Saturday, June 28, 2014

TAMWA kutoa Elimu Kupambana na Ulevi Kupindukia

TAMWA kutoa elimu kupambana na ulevi Kupindukia
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo.
KITUO cha Usuluhishi (CRC) kinachofanya kazi chini ya Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) kimejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha kinapambana na matumizi ya pombe kupindukia kwa jamii suala ambalo limezidisha vitendo vya ukatili wa jinsia unaofanywa na watumiaji pombe kupindukia.

Akizungumza na wahariri wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka alisema utafiti uliofanywa na Shirika la IOGT International unaonesha kuwa kiwango cha unywaji pombe jijini Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake huku ikibainika kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya vitendo vya ukatili na matumizi ya pombe kupita kiasi. 

Bi. Soka alisema takwimu zinaonesha kuwa wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha vipigo, kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77, huku kiwango cha ukatili kwa wanawake ambao waume ama wenzi wao hawanywi pombe ni asilimia 33.

"...Utafiti uliofanywa na shirika la IOGT International unaonyesha kwamba kiwango cha unywaji pombe katika jiji la Dar es Salaam ni asilimia 47.6 kwa wanaume na asilimia 29 kwa wanawake...lakini takwimu kutokana na utafiti wa Demographia na Afya Tanzania (TDHS) 2010...unaonesha wanawake ambao waume zao wanalewa mara kwa mara wengi wao wanakumbana na ukatili unaohusisha kipigo/kuumizwa na ukatili wa kingono kwa asilimia 77," alisema.

Aidha aliviomba vyombo vya habari kushirikiana na TAMWA kutoa elimu kwa jamii kupunguza matumizi ya pombe kupindukia kwani licha ya ukatili huo familia pia zimekuwa zikiathirika kiuchumi juu ya matumizi ya pombe huku baadhi ya watoto wakikosa huduma za msingi kutoka kwa baadhi ya wazazi ambao ni walevi kupindukia.

Alisema TAMWA inatekeleza mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unaosababishwa na pombe huku lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha maisha ya wanawake na watoto yanaboreshwa kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupindukia.

Hata hivyo alisema tayari chama hicho kimeanza kufanya utafiti mwingine katika Wilaya ya Kinondoni kuangalia madhara yanayotokana na unywaji wa pombe kupindukia ili kuangalia hali halisi ya matumizi ya pombe eneo hilo na madhara ambayo yamekuwa yakitokana na matumizi hayo.

Alisema malengo mengine ya mradi ni pamoja na kuboresha maisha ya wanawake na watoto kwa kuimarisha sheria na kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe katika wilaya ya Kinondoni na pia kujenga uelewa miongoni mwa jamii juu ya madhara yatokanayo na unywaji wa pombe kupindukia. 

Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA aliongeza kuwa mapambano hayo pia yatasaidia, kukabiliana na matumizi ya pombe na kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu ukatili dhidi ya wanawake unaotokana na matumizi ya pombe, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wa jamii kukabiliana na ukatili unaosababishwa na unywaji wa pombe dhidi ya wanawake na watoto.

2 comments:

Anonymous said...

Study na pilot area yao na iwe Dodoma ktk rural areas mojawapo TZ. Huko saa 2 asubuhi hata viongozi wa vijiji wamelewa. Siku hizi wanapanda mmea unaoitwa Rosela au Choya. Maua hulowekwa, huchemshwa maji yake kutiwa unga kidogo, kisha harira-pombe tayari wanalewa. pamoja na uzuri wa Choya kama maua ya juice nzuri-ni tatizo. Zamani akina mama wakitumia maua yake mabichi kuunga mboga kupata uchachu wake. zao la choya limeleta utata vijiji vya wilaya zote wa mkoa wa Dodoma-Ulevi. kila mtu mijini na miji midogo-frame za bar kuuza pombe ndio uchumi mkubwa. Wataweza kuzuia kweli na watu wanaanza kunywa kuanzia asubuhi. Ilikuwa rahisi wakati wa TANu na chama kimoja CCM amri ikitoka ndio hiyo. Sasa huu utandawazi, utandawizi na upinzani na tamaa ya wachaguliwa kupata kura-watu wangu wanaganga njaa waache!! Itawezekana kuzuia ulevi na uuzaji pombe ndio mtu anapata fedha?
Kama imeshindikana kupunguza mifuzo na mimomonyoko ya ardhi inayoharibu mazingira na kuathiri kipato cha jamii/familia-kuzuia kuuza na kunywa pombe na vipigo vinaonekana, ubakaji na umalizaji fedha za kipato duni ni ndoto ila tunakaribisha juhudi za TAMWA. kuna changudoa wa aina zote nje ya ofisi ya TAMWA, Legal and Human Rights na hawajaweza kuwaelimisha na kuzuia wasijiuze na wanaonekana nje ya ofisi.Mitaa yao. Bar kila kona hapo Sinza ilipo LHRC (haki za binadamu na wanasheria wake) tuone hapo kijitonyama-Sinza kubadilike hizo bar next to them zisiuze pombe asubuhi. Watu husema-Mganga hajigangi. Kubadilika sisi watanzania ni tata kama donda dugu.

HK said...

Yaani ningekuwa na cheo-ni kurudisha wajerumani kuja kutupiga bakora tubadilike. maana fimbo zao hadi leo vizee vinazikumbuka.

Ona hizi barabara na mitaro mikubwa ya maji ya mvua iliyopo mfano Dar na miji mingine. angalia wanavyotupa takataka humo. malundo ya taka kila kona. ananyoa nywele saluni anatupa humo. Mfumo wa kufakia na kuzoa taka, kutupa taka dampo upo decentralized kimtaa. lakini tunaepuka kuchangia takataka kila kona na mtaro na hizi huzima na kuona watu wakiogelea kinyesi mpaka magodoro yao. Lakini hatubadiliki. Mvua ikiisha takataka tunatupa usiku masanduku na viroba vya taka barabarani na mitaroni.
Moto ukiunguza majengo, ukiisha tunajenga na kuziba tena kuliko kwanza bila ya kuacha nafasi na kujali hata barabara za kupita wenyewe na mizigo tabu. Umewaka mwenge, mchikichini, kila mahala ni hivyo.
Suala la jangwani sunna kila masika watu kukimbilia juu ya paa, na kupewa maeneo, mabati na simenti, kupoteza mali, watoto, wazazi, ndugu-wamebadilika-NO
wanaingiza mifugo katika vyanzo vya maji, mito, inakauka na kuchafuka-kisha wanahara, kufa, kupoteza mifugo kwa kukosa maji-wanaipunguza? wanalinda vyanzo vya maji-mapigano tu. Mbona msukuma, MMaasai, Mang'ati akiwa kwao analima na halishii mifugo yake mpunga, mahindi, ngwara, njegele alimazo bali chalinze na kilosa mahindi na mpunga ni majani ya ngo'mbe?wanabadilika.No

wanandoa wengi wana michepuko na hawataki kutumia condon na wanaongoza ktk wenye HIV-kuwaje?
Nje ya ofisi ya LHRC iliyo karibu na chuo cha Ustaei jamii kuna changu doa za aina zote hadi vitoto mitaa hiyo. Nje ya jengo la TGNP kuna wananchi wamevamia mabibo waste water/sewage stabilization pond. hapo pana biashara ya mihogo, majumba ya kukaa, mauzo ya vyakula na pombe. maji ya kinyesi next to vyakula na nyama choma. Mbu wa matende na mabusha ndio wanapozaliwa. Ramani, picha na michoro ipo kuonyesha eneo lilikuwa fence likitunzwa vema miaka ya kiwanda cha urafiki na ni sehemu ya DSSD/DAWASA kuangalia. Viongozi wanaona, NGO zinaona, Idara ya afya, na maradhi yake hayana kificho. Mbona tunakesha kula na kunywa kinyesini? Nyama zinaning'inia mainzi tele tunabweda tu?

NGOs hazioni vyangudoa wa DSM hata Sinza, Kijitonyama na mashoga mwananyamala, kinondoni municipality, Buguruni makao makuu yao? Maandamano ya kisiasa namba one action haya ni kazi ngumu kutokana na tabia zetu za kisasi. Kawaondoe, wafungie wakugeche au kukuwerema au kukufulila!!
Ndio maana NGOs zipo na wananchi wanauza vyakula uchafuni, akina mama wapo bar na watoto kutwa, mama ntilie na vitoto mpaka usiku wa manane. Watoto wanaona uovu wote ukiongea nae anakubetulia mdomo. Ukienda machimboni ni hivyo pombe, umalaya, kuchezea mercury, video za matusi na wanaoweka bar na video hizo ni wazazi-wanaganga njaa. Solution-za kuwaondoa, kubomoa, kuwapeleka mahakamani-vita, mpambano. Kuelimisha bila positive change wao kubadilika imekuwa tata miaka yote. Siasa inaingilia inakuwe nuksi katika mabadiliko ya tabia. Utafunga na kupiga wangapi kabla hawajaua pilice ikabidi upeleke JWTZ badala ya hawa kwenda congo-somalia?
Skeptical. Health for all by year 2000 imekuja imeshindikana. year 2015 na 2025 itaingia na kutoka itatukuta tumehamia station na vibaraza vya rapid bus transport mpaka mvua iishe turudi jangwani. Pombe zitauzwa hapo, kubaka vitoto na kuchafua mazingira hapo. Mbunge wao atawatembelea hapo kuwapa pole na kugawa maji na chakula!! Akiwa bungeni ni kubwata kutanua mdomo na kulaumu GVT lakini akiwa jimboni kwake hahamasishi haya watakayo kufanya TAMWA ila anapita na kuwapungia mkono.
Chezea bongo wewe!!