

http://www.globalpublishers.info/profiles/blog/show?id=5398006%3ABlogPost%3A221501&xg_source=activity&page=4

Anonymous said...

todessSASA KIONGOZI NDIO ASILE URODA?

ACHENI USHAMBA WENU HATA BABA ZETU WANAFANYA HIZO

Anonymous said...

Nani alikudanganya kuwa Paka mzee hanywi maziwa? Kwanza hunywa yale yenye cream mzuri. Powaaa Prof.enjoy wakati ni huu. "Life you live only once, but when lived well, there is no regret".