Monday, March 23, 2009

Hoteli Mbili Zaungua Moto Bagamoyo!

Paradise Hotel

Kutoka Michuzi Blog:

paradise resort:imeteketea yooote hata foronya haikuwahi kuokolewa

KATIKA KUFUATILIA KWA KARIBU BALAA LA MOTO HUKO BAGAMOYO, GLOBU YA JAMII INAPASHA KWAMBA HOTEL ZA PARADISE NA OCEANIC BAY (PICHANI) ZIMETEKETEA KABISA NA MOTO.

KWA BAHATI HAKUNA MTU ALIYEJERUHIWA ILA INADAIWA HASARA INAKADIRIWA KUWA YA MAMLILIONI YA SHILINGI.

SHUHUDA WA GLOBU YA JAMII ALIYEKO HUKO AMEHABARISHA SASA HIVIKWA VODA KWAMBA MAJENGO YOTE YA HOTELI YA PARADISE YAMETEKETEA NA KWAMBA HAWAKUWAHI KUOKOA HATA FORONYA AMA GODORO AMA UFAGIO.

HALI KAMA HIYO IMEREKODIWA PIA KATIKA HOTELI YA OCEANIC VIEW, AMBAYO NI JIRANI NA PARADISE, ILA YA LIVINGSTONE CLUB, AMBAYO PIA JI JIRANI KWA UPOANDE KWINGINE, IMENUSURIKA KABISA. INASEMEKANA HII NI KWA SABABU YA UPEPO WA BAHARI KUPEPERUSHA MAKUTI KUELEKEA OCEANIC HOTEL
AMESEMA KWAMBA MOTO HUO, ULIOANZA ASUBUHI, ULIDUMU KWA MUDA WA DAKIKA 15 TU NA HOTELI ZOTE MBILI ZIKAWA ZIMETEKETEA.

YAANI FAYA AMBAO WALIKIMBIA TOKA DAR KWENDA BAGAMOYO KWA KASI ZOTE WAMEKUTA MAJIVU TU. PICHA KIBAO ZAJA MUDA SI MREFU UJAO..

************************************************

Wadau,

Miaka mingi hizi hoteli za kitalii zimeonywa kuhusu ujenzi wa makuti hasa kuezekea makuti. Mnakumbuka hall la Bahari Beach hotel ilivyoungua moto miaka ya 80? Mnakumbuka Hall la Bagamoyo College of Arts ulivyounga na kusababisha hasara kubwa?

Ni kweli makuti yapendeza ni bei rahisi na yanvutia watalii, lakini kuna faida gani kujenga nayo wakati hakuna sprinkler system mle ya kuzima moto kama utatokea? Hebu ona sasa? Hata kulia tunashindwa, tumepigwa butwaa!

Na wageni waliofikia kwenye hizo hoteli wamepata hasara. Huenda kuna wageni kutoka nchi za nje wameptoeza mpaka hatai za kisafiria! Watalipwa fidia?

Nimetembelea hotel websites na bado unaweza kufanya booking ya chumba:

Hotel Websites:


OCEANIC BAY RESORT

PARADISE RESORT

No comments: