Wednesday, December 17, 2008

Rest in Peace - Prof. Aggrey Nzali

Marehemu Prof. Aggrey Nzali

Nimepokea habari hii leo kwa masikitiko mno. Prof. Nzali alifariki mwezi Oktoba baada ya kupata ajali ya gari.

Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.
Kwa habari zaidi tembelea Jamii Forums:
http://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/19728-prof-nzali-afariki-dunia.html
*******************************************************
Wadau,

Nimesoma habari ambayo kwa kweli ni vigumu kuamini.

Ninaomba sana mwenye taarifa juu ya Prof. Aggrey Nzali wa Department of Engineering UDSM anitumie e-mail chemiche3@yahoo.com.

Prof. Nzali alikuwa rafiki wa marehemu mume wangu Prof. Henry Kadete, tulikuwa naye Uholanzi mwaka 1986 na alisimamia ubatizo wa mwanangu.

7 comments:

John Mwaipopo said...

Pole Chemi

Ni kweli Profesa Nzali alifariki. Nimemfahamu binafsi mwezi wa saba mwaka huu huu. Nilifahamiana naye wakati nafanya kazi niliyopewa na Directorate wa Research and Publications ya UDSM. Prof Nzali akawa mtu wa kuonana naye kule engineering.

Baada ya kumaliza kazi ile akaendelea kuwa rafiki. Hebu fikiria tofauti zetu za kitaaluma na kiumri lakini tunakuwa marafiki.Aliendelea kupenda kunitumia katika shughuli zake zingine.

Siku ya kwanza ananipigia zimu saa 4 usiku tena kutokea ofisini. anaongea kinyakyusa kidogo(alikuwa mbena) na kunitania kuwa mbona leo sijaenda kujirusha. Baada ya hapo anajitambulisha "Mie Aggrey". Hasemi 'profesa' mpaka baada ya kuuliza sana. Alikuwa akiongea kwa staili ya kijana mwenzangu vile.

Nilimfahamu kwa kipindi kifupi sana lakini kwake nilijifunza mambo mawili: Kunyenyekea na kusaidia unapoweza kusaidia.

Pole Chemi siye tulishapoa kwa kumpoteza mwanzazuoni huyu.

Anonymous said...

Mh hii hata mimi inanisikitisha, Prof huyu niliwahi fanya kazi nae flani hivi pale chuo na mambo yalikuwa mazuri tu Mungu amrehemu.

Simon Kitururu said...

R.I.P Prof. Aggrey Nzali

Anonymous said...

Chemi, tafadhari jaribu kufanya uchunguzi wako kama mwandishi wa habari na mtu wa karibu wa Prof. Nzari(R.I.P)

Prof pia mimi alikuwa mwalimu wangu pale FoE (1993-1997) kama alivyokuwa Prof. Kadete (R.I.P). Nimejaribu kufuatilia kidogo kwa jamaa wachache nyumbani, Prof. Nzari hakufariki kwa ajari, aliugua kwa kipindi fulani.

Of course, kama ilivyokuwa kwa Prof Kadete, taaluma imepoteza watu muhimu kwa msiba huu.

Mpaka hapo baadaye,
Ex FoE Student

Chemi Che-Mponda said...

Natoa shukurani kwa wote waliowasiliana na mimi kuhusu kifo cha Prof. Nzali. Pia mke wa marehemu amewasiliana na mimi na kunipa maelezo kwa kirefu.

Nasema tena. Asante.

Anonymous said...

Najua ujumbe wangu wa hapo mwanzoni uliupata. Nilichotaka kusema ni kwamba Prof. Nzari aliugua na hakufariki kwa ajari kama ulivyokuwa umeandika mwanzoni hapa.

Apumzike pema, Prof. Nzari.

Ex FoE Student.

Anonymous said...

Anonymous wa dec 22,2008,8:58,ukweli ni kwamba Prof.Nzali alifariki baada ya kulazwa kutokana na ajali ya gari aliyoipata.Habari kama ilivyoandikwa ni sahihi kabisa.