Monday, September 08, 2008

Choo cha Kizungu



Wadau, watu wengi wa third world (dunia ya tatu) wamezoea vyoo vile vya kiasia na vya shimo, au kuchimba dawa porini. Sasa wakikutana na hivi vyoo vya kizungu badala ya kuikalia wanaipanda halafu ndo wanachuchumaa. Matokeo yake ni kuwa lundo unaishia kwenye choo, kwenye miguu au kwenye sakafu. Kwa kweli ni balancing act ya hali ya juu kusimama kwenye choo cha kizungu halafu kulenga!

Sehemu nyingi hapa Marekani zenye watu kutoka nchi za Third World siku hizi wanajaribu kuwaelimisha hao wageni wa hvyo vyoo hata kabla ya kuondoka nchini mwao. Hata kwenye ndege za kimataifa siku hizi kuna kideo cha kuwaelimisha.

10 comments:

Anonymous said...

kinachokatazwa hapo ni kuwa kuchuchumaa juu kunaweza kuvunja hicho choo kwa sababu mtumiaji hutumia nguvu nyingi. unapokaa unarelax na hivyo nguvu huwa kidogo.lkn napenda nitofautiane na wewe kuhusu matumizi ya vyoo hivyo. kuna wazungu wengi tu ktk afisi zao pia hawana ustaarabu na wanakunya juu au chini. tusikubali kuambiwa kuwa third world ndio wenye matatizo hata wao pia. mimi nadhani huo ni ustaarabu wa mtu na sio kuwa katokea nchi gani.

Anonymous said...

Da Chemi unajua nyumbani watu kutoka kijijini inabidi waelimishwe maana wanatumia lakini hawajui kuwa wanatakiwa waziflashi. Wanaacha mzigo hapo hapo.

Anonymous said...

To the contrary Dada Chemi, sababu ya haka ka-tabia kujitokeza ni sababu ya mfumuko wa magonjwa ya ngozi ambayo mengi huambatana na ngozi lepelepe za vibonge wa nchi husika. Pamoja na kuwepo ya tissue maalum za kutandika (kwenye makalio),zinakatika kutokana na ulaini na wepesi wake kwa watuamiaji wengi unalazimisha watumiaji wengine kuachana nazo. Kwa haja namba moja, wakina dada wengi hutuama kama mbuzi, hii yote ni kukwepa hata asilimia sufuni nukta moja uwezekano wa matone ya maji kukutana na utupu wa mtumiaji, haswa kutokana na magonjwa f'lani f'ani (sio ukimwi) kuweza kujipenyeza. Therefore, ni hizi ni jitihada mbadala za kujikinga.

Unknown said...

Da chemi, eti wageni kutoka nchi zinazoendelea (sipendi utumizi wa "third world" ina madharau zaidi) ndo wanatabia ya kuchuchumaa juu ya choo kiasi ambacho hata kibao kimetengenezwa kuwazuia hicho kitendo? Kuna watu kadhaa huku U.S. kutokuwa na ungwana kwa tabia zao na labda isipokuwa wahamiaji kutoka nchi zenye vita waliomo huku (refugees), sioni uwezo wa hiyo tabia kutoka nchi maskini kutendeka sana. Wengi wanaokuja hapa wametoka mjini nchini mwao yenye vyoo vya kizungu tele!

mbu (mkenya aneishi ughaibuni)

Anonymous said...

Hata Bongo unakuta footprints za miguu na ndala kwenye hivyo vyoo vya kizungu. Na kuna washamba. Wanadhani kwa vile choo chc shimo kina mavi 24/7 basi na choo cha kizungu kiwe hivyo hivyo wala hawaflashi!

Anonymous said...

Da Chemi,
Hii picha inabidi ipelekwe UDSM hasa Halls za Campus na Mabibo. Vyoo vimevunjika kwa sababu hii. Sijapata ona tabia mbaya ya matumizi ya choo kama ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar hasa sehemu ya Mlimani, hawa ndio wanajiita wasomi. Hata kama kuna maji na ni choo cha kuchuchumaa lazima wachafue tu! Vyoo vya maeneo ya utawala ni mfano tosha, mwanaume fahari kukojolea ukuta!

Anonymous said...

Da Chemi,
Naona comment ya ya mtu mweusi umeibana. Je umeona italeta mkanganyiko wa fikra.

Hata hizo nakushukuru kwa kazi yako unayoifanya.

Keep up the good work!

NB: Usisahau kumpigia kura Obama, pia alika marafiki na ndugu.

Anonymous said...

Labda nijaribu tena huenda ile haikufika!

HOJA YANGU NI TOFAUTI KIDOGO. KWANI NCHI ZINAZOENDELEA/ MASIKINI ZIKO AFRIKA PEKEE? JE SOUTH AMERIKA, SOUTH EAST-ASIA, NA HATA MAENEO MENGINE YA USA NA UK BADO KUNA UMASIKINI. NA WATU WASIOMUDU KUTUMIA VITU VYA KISASA.

HIVI KARIBUNI KUNA TAKWIMU ZIMEONYESHA KUWA BAADHI YA MAENEO HAPA NCHINI UINGEREZA LIFE EXPECTANCE YAO NI MIAKA 56, OF COURSE MAENEO MENGI NI MIAKA 81.

LAKINI HII INAASHIRIA KUWA WAVUJA JASHO TUPO MAHALA PENGI DUNIANI. SIYO AFRIKA PEKE YAKE.

SWAHI LANGU MUHIMU NI KWANINI HII CARTOON INAONYESHA MTU MWEUSI??????? (LABDA KAMA NI COPY)

SEHEMU NYINGI DUNIANI UTAKUTA MTU MTENDA MAOVU KAMA VILE MWIZI, MCHOMOAJI, MUUAJI, SHETANI. N.K. HUONYESHA / HUCHORWA KWA RANGI NYEUSI. HIVI NI KWA NINI?!

RAFIKI YANGU MMOJA (M-GHANA) HUKO JAPAN, KUNA WAKATI ALIALIKWA KUJIUNGA NA KANISA FULANI.(SINA NIA YA KUKASHIFU DINI. MIMI MWENYEWE NI MUUMINI WA DINI HII) ALIELEKEA KUKUBALIANA NAO. LAKINI SIKU MOJA ALIPOKUWA AKIHUDHURIA MAFUNDISHO... AKASOMA AU KUONA SHETANI AKIWA REPRESENTED KWA RANGI AU JITU JEUSI. ILIKUWA NDIO MWISHO HAKUENDA TENA. NA AKAWAOMBA WAONDOE HIYO PICHA.

IPO HAJA YA KUKEMEA HISIA HII POTOFU. SISI SI MASHETANI, SISI NI WATU.

NAKARIBISHA MAONI.

MDAU LONDON.

Anonymous said...

Dada Chemi, ndio sababu tunakupenda. Unasema ukweli. Hebu wapashe hao wanaojidai wameendelea huko Bongo kumbe hawajui jinsi ya kutumia choo cha kizungu! Khaa!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

si kawaida yako DA chemi kupotea kiasi hiki?

Mzima lakini?

Maana baada ya kumaliza kuchek mail zangu na kablog kangu next huwa naanzia BC,kwako,mjengwa n.k

Natumaini mzima..tuletee mawili matatu nakukosa DA CHEMI