The late Nkwabi Ng'wanakilala |
Aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la Habari Tanzania SHIHATA na mhadhiri wa chuo kikuu cha mtakatifu Agustino, Nkwabi Ng'wanakilala amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa anaugulia matatizo ya figo yaliokuwa yanamsumbua kwa takribani wiki tatu. Mungu ailaze roho ya comrade mahala pema!
7 comments:
Poleni SAUT, poleni wanataaluma wa habari.
Kitabu vyake kuhusu Mass Communication and Development of Socialism in Tanzania, kilinisaidia kuongeza maarifa na taarifa, wakati nikiwa chuoni, hasa wakati wa kuandika dissertation.
Alikuwa mmoja wa nguli katika tasnia ya habari.
Poleni familia, ndugu, jamaa na tasnia nzima ya habari nchini kwa msiba huu.
Pumzika kwa amani kwa kazi kubwa uliyoifanyia nchi yako.
Kwangu binafsi, hili ni pigo kubwa kwa sababu tulikuwa walimu pamoja hapo Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Born Again Pagan
RIP Nkwabi Ng'wanakilala umetangulia tuko nyuma yako
Huyu bwana (Mungu ampe pumziko salama) na kitabu chake cha historia ya Tanzania hebu kifuatilie. Nchi hii hatujaandika kabisa kuhusu Tanzania na Tanganyika yetu.
Alikuwa nguzo ya taaluma ya habari SAUT. Mungu amlaze mahali pema peponi...AMINA
Ni msiba mkubwa kwa badhi yetu tuliopitia mikononi mwake!.
Tulipojiunga RTD miaka ya mwanzoni mwa 90's kulitokea change of arms kwa David Wakati (RIP) kustaafu na nafasi yake kuchukuliwa na Nkwabi akitokea Shihata.
Alifanya mageuzi makubwa ikiwemo kuanzisha FM. Sisi watangazaji vijana alitulipia decent houses na some privileges fulani fulani as a motivation to stick kwenye chalenges za more media freedom na kuingia kwa private sector kwenye broadcasting, hivyo mimi na Abou Liongo tukapangishiwa a shared flat pale Sharif Shamba Ilala.
Alipoanzisha City Radio, Betty Mkwasa ndio alipewa Ukuu wa City Radio na mimi nikawa msadizi wake, tukipewa budget inayojitegemea, ambayo ilileta heri ya aina yake.
Nkwabi alikuwa dynamic na alikubali changes for the better hali iliyopelekea kupata upinzani toka kwa ma conservatives wa "life as usual".
Alipoondolewa tuu, zile privileges zote zilifutwa na ndipo ikafuatia mass exodus ya watangazaji zaidi ya 10 kuhama kwa mpigo wakiongozwa Mikidadi Mahmood, Julius Nyaisangah (RIP), Betty Mkwasa, Ahmed Kipozi, Karim Besta, Aboubakar Liongo, Florah Nducha na wengine.
Alikuwa mtu wa watu!.
RIP Nkwabi Ng'anakilala!.
Pasco
Post a Comment