Taarifa kutoka kwa mdau S.A.
June 24, 2014
Wadau,
Jioni ya leo majambazi
wamempiga risasi mbili kifuani na tumboni mfanyabiashara maarufu kwa
jina la Warwa na inasemekana amefariki dunia papo hapo kwenye duka lake
la uwakala wa mitandao ya kutuma na kupokea pesa maarufu kama mpesa,
airtel money na tigo pesa lililopo soko kuu kwenye barabara ielekeayo
kwenye benki za nmb, nbc na posta.
Mpaka sasa mji wa Geita
umekumbwa na taharuki kubwa kutokana na tukio hilo. Mpaka kufikia saa
mbili usiku huu bado kulikuwa na makundi ya watu wengi kwenye eneo la
tukio na kwenye maeneo ya hospitali kuu ya wilaya ya Geita.
Inasikitisha sana maana
inasemekana kuwa pamoja na polisi kuwa karibu na eneo hilo lakini
majambazi hao wamefanikiwa kutoroka kwa kutumia pikipiki. Vishindo vya
risasi zinazoamika kumuua ndugu Warwa vilisikika mbali kutoka kwenye
eneo hilo la tukio.
SA.
************************
June 25, 2014
Wadau,
Taarifa zilizopo Geita
zinaoonyesha kuwa majambazi hao waliuwawa jana ile ile, walipoondoka na
pikipiki, walikuwa wakifuatwa kwa nyuma kwa mbali na madreva pikipiki
ambao waliwatonya polisi uelekeo walikokuwa wanakimbilia!
Inasemekana walikuwa
wanakimbilia uelekeo wa Nyang'wale, polisi wa Geita wakawajulisha wenzao
wa Nyang'wale ambao nao wakawatangizia hao jamaa barabarani na kuwaua.
Utambuzi wa maiti za majambazi
hao wawili ulionyesha kuwa mmojawapo ni mpwa wa marehemu aliyevamiwa na
kuuwawa! Na hii ni baada ya dada wa Warwa kumtambua kijana huyo kuwa ni
mwanae!
Habari zaidi zinasema kuwa,
kabla ya kupigwa risasi zile kifuani na tumboni, marehemu Warwa
alimtambua mpwa wake huyo na kutamka kuwa, "....hata wewe .....
umejiunga na ujambazi kuja kunivamia mimi mjomba wako?", na huenda hiyo
ilikuwa sababu ya kuuwawa kule na kijana huyo!
Taarifa zilizopo hapa Geita
zinasema jana hiyo hiyo, ndani ya muda mfupi sana, kulikuwa na matukio
mawili ya ujambazi, hilo la hapo kwa marehemu Warwa na jingine kwa
mfanyabiashara wa jumla wa bia ndugu Inyasi, ambaye yeye hakukutwa
dukani bali mke wake na watu wengine. Hapo waliishia kupora fedha na
bostora iliyokuwemo kwenye droo na kukimbilia kusikojulikana.
Haijajulikana kama matukio haya
yalifanywa na watu walewale au tofauti, lakini inasemekana yana
uhusiano. Inasemekana kiasi kikubwa cha fedha kiliporwa, na wadau
wanatonya kuwa huenda pesa hiyo ilikuwa ni zaidi ya shilingi mil. 50!
SA.
1 comment:
Poleni sana Geita. This is a failed state. A dysfunctional government. A a jungle of ruthless wolves.
Ukiona wananchi wanaishi kwa hofu bila amani katika nchi yao basi ujue taifa hilo liko ukingoni kucollapse.
Jana sister kauawa mchana kweupe pale Ubungo, Dar es Salaam, lakini hakuna atakaye kamatwa, na baada ya wiki tutasahau kama vile hakijatokea kitu.
Leo Geita. Usiku huu hatuji wapi na nai atakufa. Na kesho hivyo hivyo.. Lakini hakuna anayesema neno wala kuinua sauti kusema "enough is enough"
Hakuna aliye salama isipokuwa wale wenye madarka, pesa, na wote wanoishi kama wafalme kwa kodi zetu.
Badala ya kutulinda, wanajilinda wao na familia zao. Polisi wetu si kwa ajili yetu bali kwa wajili ya wenye pesa, tena pesa zinazotokana na jasho letu.
Sisi ki vyetu na wao kivyao. Tutaendelea kuchinjwa na kutiwa vilema mmoja baada ya mwingine, huku wao wakihubiri "nchi hii ni ya 'utulivu' na 'amani'
Nani katulia?
Nani ana amani?
Ni wale wanaolindwa na polisi wetu huku wengine tukiuawa bila wahalifu kuchukua hatua! (where the culture of impunity rules, everyone is a king of lawlesness)
Halafu bado watanzania tunacheka. Tunawashangilia. Na wengine ndio kwanza wanashabikia upuuzi upuuzi wa watu wenye sare za kijani.
Tumelaaniwa?
Post a Comment