Na Happiness Katabazi
SIKU
yangu ya Leo Juni 7 Mwaka 2014, Imeingiwa na dosari ya kuondokewa na
Furaha niliyokuwa nayo tangu asubuhi baada ya kusoma ukusara wa Mtandao
wa kijamii, wa Mwandishi wa Habari za Michezo Mwani Nyangasi,saa 9:30
Alasiri, na kuona Habari Isemayo Aliyekuwa Kiongozi wa Michezo nchini,
Kanali Mstaafu, Ally Mwanakatwe, amefariki Dunia.
Habari
hiyo imenisikitisha na kuniaribia jioni ya Leo.Ili kujiridhisha kuwa
ni kweli Mzee wangu Mwanakatwe,kafariki nilichukua simu yangu na
nikaipiga simu ya Mwanakatwe itapokelewa mtu ambaye Hana sauti ya
Mwanakatwe nikajitambulisha.
Nikamuuliza
taarifa hizi za Mzee wangu Mwanakatwe Kuwa eti amefariki, MTu Huyo
ambaye alijitambulisha Kuwa ni shemeji wa Marehemu aitwaye Denis
Mtegeti, Alisema ni kweli amefariki, Niliumia sana na kushusha pumzi na
Kisha kuendelea kuongea na Denis.
Akasema
Mwanakatwe alikuwa Ana historia ya Ugonjwa wa Shinikizo la Damu ila
hadi Jana jioni alikuwa naye alikuwa ni mzima wa Afya na walikuwa wote
Katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo wakimuuga za mmoja wa ndugu
Yao.
Lakini
Leo Mwanakatwe wakati akiingia bafuni kwake kuoga,nyumbani wake Mbezi
Beach Dar es Salaam, alishikwa na Hali isiyokuwa ya kawaida, akiwa
bafuni akawa makelele ya kuomba msaada huku akishika ukuta wa bafuni
wakapata msaada ambapo walimtoa bafuni na kumkimbiza Katika Hospitali
ya Rufaa ya Jeshi na kwamba alifia njiani Kabla akatikishwa Katika
Hospitali hiyo na kwamba mwili huo umeishahifadhiwa Katika Hospitali
hiyo na upo nyumbani KWA Marehemu Mbezi Beach, unaweza teremka Kituo Cha
Makonde au Jogoo na Taratibu za Mazishi zinaendelea.
Binafsi
nilimfahamu Mwanakatwe kupitia Kazi yangu ya uandishi wa Habari na pia
Mwanakatwe alikuwa alifanya kazi na mama yangu Mzazi na baba yangu Mzazi
pale Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi(JWTZ), ' NGOME',
Upanga. Dar es Salaam.
Mara
ya Mwisho kukutana na Mwanakatwe ni Mei Mwaka huu, Katika Hospitali ya
Jeshi Lugalo, Tulijadili mambo siasa za nchi hii, na tukakumbushiana
Enzi zile wakati alipokuwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Jeshi, ilipo
Posta Mpya Dar es Salaam.
Mwanakatwe
wakati ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Jeshi,nilikuwa na kwenda
kumtembelea Mara kwa Mara pale na alikuwa a kielelezo na kunifundisha
mambo ya jeshi letu lilivyo.
Mwanakatwe
na Marehemu Dittopile Mzuzuri wote Kwa nyakatip tofauti walikuwa
wakiniasa sana, Kuwa Katika uandishi wangu ni sipende kuandika Habari za
uzushi za kukichafua JWZT Kwani JWTZ siyo Chombo Cha kuchezewachezewa
ovyo ovyo na kwamba Jeshi ni Chombo nyeti na kwamba raia tusione
tunalala na tunaamka Kwa Amani tukae tukijua kuna watoto watu yaani
Wanajeshi Wanajeshi macho kujilinda nchi hii isivamiwe na maadui.
Siwezi
Kusema yote niliyokuwa nikielezwa na kafundishwa na Mzee wangu
Mwanakatwe hapa, ila aliyokuwa amenifundisha yalinisaidia sana Katika
uandishi wangu na kufahamu Vyema vyombo Vya Ulinzi na Usalama
vinafanyaje Kazi na vyombo Vya Habari hatupaswi kuvishutumu bila Kuwa na
Sababu za Msingi za kuvishutumu.
Mwanakatwe
nitakukumbuka sana niliyokuwa nakuja pale NGoME na Makumbusho ya JWTZ
wakati mwingine nilikuwa nakuja na mwandishi wa Gazeti la Habari Leo ,
Halima Mlacha ambaye ni mtoto wa Kanali Mnyani, Wanajeshi wadogo
walikuwa wakitupokea vizuri na kutuia sisi ni " watoto wa Wanajeshi",
hatuna madhara.
Nitamkumbuka
Mwanakatwe Kwa utanishati wake, jamani Mwanakatwe alikuwa ni mtanashati
hasa, ukiingiia ofisini kwake Ana Mti maalum, uliotundikwa uniform zake
,zimepigwa pasi ,zimenyooka, kiatu kinameremeta Kama Kiatu Cha Jeshi
alichokuwa anavaa Mnadhimu wa JWTZ Mstaafu, Abdullahman Shimbo.Kwakweli
ni watanashati Wanajeshi hawa licha simaanishi Kuwa Wanajeshi wengine
siyo watanashati.
Mwanakatwe
Ni miongoni mwa Wanajeshi ambao unajeshi ulikuwa Kwenye Damu yake, na
alikuwa Mwanajeshi kweli hata unavyomtazama na kumsikiliza mazungumzo
yake.
Hakina kifo Chako ni pigo KWA JWTZ, CCM, wapenzi wa Soka na familia yake Kwa ujumla.
Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
The Late Colonel Ally Mwanakatwe |
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Juni 7 Mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment